KAGERA: Aliyemuua mke wake kikatili Kagera atiwa mbaroni

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
773
1,000
Jeshi la polisi mkoani Kagera limefanikiwa kumtia mbaroni Sendon Andrew mkazi wa kijiji cha Byamtemba kilichopo katika kata ya Nsunga iliyoko wilayani Misenyi mkoani Kagera aliyekimbilia nchi jirani ya Uganda kwa tuhuma ya kumuua kikatili mke wake Rosemery Desdery kwa kumpigwa fimbo na mateke katika seheme mbalimbali za mwili wake.

Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera mrakibu mwandamizi wa jeshi hilo Abel Mtagwa ambaye pia ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa mkoa huo,amesema mtuhumiwa huyo baada ya kufanya mauaji hayo kwenye eneo la Sebure ya nyumba yao alimburuza marehemu hadi kwenye chumba chao cha kulala na kumfunika na blanketi na wakati akitoroka aliwambia watoto wao kuwa amemuacha mama yao amelala na anaondoka atarudi kesho yake.

Kaimu kamanda huyo akitoa wito kwa wananchi amesema jeshi hilo halitawavumilia mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya mauaji kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na taratibu na sheria za nchi.
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,381
2,000
Bora wawakamate. Kule kanda maalum huwa kimya kimya. Wengi wanafanyiwa ukatili hasa.
 

jozzeva

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,198
2,000
dah sasa sijui kisa kilikuwa nini mpaka akaamua kufanya mauaji hayo ya kinyama?
 

Sagungu 1914

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
829
500
Watu wengine bwana sijui huwa bangi? Unawezaje kumuua mke wako ambaye ulimtongoza kwa mbwembwe zote kipindi cha ujana wenu?.Basi afungwe tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom