Kagera haki ya kupata msaada wa sheria kwa mtu wa kawaida imeminywa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagera haki ya kupata msaada wa sheria kwa mtu wa kawaida imeminywa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Nov 28, 2010.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa Mkoani Kagera huduma ya msaada wa sheria kwa watu wasio na uwezo haipo. Katika hali hiyo tegemeo la mtu wa kawaida hasiyekuwa na uwezo wa kuajiri wakili msomi na mwenye leseni ilikuwa ni kutumia watu wenye ujuzi wa sheria kwa kuwapa viapo vya uwakilishi. Utaratibu huo ni halali chini ya sheria na ni haki ya msingi kikatiba. Kwa bahati mbaya, hivi majuzi siku ya Ijumaa tarehe 26/11/2010, Mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Bukoba imepiga marufuku utaratibu huo kwa shinikizo la mawakili wenye leseni ambao wanahisi kuwepo kwa watu hao kunawapunguzia biashara. Jambo la kusikitisha ni kwamba uamuzi huo ulifikiwa bila ya wahusika wanao wakilishwa kupewa fursa ya kusikilizwa. Matokeo yake ni kwamba hivi sasa hawajui hatma ya kesi zao zilizokuwa zinaendelea kwa msaada wa hao waliopigwa marufuku.
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Mbunge wako yuko wap? yaani kwa jinsi huo mkoa ulivyo na wanasheria wengi inakuaje hauna wanasheria wenye utaratibu wa bure?
   
 3. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Si unajua tena nchi yetu haki ununuliwa kama bidhaa nyingine!
   
 4. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45

  Hili jambo na mimi nimelisikia kwa kutumiwa SMS na mtu ambaye simu yake haipatikani

  Nitafuatilia jambo hili siku si nyingi nitakuwa na la kusema kupitia media

  Inawezekana kuna issue ya kibishara au vinginevyo.TUSUBIRI KIDOGO

  Byabato
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Money speaks siku izi ndugu zanguni
   
Loading...