Kagasheki nauliza, “unatetea vipi kontena lenye meno ya ndovu na origin yake ni Dar?”

palalisote

JF-Expert Member
Aug 4, 2010
8,335
1,455
Unaieleza vipi, na unatetea vipi, kontena lenye meno ya ndovu, wanakwambia kwamba origin yake ni bandari ya Dar es Salaam? Pale bandarini, kuna vyombo mbalimbali --kuna polisi, kuna customs TRA, kuna watu wa pori wenyewe, kuna watu wa usalama, na kadhalika -- kontena linatoka na meno ya ndovu, linakwenda kukamatiwa Hong Kong, linakwenda kukamatiwa Philippines, linakwenda kukamatiwa Vietnam. Kama yapo masuala ya msingi jamani tujiulize, kontena linatokaje? Utaratibu ni upi wa kontena kutoka nchini? Tusaidiane. It is risky, kuna pesa nyingi, lakini some people inabidi wafanye wanavyoweza kufanya for the future of the country, lakini pia, vizazi vijavyo vitatuhukumu kwa...

Last edited by a moderator:
Hiyo maswali itabidi watetezi wa kinanna wajiulize...zaidi ya mara kumi kabla ya kumtetea...ila kama unamtetea kwasababu ya njaa...hutaweza kujiuliza hayo maswali...!!!
 
Nani wa kumuuliza? kwababu wananchi wameuliza hili kupitia wawakilishi wao Bungeni, akatumwa haraka sana Nchimbi kujibu kisiasa. Mimi naamini Uhujumu wa Uchumi wetu una baraka zoote kutoka Jakaya Mrisho Kikwete, kwasababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii na vyombo vyoote vya Usalama vinapokea maagizo yake,

Haingii akilini eti Twiga anapakiwa kwenye Ndege Airpot alafu Polisi, Jeshi na Hata Usalama wa Taifa usijue, hii ishu siyo ya watu wadogo wadogo kama akina Kinana kama Kinana as an individual ni Ishu imepangwa vizuri na viongozi wakuu wa nchi ili kuhujumu Nyara za Serikali,

Hebu tujiulize Ili upakie Twiga pale uwanja wa ndege unatakiwa uhonge watu wangapi ili iwe profitable??? ili uvushe Contena la meno ya Ndovu toka porini mpaka Bandarini inatakiwa uhonge watu wangapi ili liwe Profitable??? Ninavyoamini mimi ni mkuu wa nchi mwenye mamlaka ya kuwaagiza wakuu wa vyombo vya usalama kutokufuatilia kontena husika, kama tulivyoambiwa haitakiwi kuchunguza ufisadi wa Meremeta kwani ulikuwa ni mradi wa usalama wa Taifa ilihali usalama wa Taifa hawafanyi biashara, nina hasira sana na viongozi wetu Mungu aniepushie mbali nisije nikachukua sheria mkononi
 
Aisee na yeye hajui! CCM wakiamua uonekane ---- wanaweza. Uongozi CCM ni kama mbio za rilei anayakupa kijiti hata kama kakipaka mavi kuuliza akakwambia ukweli ni ngumu. Atasingiziwa wa kwanza naye atamrushia wa pili na kuendelea.
 
Kontena lenyewe lemebebwa na mwenyekiti wa chama chetu cha mafisadi halafu hatujui ni la nani!
 
Tusipofanya mabadiliko makubwa nchi hii tutaendelea kushuhudia wizi huu unaofanywa na wakubwa kila siku na kushuhudia wanao kwenda magereza ni walalahoi. Taratibu zipo wazi kabisa pale bandarini kwamba mpaka mzigo upite ni lazima ufuate hatua zote. Lazima documents za mzigo husika zitaonyesha zilikuwa logged lini, nani alizikagua na kuzipitisha, Agent, n.k. Sasa leo unapoambiwa mzigo umetoka Dar es salaam, Tanzania halafu huku kwetu hatuna records, kweli ukiwa na akili unaweza kuelewa hiyo?

Tumeshuhudia yule Mkurugenzi wa Wanyamapori (Obedi Mbangwa) aliyesimamishwa kwa tuhuma za kuidhinisha vibali vya kuuza Twiga na wanyama wengine akirudishwa kazini, je ni nani aliyetoa vibali vile? Mhe Kagasheki kama kweli wewe nimzalendo wa kweli, tungefurahi na kukusifu kama ungesimama na hakikisha ukweli unajulikana. Sasa kama ni mkubwa wako utaweza kujitoa mhanga?

Jamani Tembo wanakwisha, mafisadi tuliowapa nyadhifa sasa wameamua kubebana na kufanya wanachotaka na ndio wanatumalizia wanyamapori wetu.
 
Unaieleza vipi, na unatetea vipi, kontena lenye meno ya ndovu, wanakwambia kwamba origin yake ni bandari ya Dar es Salaam? Pale bandarini, kuna vyombo mbalimbali --kuna polisi, kuna customs TRA, kuna watu wa pori wenyewe, kuna watu wa usalama, na kadhalika -- kontena linatoka na meno ya ndovu, linakwenda kukamatiwa Hong Kong, linakwenda kukamatiwa Philippines, linakwenda kukamatiwa Vietnam. Kama yapo masuala ya msingi jamani tujiulize, kontena linatokaje? Utaratibu ni upi wa kontena kutoka nchini? Tusaidiane. It is risky, kuna pesa nyingi, lakini some people inabidi wafanye wanavyoweza kufanya for the future of the country, lakini pia, vizazi vijavyo vitatuhukumu kwa...

