Kagera: Ajali yaua watu nane wakiwemo watano wa familia moja Julai 12, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,875
POLISI.jpg
Watu wanane wamefariki Dunia watano wakiwa wa familia moja baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika Barabara Kuu ya kutoka Lusahunga kwenda Nyakahura Wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera, usiku wa kuamkia leo Julai 12, 2022.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema miongoni mwa watu hao waliofariki wamo watano wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wanne.

Kamanda Mwampaghale amesema ajali hiyo imehusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea Nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala Wilayani Biharamulo kuelekea Benaco Wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye naye aliyefariki katika ajali hiyo.

Amesema pia abiria wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed walipoteza maisha, majina yao ni Nyawenda Bisalo (35), Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).

Kwa mujibu wa Kamanda Mwampaghale uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, na kusababisha magari hayo kugongana uso kwa uso.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi kilichoko wilayani Biharamulo.

Amesema dereva wa lori, Vicent Gakuba alitoroka baada ya ajali hiyo ila Polisi walifanikiwa kumkamata baada ya muda mfupi katika kizuizi cha Kahaza mpakani mwa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, akiwa katika Lori lililokuwa likielekea Nchini Rwanda na atafikishwa Mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
 
Zamani kulikuwa na Vibao vikiwakumbusha Madereva kuwa watembelee kushoto na ukiingia Rwanda kulikuwa na Vibao vinavyokumbusha Madereva watembelee kulia.

Vile vibao vilikuwa vimewekwa kwa Kilomita 50.

Ni rahisi kwa Dereva kusahau na kufikiri kuwa bado yuko Rwanda. au Tanzania.
 
Hapo hapo hapo walevi wa malori na mabasi wanalalamika wanabanwa barabarani...nikiwa Rais Mimi ndani ya kipindi changu usilalamike Kama unaona unacholalamika kinaweza kukuletea matatizo mwenyewe
 
Watu wanane wamefariki Dunia watano wakiwa wa familia moja baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika Barabara Kuu ya kutoka Lusahunga kwenda Nyakahura Wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera, usiku wa kuamkia leo Julai 12, 2022.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema miongoni mwa watu hao waliofariki wamo watano wa familia moja ambao ni mama na watoto wake wanne.

Kamanda Mwampaghale amesema ajali hiyo imehusisha gari la mizigo lililokuwa likitokea Nchini Rwanda kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Vicent Gakuba (52) raia wa Rwanda na Toyota Succeed lililokuwa likitokea eneo la Nyamalagala Wilayani Biharamulo kuelekea Benaco Wilayani Ngara likiendeshwa na Nyawenda Bihela (35) ambaye naye aliyefariki katika ajali hiyo.

Amesema pia abiria wote waliokuwa katika gari aina ya Toyota Succeed walipoteza maisha, majina yao ni Nyawenda Bisalo (35), Jesca Leonard (45), Magreth Sekanabo (14), Adidas Sekanabo (12), Zabron Sekanabo (6), Vedastina Sekanabo (8), Michael Charles (28) na Majaliwa Kanundo (32).

Kwa mujibu wa Kamanda Mwampaghale uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Lori kutokana na kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara na kuendesha gari upande wa kulia, na kusababisha magari hayo kugongana uso kwa uso.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, katika kituo cha afya Nyakanazi kilichoko wilayani Biharamulo.

Amesema dereva wa lori, Vicent Gakuba alitoroka baada ya ajali hiyo ila Polisi walifanikiwa kumkamata baada ya muda mfupi katika kizuizi cha Kahaza mpakani mwa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, akiwa katika Lori lililokuwa likielekea Nchini Rwanda na atafikishwa Mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
Moyo unauma aisee.

Mungu awape ujasiri wanafamilia waweze kulibeba hili jaribu.

R. I. P.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom