Kagasheki: Vigogo wanahusika biashara ya pembe za ndovu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
KITAIFA

Na Mwandishi Wetu


Posted Jumapili,Novemba18 2012 saa 9:10 AM


KWA UFUPI


"Napenda sasa kutangaza vita na wale wote wanaohusika katika biashara hii haramu, nitapambana nao. Hali hii inanifanya niamini kuwa kuna mkono wa vigogo katika mtandao huu," alisema Kagasheki


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema kuna mkono wa vigogo katika biashara haramu ya pembe za ndovu na kuahidi kuwa atapambana nao hadi mwisho.

Kauli hiyo ya Kagasheki inakuja siku chache baada ya shehena kubwa ya pembe za ndovu kukamatwa na maofisa usalama nchini Hong Kong ikitokea Tanzania.


Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti dada la Mwananchi la The Citizen, Balozi Kagasheki alithibitisha kuwa pembe hizo zenye thamani ya Sh2.4 bilioni zilitokea nchini na kusema inaonekana kuna mkono wa watu wazito katika biashara hiyo.

Aliwashukia maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuwa hawakuchukua hatua stahili katika kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu na kuongeza kuwa ni jambo lisiloingia akilini mzigo mkubwa kama huo upakiwe nchini bila mamlaka husika kujua.

"Napenda sasa kutangaza vita na wale wote wanaohusika katika biashara hii haramu, nitapambana nao. Hali hii inanifanya niamini kuwa kuna mkono wa vigogo katika mtandao huu," alisema Kagasheki na kuongeza:

"Uchunguzi wetu hautamwacha mtu hata mmoja na hatua za kisheria zitachukuliwa."
Aliongeza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, atafanya mabadiliko makubwa katika Idara ya Wanyamapori, mapori ya akiba na hifadhi za taifa.


Kwa mujibu wa Waziri Kagasheki, ameshawasiliana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na wamekubaliana kuunda timu itakayofanya uchunguzi wa suala hilo.
Kuhusu pembe hizo zilizokamatwa, Kagasheki alisema alipata taarifa kutoka Dubai zilizothibitisha kuwa shehena hiyo ilitoka Tanzania na hati za mzigo huo zilionyesha kuwa makontena hayo yalikuwa yamebeba alizeti kutoka Tanzania kwenda Dubai.


Alisema kuwa pembe 569 zilikamatwa kutoka katika makontena hayo na hivyo, ikamaanisha kuwa zaidi ya ndovu 150 waliuawa nchini.

Maofisa wa Forodha wa Hong Kong walikamata zaidi ya tani moja ya pembe za ndovu zenye thamani ya Dola za Marekani 1.37 milioni katika soko la pembe za ndovu nchini China.

"Pembe hizo zilikuwa zimefichwa pamoja na bidhaa nyingine. Kulikuwa na magunia 400 ya mbegu za alizeti zilizotumika kuficha ukweli," alisema Mkuu wa Komandi Baharini na Bandari wa Hong Kong, Wong Sui-hang.

Alisema pembe hizo zilisafirishwa kutoka Tanzania kwa meli kabla ya kupakiwa kwenye meli nyingine zilipofikishwa Dubai na kuanza kusafirishwa kwenda Hong Kong.

Oktoba mwaka huu, maofisa usalama nchini China walikamata karibu tani nne za pembe za ndovu zenye thamani ya Dola 3.4 milioni zilizosafirishwa kutoka Tanzania na Kenya.

Baada ya shehena hiyo kukamatwa, gazeti dada la The Citizen liliripoti kuwa uchunguzi uliofanywa na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ulibaini kuwa kuna Watanzania wanne waliohusika katika usafirishaji wa pembe hizo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari kutoka Interpol, watu hao walibainika baada ya polisi kufanya mahojiano na watuhumiwa kwa siku tatu huko Guangdong, China na kuongeza kuwa waliwasiliana na Tanzania wakitaka watu hao wakamatwe.





 
wa kwanza ni KINANA na yeye mwenyewe kakubali kuwa meli ni zake. Yeye sio mjinga kuwa atakubali kuwa mzigo ni wake
 
VIGOGO ni VIONGOZI wa NDANI wa CCM; Inasikitisha... HALAFU kila MTU NDANI ya CCM wanahubiri dhidi ya UFISADI kumbe ndio WENYEWE wezi wa MALI za TAIFA

Na Wamepewa VYEO na CHAMA TAWALA... Na Wanajuana... SHIDA kuwataja!!!
 