Naamini huko CCM kuna aina fulani ya uenda wazimu hivi!!??? Kwa nini Kagasheki maswali hayo haku muuliza Nchimbi kule Bungeni alipokuwa mishipa imemtoka kutetea hayo Makontena ya Pembe za Ndovu?

Anakuja uraiani kutafuta huruma ya wananchi wakati ana nafasi ya kuuthihirishia Umma wa waTanganyika kwamba nani anapaswa kuwajibika kuhusu kashfa hii!

Cha ajabu ni kwamba hata hakuomba uthibitisho kutoka kwa Mh. Mch. Msigwa juu ya sakata hili na badala yake walimshambulia kwa matusi na kuidhalilisha fani yake ya Utumishi wa Mungu. na pia kuwakashifu wale wanaoongozwa na Mh. Mch. Msigwa kwa kumwambia kwamba ni Mchungaji wa Nguruwe.

Leo hii anakuja na maneno ya kujipendekeza kwa waTanganyika wakati ni unafiki mtupu.

Wao wasubiri kuwajibika kwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia Tanganyika hasara ya matrilioni ya fedha 2015.
 
Last edited by a moderator:
Ccm imechoka kufikiri. Wa Tz tubadilike tuachane na haya majizi ccm. Mwanzoni kinana alisema vilivyokuwa vimebebwa kwenye kontena ni plastiki iliyosagwa sasa anasema hajui, sasa huyu si mwendawzaimu? Wa tz sasa hivi hawadanganyiki.
 
Nani wa kumhoji,waliomtuma ni Mwenyekiti na katibu wa chama kinachoongoza nchi kwa sasa'
 
Nani wa kumuuliza? kwababu wananchi wameuliza hili kupitia wawakilishi wao Bungeni, akatumwa haraka sana Nchimbi kujibu kisiasa. Mimi naamini Uhujumu wa Uchumi wetu una baraka zoote kutoka Jakaya Mrisho Kikwete, kwasababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii na vyombo vyoote vya Usalama vinapokea maagizo yake,

Haingii akilini eti Twiga anapakiwa kwenye Ndege Airpot alafu Polisi, Jeshi na Hata Usalama wa Taifa usijue, hii ishu siyo ya watu wadogo wadogo kama akina Kinana kama Kinana as an individual ni Ishu imepangwa vizuri na viongozi wakuu wa nchi ili kuhujumu Nyara za Serikali,

Hebu tujiulize Ili upakie Twiga pale uwanja wa ndege unatakiwa uhonge watu wangapi ili iwe profitable??? ili uvushe Contena la meno ya Ndovu toka porini mpaka Bandarini inatakiwa uhonge watu wangapi ili liwe Profitable??? Ninavyoamini mimi ni mkuu wa nchi mwenye mamlaka ya kuwaagiza wakuu wa vyombo vya usalama kutokufuatilia kontena husika, kama tulivyoambiwa haitakiwi kuchunguza ufisadi wa Meremeta kwani ulikuwa ni mradi wa usalama wa Taifa ilihali usalama wa Taifa hawafanyi biashara, nina hasira sana na viongozi wetu Mungu aniepushie mbali nisije nikachukua sheria mkononi
Mkuu mvaa Tai hata ukimwangalia kagasheki anavyoongea anaonekana kama kustuka kwamba hii ishu itakua kubwa kumzidi yeye...ila naamini ipo siku tuu mambo yatakuja kuwekwa wazi...
 
Nani wa kumuuliza? kwababu wananchi wameuliza hili kupitia wawakilishi wao Bungeni, akatumwa haraka sana Nchimbi kujibu kisiasa. Mimi naamini Uhujumu wa Uchumi wetu una baraka zoote kutoka Jakaya Mrisho Kikwete, kwasababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii na vyombo vyoote vya Usalama vinapokea maagizo yake,

Haingii akilini eti Twiga anapakiwa kwenye Ndege Airpot alafu Polisi, Jeshi na Hata Usalama wa Taifa usijue, hii ishu siyo ya watu wadogo wadogo kama akina Kinana kama Kinana as an individual ni Ishu imepangwa vizuri na viongozi wakuu wa nchi ili kuhujumu Nyara za Serikali,

Hebu tujiulize Ili upakie Twiga pale uwanja wa ndege unatakiwa uhonge watu wangapi ili iwe profitable??? ili uvushe Contena la meno ya Ndovu toka porini mpaka Bandarini inatakiwa uhonge watu wangapi ili liwe Profitable??? Ninavyoamini mimi ni mkuu wa nchi mwenye mamlaka ya kuwaagiza wakuu wa vyombo vya usalama kutokufuatilia kontena husika, kama tulivyoambiwa haitakiwi kuchunguza ufisadi wa Meremeta kwani ulikuwa ni mradi wa usalama wa Taifa ilihali usalama wa Taifa hawafanyi biashara, nina hasira sana na viongozi wetu Mungu aniepushie mbali nisije nikachukua sheria mkononi

MAMA MDOGO! mbona unajichanganya sana?? kama mkuu wa mchi anahusika! huwezi kuuliza eti ni watu wangapi wamehongwa,,,,,, mkuu wa nchi anatoa amri tuu na sio hongo. ukishaweka kauli ya HONGO tafadhali ondoa neno MKUU WA NCHI. Mbururaaaa weweeeeeee
 
Back
Top Bottom