Kagera: Dennis Joseph Sebugwao, aliyekuwa Meneja Mkuu wa STAMIGOLD na wenzake watatu, wapandishwa Kizimbani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973

ALIYEKUWA MENEJA MKUU WA KAMPUNI YA STAMIGOLD NA WENZAKE WATATU WAPANDISHWA KIZIMBANI-KAGERA

TAARIFA KWA UMMA

Februari 19, 2021

Ndugu wanahabari,

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera tumeendelea kutekeleza majukumu yetu kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007. Katika utekelezaji wa majukumu yetu tumeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Rushwa wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa serkali na wananchi kwa ujumla. Aidha majukumu haya yametekelezwa katika wilaya zote zilizo chini ya Mkoa wa Kagera.

Ndugu wanahabari,

Tunapenda kuujulisha umma kuwa mnamo tarehe 12/02/2021 tuliwafikisha katika mahakama ya Wilaya ya Biharamulo watuhumiwa wanne ambao ni watumishi wa Kampuni ya Uchimbaji wa Madini - STAMIGOLD kwa makosa ya kujihusisha na vitendo dhidi ya Rushwa na matumizi mabaya ya ofisi chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na na Rushwa , namba 11 ya mwaka 2007 na wamefunguliwa Shauri la jinai lenye namba CC 12/2021.

Ndugu wanahabari,

Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni hawa wafuatao;-

  • Dennis Joseph Sebugwao - ambaye alikuwa Meneja Mkuu (General Manager) wa Mgodi wa STAMIGOLD Co Ltd katika kipindi cha mwaka 2016/2017

  • Bwire Kanyaranyara Eliaseph- ambaye alikuwa Afisa Manunuzi wa kampuni STAMIGOLD Co Ltd katika kipindi cha mwaka 2016/2017

  • Sadick Soud Kasuhya – ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi cha Mgodi wa STAMIGOLD Co Ltd kwa kipindi cha mwaka 2016/2017

  • Clara Aaron Mwaikambo - ambaye alikuwa Mkuu wa Idara ya Fedha wa Kampuni ya STAMIGOLD Co Ltd

Ndugu wanahabari

Uchunguzi wa TAKUKURU mkoa wa Kagera umeweza kuthibitisha kuwa katika kipindi cha kuanzia 30/06/2016 hadi 31/12/2017 kwa nyakati tofauti wakiwa watumishi wa Kampuni ya STAMIGOLD CO. LTD ambayo ni Kampuni tanzu ya kampuni STAMICO (STATE MINING CORPORATION) yenye Makao Makuu yake katika Wilaya ya Biharamulo katika Mkoa wa Kagera walitumia vibaya nafasi zao na kusababisha Kampuni ya SUPERCORE kujipatia manufaa

Ndugu wanahabari,

Watuhumiwa wote kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa Kampuni ya STAMIGOLD kwa nafasi tofauti tofauti katika kipindi cha 30/06/2016 hadi 31/12/2017 walitumia vibaya nafasi zao na hivyo kupelekea kuingiwa kwa Mktababa baina ya STAMIGOLD CO LTD na kampuni ya SUPERCORE wenye thamani ya shilingi bilioni nne milioni mia sita ishirini na mbili elfu laki nne ( Shs 4,622,400,000/=) badala ya shilingi bilioni tatu milioni mia nne elfu tisini na sita elfu (Shs 3,496,000,000/=) na hivyo kupelekea kampuni ya SUPERCORE kujipatia manufaa ya jumla ya shilingi bilioni moja milioni mia moja ishirini na sita laki nne (Shs 1,126,400,000/=)

Ndugu wanahabari,

Baada ya shauri hilo kufunguliwa, Mshitakiwa mmoja ambaye ni Clara Mwaikambo aliweza kupata dhamana na watuhumiwa wengine watatu waliobaki siku hiyo hawakuweza kutimiza masharti ya Dhamana. Hata hivyo washitakiwa wawili ambao ni Dennis Joseph Sebugwao na Bwire Kanyaranyara Eliaseph walifanikiwa kupata dhamana siku ya tarehe 16/02/2021 na Mshitakiwa Sadick Soud Kasuhya bado hajaweza kukidhi masharti ya dhamana hadi leo.

Ndugu wanahabari,

Ikumbukwe kuwa maandiko matakatifu kutoka katika Vitabu vitakatifu hasa BIBILIA na QURAN yametamka bayana kuwa Rushwa ni dhambi, na yamekataza mtu yeyote kujihusisha na vitendo vya Rushwa kwa njia yoyote, hivyo kujihusisha na vitendo dhidi ya Rushwa ni kwenda kinyume na Makatazo ya Mwenyezi Mungu na ni kuharibu uhusiano baina yako ya Mwenyezi mungu.

Hitimisho

Ndugu zangu ni vyema ikaeleweka kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuchukua hatua kila anapoona kuna dalili ya vitendo vya rushwa kufanyika na ni vyema kila mmoja wetu kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi zilizowekwa kwa maslahi mapana ya Taifa. Hivyo nitoe wito kwa Wananchi wote wa mkoa wa Kagera kuchukua hatua mahususi pale wanapoona kuna dalili au ukiukwaji wa sheria zetu za nchi au kuna viashiria vya uwepo wa vitendo vya rushwa.

Signed
JOHN K.E JOSEPH
MKUU WA TAKUKURU (M)
 
Aisee
 
Signed
JOHN K.E JOSEPH
MKUU WA TAKUKURU (M)

YEYE ASIYE NA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KUKUTUPIA JIWE. ( Yoh.8:7 )​

“Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. ” Yoh.8:7-9

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa lugha nyingine Bwana Yesu anawaambia ikiwa kama watu hao hawana dhambi basi wawe wa kwanza kumuhukumu huyo mwanamke. Anawaambia watesi wako siku ya leo kwamba ikiwa kama hawana makosa basi wawe wa kwanza kukuhukumu wewe.
Ndiposa nikajifunza jambo moja kubwa hapo,kwamba;
Hata wenye kukuhukumu wewe,kumbe wao pia wanadhambi za kuhukumiwa,hivyo hawastahili kukuhukumu,pia nikajua kwamba;Usalama wako haupo kwa wanadamu bali usalama wako upo magotini pa Yesu. Ujapowakimbilia wanadamu kwa msaada,msaada wako kamwe hautapitikana kwao,sababu;
Wanadamu wamejaa kuhukumu wakosa hali wao ni wakosaji wakubwa.
 
Siku wakiwakamata Lugola, Makonda na Mnyeti ndiyo nitajuwa kweli wanapambana na rushwa, vinginevyo ni maigizo na uonevu kwa watu wa chini
 
Dennis Joseph Sebugwao namkumbuka toka akiwa Tulawaka... Alikuwa metalligist mzuri sana ila akafukuzwa baada ya kashifa ya ngono alikuwa anapenda totoz balaa... Then.. Basie Maree alimrudisha North Mara as Metalligist Superitndate ghafla kachomokea Stamico as GM kumbe kaenda kula pin Dah pole yake.
 
Na upelelezi ukamilike, msiwaweke ndani watu kwa hisia, ni kuwaumizi huku hamna ushahidi, naona tatizo hilo kwa Seth, mashehe uhamsho, na wengine!
 
Naomba kukumbushwa kesi ambayo hawa TAKUKURU wameshawahi kufunga mtu kiushahidi mbali ya kufungua kesi na wao kugeuka omba omba wa rushwa!
Acheni tu kusumbua watu.
 
Back
Top Bottom