Kagasheki awashukia wanaolalamikia vitu kupanda bei | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kagasheki awashukia wanaolalamikia vitu kupanda bei

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Sep 30, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Bukoba mjini jana amewaijia juu wale wanaolalamikia kupanda kwa bei za vitu na kupanda kwa gharama za maisha katika miaka mitano.

  Akihutubia katika mkutano wa kampeni katika kata ya Kagondo na huku akisikika moja kwa moja katika redio ya Kasibante FM anayoimiliki, Kagasheki aliwaambia wananchi wa kata hiyo wakati akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo kwa tiketi ya ccm Amani kuwa wasiwasikilize wanaolalamikia upandaji wa bei vitu wala gharama za maisha.

  Kagasheki aliwambia wananchi waliokuwa wakimsikiliza kuwa kupanda bei kwa vitu ni kitu cha kawaida na si kitu cha ajabu kwa kuwa vitu haviwezi kubaki katika bei ile ile miaka yote na upandaji wa vitu bei unatokana na mfumuko wa bei.

  Aliwataka watu wawadharau watu wote wanaolamikia upandaji wa bei na upandaji mkubwa wa gharama za maisha kama watu wasio kuwa na hoja na wawanyime kura kwa sababu hilo si suala la maana.

   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  MF
  Duh! yaani imebidi nicheke kwanza baada ya kusoma.
  Huyo bwana inabidi akapimwe akili kwanza maana kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuthubutu kuongea upuuzi kama huo mbele ya watu wazima unless awe anahutubia wehu.
   
 3. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mbona hakueleza mfumuko wa bei umesababishwa na nini
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,511
  Likes Received: 2,751
  Trophy Points: 280
  Kwani unafikiri anajua????
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huyo mzee mwacheni tu. Mie naona yuko sahihi iwapo atatumia nadharia yake hiyo ya kwamba lazima bei za vitu zitabadilika kueleza kwa jinsi gani pia YEYE kama Mwakilishi wa Wananchi amesaidia kuhakikisha kuwa wananchi wanawekewa mazingira mazuri waweze nao kubadilika na kumudu changamoto zitokanazo na hayo mabadiliko. Mfano, katika mfumuko huo wa bei Mkulima, Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Wastaafu wamewezeshwa vipi kumudu gharama za maisha?
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Duu basi msumbiji ndo hawana akili kabisaa kugoma sababu ya kupanda kwa bei ya mkate!??
   
 7. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jamaa ana elimu ya chekechea nini? Pole Kagasheki, lakini utakuta anashangiliwa.
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama ulikuwepo vile.............. vichwa wazi tanzania hawakosi. Kama wanamshangilia kikwete unadhani watashindwa vipi kumshangilia huyu?
   
 9. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Lakini mbona yeye na boss wake kikwete wanatusomea makaratasi jinsi walivyoweza kushusha mfumuko wa bei?
  Bahati mbaya Makamba ametuzuia kuuliza maswali lakini pia kwenye mikutano hatupewi nafasi ya kuuliza maswali, anadhani yeye anajua kuliko wasikilizaji wote wa hotuba zao! Na hapo nabaki nikijiuliza, hivi kama hawa ndio viongozi wetu......... kweli tutafika nchi ya ahadi?
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Anajua wapi? Maana angelijua asingesema hayo ayasemayo. Bado yeye anaota uwaziri basi..............kuropoka mtindo mmoja.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii ni aina ya viongozi tulionao Tanzania. Hajui lolote. Huyu bwana pamoja na kwamba ni mtu kakaa nje ya nchi hajui hata kutumia computer. Aliwahi kukaribishwa kwenye sherehe katika shule moja na akapewa Lap top ili azindue website ya shule akashindwa kuifungua lol.
  Sasa nambie wategemea nini? Nakwambia These are samples of leaders we have in our country who are preaching developments. Do you expect to have these developments?
   
 12. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  huyu kagasheki si ndo yule mzee mpuuzi kuliko wote aneyjiita baloz?!!!

  hajui maisha yalivyo huyo!!??
   
 13. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Jmani, kuna Muhaya hapa? Kama yupo atuambie nini maana ya 'kagasheki'...
   
 14. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,559
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160

  Nimewahi kuongea na Kagasheki juu ya matumizi ya redio yake katika kampeini za kisiasa.

  Tulikubalina kuwa hatatumia redio hiyo kisiasa kwani inaweza kumpunguzia kura badala kumuongezea.

  Lakini naona hakutekeleza,Redio hiyo itamuaribia kabisa kwani redio yenyewe itapotoza wasikilizaji na matangazo(mapato) na jamii inaeza kudhani yanayotanagzwa hapo ni ya uongo kwani mmiliki ni yeye mwenyewe.

  Hata wahariri wa redio hiyo ambao ni wanataaluma naona wamepoteza heshima kwa kukubali kutanagza hadi upuuzi.

  kagasheki akibadilisha washauri siyo mtu mbaya sana kimtazamo
   
 15. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  KAGASHEKI=IT CANNOT DO ANYTHING=IT CAN DO
  NOTHING=INCAPABLE=INCOMPETENT
  Kwa Kiswahili kisicho rasmi= …siyoweza kitu, ..siyeweza kitu

  Nyongeza ya hapo, Wahaya wana Msemo maarufu unaotoa tahadhari kwa wazazi kutafakari kwa kinakabla ya kutunga jina au kumbatiza mtoto.

  Wanasema hivi: Eibala libi, liita Nyinalyo yaani Jina Baya Humua Mbatizaji au Jina Huakisi Matendo/Uwezo Tarajiwa ya Mbatizwa.

  Maana halisi ya msemo huu inanoga na kutoa tafsiri nzuri kwa KIHAYA. KAGASHEKI ni muathirika wa utabiri wa jina lake. HE IS INCOMPETENT THAT MUCH I KNOW!
   
 16. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Rutunga,
  Mimi pia nimekuwa miongoni mwa Washauri wake lakini kuanzia mwaka huu tulipishana kitaaluma na chaguo sahihi kuheshimu taaluma na ushauri niliokuwa nampa nikaamua na kumwambia kuwa sasa ni vema Tusherekee Kuwa Totauti. Nimeachana naye na amekuwa akiwasiliana nami kukiri japo si moja kwa moja kuwa makosa ya kutumia Wataalamu kisha akaukataa ushauri wao linamghalimu saaaana.
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  kwani anafahamu hilo somo, kichani mwake hakuna tools of analysis na hili ni tatizo lililoivamia ccm kwa sasa. Hata anavyobomoa haelewi.
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Yeye si analipiwa kila kitu akiambiwa kilo ya nyama 5,000 kwake ni hela ya pipi kwa mjukuu wake...
  Hayo ni matusi kwa maskini wa nchi hii..
  Na hawa ndo washauri wa Mkulu. ...!!?
  Sasa sishangai kwanini Mkulu alisema Hajui kwanini tuko maskini...
   
Loading...