Kagasheki: Tanzania haiko chini ya utawala wa kijeshi. Askari kumtolea bastola raia.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,459
2,000
Anaandika aliyekuwa Mbunge na Waziri wa Maliasi na Utalii Mhe Khamis Kagasheki Tanzania haiko chini ya utawala wa kijeshi. Askari kumtolea bastola raia ambaye hana silaha yoyote, haikubaliki na si kitendo cha kufurahia.
tmp_12462-IMG_20170323_223106678596951.jpg

My take ==
Mara nyingi sana tumezomea kuona Jeshi la Polisi wakitumia nguvu kubwa sana kupambana na upinzani kuliko kutumia akili au njia sahihi katika kutimiza wajibu wao huo.
Kitendo ambacho kimefanywa leo na Afisa wa Jeshi la Polisi kuonyesha bastola hadharani kinatakiwa kulaani na kupingwa kwa nguvu zote.
Jamaa kaambiwa na Nape Onyesha Kitambulisho Katoa Bastola, sasa akiambiwa onyesha cheti si atatoa Bomu!!
 
Attachments

  • tmp_12462-Screenshot_2017-03-23-22-19-30167157881.png
    File size
    372.1 KB
    Views
    90

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,459
2,000
.
Mara nyingi sana tumezomea kuona Jeshi la Polisi wakitumia nguvu kubwa sana kupambana na upinzani kuliko kutumia akili au njia sahihi katika kutimiza wajibu wao huo.
Kitendo ambacho kimefanywa leo na Afisa wa Jeshi la Polisi kuonyesha bastola hadharani kinatakiwa kulaani na kupingwa kwa nguvu zote.
 
Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,138
2,000
Najiuliza wakati nape alipokuwa katibu mwenezi ccm je hakuwahi kupanga mipango yoyote ya jinsi ya kuwadhibiti wapinzani, ikiwemo kutumia nguvu ya dola???.
OK
Kama jibu ni ndio basi wacha nayeye aonje joto walio onja wapinzani kama alivyo fanyagwa Lipumba kabla haja badilika na kupoteza dira.
 
Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,459
2,000
Ameshiriki mipango mingi sana kuimaliza upinzani lakini hayo tuache tujadili nguvu kubwa sana ya Jeshi la Polisi inayotumiwa kwenye mambo ambayo hayataji nguvu hiyo
Najiuliza wakati nape alipokuwa katibu mwenezi ccm je hakuwahi kupanga mipango yoyote ya jinsi ya kuwadhibiti wapinzani, ikiwemo kutumia nguvu ya dola???.
OK
Kama jibu ni ndio basi wacha nayeye aonje joto walio onja wapinzani kama alivyo fanyagwa Lipumba kabla haja badilika na kupoteza dira.
 
kizwezwe

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
985
1,000
KWANI BASTORA inatakiwa kuoneshwa wapi? ukizingua hata hadharani inatoka tuu nyie karirini hivyo vi sheria halafu mje mzingue .
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,935
2,000
Ni kweli ulichokisema.

Lakini mwanausalama alikuwa 'calm' tena aliongea kwa upole 'Mheshimiwa rudi kwenye gari..', Wakati huo Mh. Nape akiwa amevaa shati bila kuchomekea na ameweka mikono yote mifukoni (kulia na kushoto); baadaye anasikika (Nape) akimwambia mwana usalama " ....usinishike hivyo Bwana, ondoka" wakati huo anamsukuma mwanausalama kwa mkono wa kushoto lakini mkono wake wa kulia ukiwa bado humo mfukoni; kwa akili za kawaida...askari lazima ajihami maana huo mkono wakulia wa Nape ambao umo mfukoni hajui umeshika nini. Na hata Nape alivyosukumwa sukumwa hakutoa mkono huo wa kulia mpaka (labda) alipohakikisha kuwa sasa mfuko wa kulia wa suruali lake umezibwa na gari ndipo alipotoa mkono mfukoni. Na watu wakaongezeka pale...!

Naliona hivyo tukio hili. Lakini maelezo mazuri anaweza kuyatoa mwanausalama mwenyewe kwa nini alifanya vile.
 
illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,275
2,000
.
Mara nyingi sana tumezomea kuona Jeshi la Polisi wakitumia nguvu kubwa sana kupambana na upinzani kuliko kutumia akili au njia sahihi katika kutimiza wajibu wao huo.
Kitendo ambacho kimefanywa leo na Afisa wa Jeshi la Polisi kuonyesha bastola hadharani kinatakiwa kulaani na kupingwa kwa nguvu zote.
Nani aliyekwambia wale walikuwa maofisa wa jeshi la polisi mi niliona ni kama wahuni wenye silaha
 
roboka kafwekamo

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
823
500
Utawala wa idd amin ulikuwa hivi nyerere akawasaidia kueatolea madarakani .

Leo rais wa tanzania ANAGANDAMIZIA utawala wa mtu alipokea utawala kutoka kwa iliyosaidiwa na tz haaaa.
 
Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,549
2,000
Kabla ya jua halijachomoza atakuja hapa kuikana hiyo account kama sio yake subirini tu, ccm kwa unafiki hawajambo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom