Elections 2010 Kagasheki kugombea au kutogombea tena 2010?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Mjini, Hamis Kagasheki, ametangaza kutogombea ubunge katika uchaguzi mkuu mwakani.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano hivi karibuni mkoani Kigoma, kabla ya kuanza kwa ziara ya kukagua kambi mbalimbali za wakimbizi ambazo zimefungwa na zinazohitajika kufungwa kutokana na nchi walizotoka kwa sasa kuwa na hali ya utulivu, alisema hatogombea tena ubunge kwa sababu ana mambo mengi ya kufanya.

Kagasheki ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2005 alipata ushindani mkubwa kutoka kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare, alisema hawezi kufanya kazi kwa presha huku kukiwa na kazi nyingine za kufanya ambazo hazina presha.

Alisema anaweza kuwa mtumishi mzuri wa jamii iwapo atafanya kazi bila msukumo kuliko hivi sasa akiwa mbunge ambapo amekuwa akiishi kwa presha.

“Kwa kweli ubunge sigombei tena, hiyo ni kazi ya presha, kila wakati unakuwa roho juu, lakini nimeona kuna kazi nyingine ambayo pia naweza nikafanya ya kuhudumia jamii bila ya kuwa na presha kama hii ambayo kwa sasa naifanya,” alisema Kagasheki.

Alisema baada ya kumaliza kipindi chake cha ubunge mwaka 2010, atafanya shughuli nyingine ambazo ni muhimu kwa taifa, na kwamba atajitolea kuhudumia jamii kupitia kazi nyingine na si ubunge.

Akizungumzia kuhusu kuzagaa kwa silaha katika Mkoa wa Kigoma, hasa katika Wilaya ya Kibondo, alisema kuwa watajipanga kuhakikisha kuwa kunadhibitiwa.

Aidha, alikiri kuwapo na ukosefu wa vitendea kazi akitolea mfano wa magari, mafuta pamoja na vituo vya polisi, ambapo alikiri inaweza ikawa sababu kubwa ya kuongezeka kwa matukio ya ujambazi.

Source: Tanzania Daima.

Bila shaka Kagasheki amesoma alama za nyakati.

Si siri Wilfred Lwakatare wa CUF anakubalika zaidi Bukoba mjini kama si nguvu za dola kutumika vibaya Bwana Kagasheki asingekuwa mbunge.
 
Last edited by a moderator:
- Hela za Geneva zitakuwa zimeanza kumuishia, halafu Bukoba sio mchezo ameshajua kuwa tayari hana ubavu wa kuwashinda wapinzani, alitaka uwaziri wa nje lakini hakuwa mtandao in full hawakumpa, sasa anataka ubalozi akarudishe hela zake nyingi azizopoteza kwenye last ubunge, watch!

FMES!
 
Bora lakini siyo king'ang'anizi kama wengine. Tungoje tuone sasa kama hata gombea kweli maana Msekwa nae hivyo hivyo akasema anastaafu nikashanga mu yupo kwenye kinyang'anyiro cha uspeaker.
 
Kwa hiyo hii danganya toto tu. Kashajua ubunge kuupata ni vigumu sasa anataka kutafuta maslahi sehemu nyingine. Ila sishangai sana, hawa viongozi wetu hawastaafu bali wana hama hama tu sehemu za kutu fisadi.
 
mambo ya ndani si maskhara hasa ukizingatia boss wako ndio huyo Lau...:)
 
Bora lakini siyo king'ang'anizi kama wengine. Tungoje tuone sasa kama hata gombea kweli maana Msekwa nae hivyo hivyo akasema anastaafu nikashanga mu yupo kwenye kinyang'anyiro cha uspeaker.

- Msekwa alisema hagombei tena ubunge na hajagombea mbona unachanganya facts kwa makusudi?

- La ung'ang'anizi una maana kama Kagasheki ameishiwa hela za kununua ubunge, basi wengine wote ambao hawakununua ubunge nao wajitoe kama yeye? Mkapa hakuwa king'ang'anizi akaachia urais kilichobadilika ni nini hasa?

- Halafu vipi zile mbio zako za kugombea hilo jimbo au jamaa walikuwa wanakupakazia tu?

Respect.

FMES!
 
Kwa hiyo hii danganya toto tu. Kashajua ubunge kuupata ni vigumu sasa anataka kutafuta maslahi sehemu nyingine. Ila sishangai sana, hawa viongozi wetu hawastaafu bali wana hama hama tu sehemu za kutu fisadi.

Mnafiki huyo baharia usimwamini, ana mid age crisis basi hujifanya much know kutafuta recognition.

Hebu muulize Malecela atang'atuka lini ubunge? Na kama aking'atuka na yeye ananyemelea ubalozi?
 
Last edited by a moderator:
Kwani 2005 Pius Msekwa hakua kwenye kinyanganyiro cha kuwania uspeaker wa bunge tena? Kama nime kosea basi samahani siyo kupotosha facts makusudi.
 
Kwani 2005 Pius Msekwa hakua kwenye kinyanganyiro cha kuwania uspeaker wa bunge tena? Kama nime kosea basi samahani siyo kupotosha facts makusudi.

Na wewe mtu mzima samahani zako zinabore, LOL.

ACHA NIDHAMU YA UOGA. Haigopwi huyo much know, alishapoteza marbles zamani.
 
Mnafiki huyo usimwamini, ana mid age crisis basi hujifanya much know kutafuta recognition
.

- Ala Kagasheki kumbe ni mnafiki? au ni wewe ndiye mnafiki unajisema? Labda ufafanue kidogo hapo mkuu?

Hebu muulize Malecela atang'atuka lini ubunge? Na kama aking'atuka na yeye ananyemelea ubalozi?
- Malecela hana sababu ya kung'atuka maana wananchi wa jimbo lake bado tunaridhka naye, na hajasema anataka kutoka kama Kagasheki kwamba anatafuta ubalozi., au?

Ahsante.

William.
 
Kwani 2005 Pius Msekwa hakua kwenye kinyanganyiro cha kuwania uspeaker wa bunge tena? Kama nime kosea basi samahani siyo kupotosha facts makusudi.

Alisema hatagombea uSpika, lakini akagombea tena akisema kuna kazi anataka kumalizia, akapigwa chini.
 
Kwani 2005 Pius Msekwa hakua kwenye kinyanganyiro cha kuwania uspeaker wa bunge tena? Kama nime kosea basi samahani siyo kupotosha facts makusudi.

- Hakusema hatagombea u-Spika, ila alisema hatagombea ubunge tena na he never did, hakuwahi kusema hatagombea tena u-Spika.

Respect.

FMEs!
 
Hebu muulize Malecela atang'atuka lini ubunge? Na kama aking'atuka na yeye ananyemelea ubalozi?
Hivi Malecela(75) huyu mzee inabidi apewe chumba pale mjengoni awe anaishi mule... anapapenda sana miaka 19 bado tu anakaba tu....
 
- Ala Kagasheki kumbe ni mnafiki? au ni wewe ndiye mnafiki unajisema? Labda ufafanue kidogo hapo mkuu?

- Malecela hana sababu ya kung'atuka maana wananchi wa jimbo lake bado tunaridhka naye, na hajasema anataka kutoka kama Kagasheki kwamba anatafuta ubalozi., au?

Ahsante.

William.
Kwa ufafanuzi, wewe ndio mnafiki kama umesahau nakukumbusha.

Malecela anakila sababu ya kung'atuka, labda arithishe mabint zake, yeye yuko kwenye senescence sasa.

Uache hizo 'asante zako za kinafiki'. Hazina mshiko wala mvuto.
 
Msekwa alisema hagombei tena ubunge na hajagombea mbona unachanganya facts kwa makusudi?

- La ung'ang'anizi una maana kama Kagasheki ameishiwa hela za kununua ubunge, basi wengine wote ambao hawakununua ubunge nao wajitoe kama yeye? Mkapa hakuwa king'ang'anizi akaachia urais kilichobadilika ni nini hasa?
Una maanisha nini hapa? Maana wewe mwenyewe umesema anataka ubalozi sasa hapo kama si kuhama tu sehemu lakini kubaki kwenye uongozi ni nini?
Mkapa alikua raisi, the highest post, whichh means he had no where else to go but down kama angeamua kutafuta nafasi nyingine. Na uraisi una terms siyo kama ubunge sasa hata angetaka kugombania tena nani ange mruhusu?

- Halafu vipi zile mbio zako za kugombea hilo jimbo au jamaa walikuwa wanakupakazia tu?

Respect.

FMES!
?????? Wewe nani kakuambia nataka kugombea hilo jimbo? Habari hizo nasikia kwako wewe unasema wameni pakazia, wakina nani wameni pakazia unaweza kufafanua? Wapi umesikia nataka kugombea huko na umeambiwa na nani?
 
Kwa ufafanuzi, wewe ndio mnafiki kama umesahau nakukumbusha.

Malecela anakila sababu ya kung'atuka, labda arithishe mabint zake, yeye yuko kwenye senescence sasa.

Uache hizo 'asante zako za kinafiki'. Hazina mshiko wala mvuto.

- Vipi ukiweka sababu za unafiki wa Mkuu William? Kuhusu Malecela sioni hoja, ya ahsante wewe huwezi kumuamulia what to write and what not to!

Respect.

FMEs!
 
- Malecela hana sababu ya kung'atuka maana wananchi wa jimbo lake bado tunaridhka naye, na hajasema anataka kutoka kama Kagasheki kwamba anatafuta ubalozi., au?

Ahsante.

William.
aarrrg Jumanne (75) muda wake umefikia kikomo hawa ndio wabunge ving'ang'anizi ambao hata kama walifanya jema wananchi tunakuja kuyasahau.....hana jipya Jumanne
 
Back
Top Bottom