Kagera, Biharamulo: Rushwa yamfikisha Mahakamani Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi(CCM), pamoja na wenzake kumi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa Stamigold ulioko Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

IMG_20180806_140547.jpg

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Biharamulo, Hassan Mosi amesema mbunge huyo na wenzake walikamatwa na kuwekwa rumande katika gereza la wilaya hiyo Jumamosi Agosti 4, 2018.

Amesema leo Jumatatu Agosti 6, 2018 watafikishwa mahakama ya wilaya ya Biharamulo kwa kosa la kufanya miamala ya kupokea rushwa.

Mosi amesema kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha15 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

"Wakifikishwa mahakamani watasomewa mashtaka yanayowakabili. Wanaweza kukiri au kukanusha na sheria itachukua mkondo wake,” amesema.

Ndugu, jamaa na marafiki leo wamejitokeza kwa wingi katika mahakama hiyo, huku wengi wakionekana kuwa na shauku ya kujua hatima ya viongozi hao.

=====

Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wakishtakiwa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Wakizungumza mahakamani leo Jumatatu Agosti 6, 2018 waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dismas Muganyizi na Joseph Mulebya wamesema watuhumiwa hao walifanya miamala ya rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria namba 11 cha mwaka 2007 ya taasisi hiyo.

Amesema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti katika mgodi wa Stamigold ulioko wilayani Biharamulo kati ya Septemba 2015 hadi Oktoba 2016 walitenda kosa la kufanya miamala ya rushwa na kuvunja kifungu cha 15(1) (a&b) cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Flora Ndale, Muganyizi amewataja washtakiwa hao kuwa ni Clara Mwaikambo, Chacha Wambura, Christopher Mwinuka, Sadick Kaswia, Fortunatus Rulemeja, Reginald Haule, Yasini Mohammed, Fabian Ngelela , Felician Edward, Braithony Luchagula na Nchambi.

Amesema Nchambi na Mohammed, Oktoba 2016 walifanya muamala wa rushwa na kumpatia Sh5 milioni mhasibu wa Stamigold co. Ltd ambaye ni Clara kama zawadi ya kupatikana malipo yao ya dola 170,945 za Marekani walizokuwa wakidai katika machimbo ya mgodi huo.

Washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh10milioni, huku mmoja akiwa mtumishi wa umma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3, 2018 itakapotajwa tena.
 
Hiyo rushwa walikuwa wanapokea kwa nani na ili iweje? Isije kuwa ni kuchafuana tu au ana bifu na jiwe.
 
Alikuwa na mabasi yaliitwa Mombasa raha mokonda walikuwa watoto wazuuri yako wapi siku hizi
 
Mbunge wa Kishapu (CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa Stamigold ulioko Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.

View attachment 828391

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Wilaya ya Biharamulo, Hassan Mosi amesema mbunge huyo na wenzake walikamatwa na kuwekwa rumande katika gereza la wilaya hiyo Jumamosi Agosti 4, 2018.

Amesema leo Jumatatu Agosti 6, 2018 watafikishwa mahakama ya wilaya ya Biharamulo kwa kosa la kufanya miamala ya kupokea rushwa.

Mosi amesema kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha15 cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

"Wakifikishwa mahakamani watasomewa mashtaka yanayowakabili. Wanaweza kukiri au kukanusha na sheria itachukua mkondo wake,” amesema.

Ndugu, jamaa na marafiki leo wamejitokeza kwa wingi katika mahakama hiyo, huku wengi wakionekana kuwa na shauku ya kujua hatima ya viongozi hao.
Yaani utakuta limebambwa na rushwa ya milioni mbili au tatu wakati ana uwezo wa kukopa bank hadi milioni 500 na kila mwezi anakula mshahara wa milioni 12 lakini anatolea macho rushwa za milioni mbili au tatu.
 
Mbunge wa Kishapu kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Suleiman Nchambi pamoja na wenzake kumi wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Biharamuro Mkoani Kagera wakikabiliwa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

======

MBUNGE RUSHWA.jpg

Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wakishtakiwa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Wakizungumza mahakamani leo Jumatatu Agosti 6, 2018 waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dismas Muganyizi na Joseph Mulebya wamesema watuhumiwa hao walifanya miamala ya rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria namba 11 cha mwaka 2007 ya taasisi hiyo.

Amesema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti katika mgodi wa Stamigold ulioko wilayani Biharamulo kati ya Septemba 2015 hadi Oktoba 2016 walitenda kosa la kufanya miamala ya rushwa na kuvunja kifungu cha 15(1) (a&b) cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Flora Ndale, Muganyizi amewataja washtakiwa hao kuwa ni Clara Mwaikambo, Chacha Wambura, Christopher Mwinuka, Sadick Kaswia, Fortunatus Rulemeja, Reginald Haule, Yasini Mohammed, Fabian Ngelela , Felician Edward, Braithony Luchagula na Nchambi.

Amesema Nchambi na Mohammed, Oktoba 2016 walifanya muamala wa rushwa na kumpatia Sh5 milioni mhasibu wa Stamigold co. Ltd ambaye ni Clara kama zawadi ya kupatikana malipo yao ya dola 170,945 za Marekani walizokuwa wakidai katika machimbo ya mgodi huo.

Washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh10milioni, huku mmoja akiwa mtumishi wa umma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3, 2018 itakapotajwa tena.

Chanzo: Mpekuzi
 
Anayekula nyama ya mtu haachi - JK NYERERE

Taarifa kutoka Kagera zinasema Yule Mwarabu wa kisukuma ambaye pia ni mbunge wa kishapu kwa tiketi ya ccm ndugu Nchambi amedakwa kwa tuhuma za rushwa , hivi hizi kesi za rushwa za wabunge wa ccm zinaishaje ? mnakumbuka kesi ya rushwa ya Kangi Lugora ilikoishia ?
KAGERA_ Mbunge wa Kishapu(CCM), Suleiman Nchambi na viongozi watatu wa mgodi wa .jpg
 
Back
Top Bottom