Hata maige alisema vigogo wanahusika kwenye biashara hiyo lakin mpaka leo kagasheki anapotamka maneno yaleyale hatujamwona kigogo yeyote kukamatwa wala kuchukuliwa hatua zaid twashuhudia vipusa vikikamatwa daily hongkong, ths absurd!!
 
Analalama nini achukue hatua ya kuwataja kama na yeye ajatoswa hakuna aliyemsafi ccm!
 
wa kwanza ni KINANA na yeye mwenyewe kakubali kuwa meli ni zake. Yeye sio mjinga kuwa atakubali kuwa mzigo ni wake
acheni utoto nyie kwani uiwa na dala dala yako ikakamatwa kwa kuiba route au kuvunja sheria yeyeote barabarani unatakiwa ukamatwe au kuhukumiwa wewe?heb tuache ushabiki na tuwe fair sometimes
 
Acha kuzunguka bw. Kaga mi naamini pa kuanzia unapajua, Kinana ameshakubali meli ni zake basi huyu atakuwa ndo miongon mwa vigogo unaowazungumzia kama kweli una nia ya dhati kukomesha ujangili huu unaofanywa na katibu wenu, dili na huyu na wengine atataja
 
Hii nchi maneno yashakuwa kibao hadi yamechosha, kila kukicha ni maneno tuuuuuuu na ahadi zisizotekelezeka! Mara ngapi ameahidi kufanya hayo anayoahidi kuyafanya tena?
 
Achukue hatua aache kulalamika, fuata nyayo za Mwakyembe acha kulemba, kagasheki analalamika je mwananchi wa kawaida afanye nn? Nazidi kuchoshwa na magamba unadhani kwann Kinana kapewa nafasi ile siyo bahati mbaya ili kulinda mali ukiwa katibu mkuu waziri hawezi kukuchunguza bongo hata kama kesi ya ugoni wote watakanusha, ndiyo maana hata wanaoshikwa na pccb wanaachiwa ili kukinusuru chama na kukanusha haraka ni uzushi mwenye ushahidi autoe.
 
Tatizo la viongozi wa ccm ni kuongea tu hakuna hatua zozote za mana watachukua! Huyu kagasheki anaongea tu wala hakuna la maana atakalolifanya, anajua sisi watz tunajua kusifia kwa matamko, hivi ndani ya ccm kuna nani msafi? Hata prof muhingo aliingia kwa speed 120, yuko wapi? chezea magamba wewe!!!!! Ukijiunga nao hata kama zilikuwa zinakutosha, zitakupungua tu!
 
KINANA- PEMBE ZA NDOVU N.K., Mangula-EPA nk, JK-Richmond,EPA nk, Nchemba-muuaji, Nape-Vuvuzela. CCM wote majizi
 
Hivi kigogo ni nani?

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
pcman,
Am always cracking to know who the KIGOGO thing is all about. Unakumbuka hata Pinda aliwahi kusema mafisadi wakikamatwa Nchi itayumba,ati ni Vigogo..Yaani Wezi wanatukuzwa kiasi hiki Tanzania? Haki ya Mungu,sometime nalaani kuzaliwa Nchi ya kipuuzi kama hii. Bullshit!
 
Last edited by a moderator:
kigogo wa kwanza ni kinanda haiwezekani ana kampuni ya meli asijue amebeba nini,huyu ni mzoefu kwenye hii deal ya pembe za ndovu!!!napata uchungu sana ninapomuona mtu anayeshabikia haya magamba bila kujua muda si mrefu watoto wetu watamsoma tembo kama historia kama ilivyo kwa wale dinosor!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom