Kagame yupo katika hali ngumu

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Pamoja na mafanikio ya Uchumi ambayo nichi ya Rwanda imeyapata, inaonenakana kwamba kuna fukuto la chini kwa chini la upinzani ambalo linamkabili Kiongozi huyu.

Ifuatayo ni document iliyoandikwa na wapinzani wakubwa wa kisiasa, kuuonya Ulimwengu kwamba Rwanda chini ya Kagame inaelekea Kubaya, na watu hawana budi kuwa makini.
 
Attachments

  • RWANDA BRIEFING BY KAYUMBA,KAREGEYA,GAHIMA, AND RUDASINGWA.pdf
    415.5 KB · Views: 315
I am glad umewabrand hawa kuwa ni wapinzani wakubwa. Of course they will have nothing nice to say about Kagame. Hata kama wao wataingia mamlakani, believe me wataanza kuchinjana wao kwa wao.
 
Kuna uwezekano Kagame akawa ni DIKTETA lakini kwa mimi ananikongo moyo sana KWA KUCHUKIA RUSHWA. Hiyo tu ndio siri ya mafanikio makubwa Rwanda.
 
Sawa hata wakisema Kagame ni DICTATOR lakini kuna aina mbili za madictator , wale ambao wanawaletea maendeleo watu wao [ BENEVOLENT DICTATORS] na wale ambao wanawakandamiza wananchi wao na kutojali maendeleo yao; Kagame ni yule dictator anaeleta maendeleo kwa wanyaruanda kwahiyo anapaswa kuungwa mkono!! I would rather be ruled by a benevolent dictator than a COMEDIAN!!
 
Sina msimamo katika hili. Ni kweli Kagame ni mtu wa maendeleo. Pia ni kweli Kagame ni dictator. Nataka vyote maendeleo na uhuru wa kufanya na kutekeleza mambo. The man has to change. Inawezekana kuleta maendeleo na kukwepa kuwa dictator. Kama wanavyoconclude, Rwanda is a socially polarized country and in a free and fair elections RPF can not win. Kwa sababu hiyo basi Kagame is gonna remain a dictator for as long as he is in power. And since he is a good friend of the westerners expect no pressure on him
 
Sina msimamo katika hili. Ni kweli Kagame ni mtu wa maendeleo. Pia ni kweli Kagame ni dictator. Nataka vyote maendeleo na uhuru wa kufanya na kutekeleza mambo
Jerry Rawlings aliwahi kuitwa dictator kwa kuwazaba vibao watu waliokuwa wanazuia utekelezaji wa sera za serikali kwa manufaa ya wote, kwa Africa unahitaji kuwa dictator ili mambo ya maana yaende, kwa hili namsupport Kagame
 
Sawa hata wakisema Kagame ni DICTATOR lakini kuna aina mbili za madictator , wale ambao wanawaletea maendeleo watu wao [ BENEVOLENT DICTATORS] na wale ambao wanawakandamiza wananchi wao na kutojali maendeleo yao; Kagame ni yule dictator anaeleta maendeleo kwa wanyaruanda kwahiyo anapaswa kuungwa mkono!! I would rather be ruled by a benevolent dictator than a COMEDIAN!!

kagame hakuna maendeleo anayoleta kwa wanyarwanda, anatumia resources za inchi kwa maslahi yake na familia yake zaidi na si kwa maslah ya wananchi: mfano, anamiliki jet mbili anazozitumia kutembelea wanafamilia na marafiki zake abroad. Kwasababu ya ukatiri na uuaji wake anajeshi kubwa la kumlinda yeye binafsi
 
kuna mengi yanaendelea hapo rwanda,by the way rwanda inahitaji kuwa na rais kama kagame maana vinginevyo ni ngumu sana kutawala hiyo nchi.mbaya zaidi hawa wenzetu wanabaguana vibaya sana kiukabila,hilo ndio tatizo kubwa sana hapo rwanda maana revenge hazitaisha.makosa anayofanya kagame sasa ndio aliyofanya habyarimana.rwanda ni bomu linalochemka.vita inaweza kulipuka wakati wowote ule kutokana na kwamba wapinzani wengi wa kagame wako nje na wanajiandaa kwa mashambulizi.mbaya zaidi ni pamoja na hawa walioandika hii briefing ambao ni marafiki zake na wanafahamu uongozi wa R.P.F.in and out.
google hii www.afroamerica.net/.../cndp-desert-fardc-general-kayumba-suspected/ -ukajisomee
 
Sawa hata wakisema Kagame ni DICTATOR lakini kuna aina mbili za madictator , wale ambao wanawaletea maendeleo watu wao [ BENEVOLENT DICTATORS] na wale ambao wanawakandamiza wananchi wao na kutojali maendeleo yao; Kagame ni yule dictator anaeleta maendeleo kwa wanyaruanda kwahiyo anapaswa kuungwa mkono!! I would rather be ruled by a benevolent dictator than a COMEDIAN!!

BRAVO: Hata hivyo, kuna wakati mtu anaweza akawa dikteta akawaletea sio maendeleo alakini AMANI na utu, e.g. Mugabe....mnasemaje hapo?
 
... Sijui nifanye nini ..Niweze kumuamini Kagame!!

... Najaribu kumtafakari kwa kila namna .. lakini hapana... Kwangu yule bwana simuamini kabisa!!
 
All in all mie namuona kama kiongozi mzuri ambae anawasaidi sana watu wa Rwanda
 
Jerry Rawlings aliwahi kuitwa dictator kwa kuwazaba vibao watu waliokuwa wanazuia utekelezaji wa sera za serikali kwa manufaa ya wote, kwa Africa unahitaji kuwa dictator ili mambo ya maana yaende, kwa hili namsupport Kagame

Wewe binafsi ungefurahia kuzabwa vibao na kiongozi wako? Au ni ule msemo "mkuki kwa nguruwe....."

It's time to borrow a leaf from Kagame, lol!
 
Pamoja na mafanikio ya Uchumi ambayo nichi ya Rwanda imeyapata, inaonenakana kwamba kuna fukuto la chini kwa chini la upinzani ambalo linamkabili Kiongozi huyu.

Ifuatayo ni document iliyoandikwa na wapinzani wakubwa wa kisiasa, kuuonya Ulimwengu kwamba Rwanda chini ya Kagame inaelekea Kubaya, na watu hawana budi kuwa makini.

Ni kweli, anawabagua sana Wahutu, ni kama analipiza kisasi. Na kuna bwana mmoja ambaye alikuja kutoa ushahidi kuonesha jinsi gani Kagame alivyohusika kuleta mauaji Rwanda baada ya kuamuru majeshi yake yaitungue ndege iliyowabeba marais wa Ruanda na Burundi waliotoka Dar kwa Mwinyi kwenye kikao. Alifukuzwa kazi. Kwa kifupi kuna waruanda wengi nje na ndani ya Ruanda hawajaridhika na jinsi Kagame anvyoachiwa bila kufikishwa mahakamani.

DAMU YA MARAIS ALIOWAUA MWAKA 1994 BADO INAMFUATA.
 
Nounga mkono udikteta wa Kagame so long as nchi yao inapata maendeleo ya watu na amani/usalama kuendesha maisha bila kuvunja sheria. Kuna watu ambao haiwezekani kuwaongoza bila bakora pembeni na nadhani waRwanda ni miongoni mwao. Chukua mfano wa Iraki ona ilivyo ngumu kutawalika. aliiweza saddam tu.
 
Nounga mkono udikteta wa Kagame so long as nchi yao inapata maendeleo ya watu na amani/usalama kuendesha maisha bila kuvunja sheria. Kuna watu ambao haiwezekani kuwaongoza bila bakora pembeni na nadhani waRwanda ni miongoni mwao. Chukua mfano wa Iraki ona ilivyo ngumu kutawalika. aliiweza saddam tu. Na Rwanda anaiweza Kagame tuu. Akiondoka uje uone watakavyochinjana wale jamaa
 
Sina msimamo katika hili. Ni kweli Kagame ni mtu wa maendeleo. Pia ni kweli Kagame ni dictator. Nataka vyote maendeleo na uhuru wa kufanya na kutekeleza mambo. The man has to change. Inawezekana kuleta maendeleo na kukwepa kuwa dictator. Kama wanavyoconclude, Rwanda is a socially polarized country and in a free and fair elections RPF can not win. Kwa sababu hiyo basi Kagame is gonna remain a dictator for as long as he is in power. And since he is a good friend of the westerners expect no pressure on him

Nimeipenda sana comment yako The Dreamer. Inaonekana una ufahamu wa kutosha katika mambo yanayoendelea kwa hawa majirani zetu. Nimeifuatilia sana historia ya nchi ya Rwanda na naweza kusema kuwa nina ufahamu wa kutosha wa siasa za Rwanda. Ninachoweza kusema hapa ni kwamba Rwanda ilikuwa inahitaji kiongozi kama Kagame katika kipindi alichoingia madarakani. It was a fragile state and it could go back to instability any time if it hadn't had an uncompromising leader like him. Alikuja na agenda ya maendeleo na aliitekeleza. Lakini vile vile tusisahau kwamba alikuja na agenda nyingine ya kusuppress any dissenting voice. He instituted a reign of terror in Rwanda, and it seems it has worked for him for some time. Kwa mfano nchini Rwanda watu hawaruhusiwi kuzungumzia genocide from an angle different from the Government's stand. Hii imetungiwa sheria kabisa as there is an offense called "Genocide denial". Reign of terror inasaidia kiongozi dictator kufikia malengo yake, lakini ni relatively for a short time. Kagame had a vision, but his way towards achieving it is still wanting. Niliwahi kuwa na rafiki yangu Mnyarwanda, a staunch ally of Kagame. We were one day discussing the issue of Kagame and the Nyamwasas. In his own words (which reflect Kagame's stance) he said that in Rwanda now the focus is on development, and democracy will come later. I asked him what would be the need of building a country that you are sure is going to be destroyed again in the near future. He had no answer to that. Kagame did great things for Rwanda (just like Museveni when he came into power in 1986), but the path he is treading on now will lead the tiny country in yet another bloodshed. I am not a doomsayer, that's my humble assessment of the situation. If you happen to be in Kigali some time, you can feel that the air is so tense. You can feel that there is a kind of invisible hand with a powerful authority that commandeers every tiny detail of life, from the way people dress to what they discuss.
 
Rais kagame kafanya mengi mazuri kwa taifa la Rwanda. Kwa kweli mafanikio yake ni makubwa na ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine wa Africa. Lakini bado suala la demokrasia ni muhimu sana. Kagame hawezi kuendelea kujificha kwenye mafanikio ya kiuchumi na kuendelea kuwakandamiza wananchi wake. Tukumbuke kuwa demokrasia ni maendeleo pia.

Maendeleo ya kiuchumi bila amani yatakuwa hayana maana. Hatutaki kuanza kupokea wakimbizi tena hapa kwetu. Kagame ajirekebishe, alete demokrasia.....yeye sio Mungu
 
Mimi naungana mkono na wale wanaosema kuwa dikteta anayeleta maendeleo ni mzuri. Ndivyo alivyo KAGAME. Kiongozi huyu he has his country at heart. Anawapenda watu wake. Ipo story kuwa hata mdogo wake (sijui dadake?) ni machinga kwa maana kuwa anafanya biashara ndogo ndogo. Kagame hataki upendeleo wa kumpa maisha ya peponi mdogo wake huyo.

Kwa viongozi wa Tanzania wengi wao wamejaa upendeleo mkubwa. Ukiwa kiongozi Tanzania ni mwanzo wa kutajirika kwa kujilimbikizia mali. Kiongozi akiwa madarakani hapa kwetu ni kufanya upendeleo mtupu kwa kutoa vyeo ovyo na hata madaraka.

KAGAME anaweza kuwa dikteta lakini analeta maendeleo. Hivi sasa RWANDA huwezi kulinganisha na Tanzania kiuchumi kwani nchi hiyo ndogo na isiyo na rasilimali (labda zile za kuiba huko DRC) uchumi wake ni imara.

Watanzania tumebaki kupiga soga kwa jina la demokrasia. Wale wa CHADEMA waliosusia hotuba ya JK ingekuwa ni RWANDA wangeipatapata. Wasingefanyiwa jambo na wasirudie ujinga huo.

Kimsingi 'dictatorship' in Africa at its present stage is a positive thing. Waafrika hatuwezi kuendelea mpaka kwa viboko. Ndio maana Wajerumani walituchapa bakora wakati wa ukoloni.

Hivi jamani yuko wapi yule DC mkoani Kagera aliyewachapa waalimu waliokuwa wakichezea kazi? That man is my hero. Hakuna kubembelezana hapa. Urusi imeendelea kutokana na udikteta wa Stalin. Hata waingereza wapo pale kutokana na udikteta mkubwa wakati wa mapinduzi ya viwanda. Marekani ili wachapane kwanza vita vya wenyewe kwa wenyewe ndipo akili ikawajia.

Sasa sisi watanzania tunataka nalenale tu. Mtu anakwapua fedha za EPA halafu anatuchezea. Ukiiba China ni risasi tu na wengine hawarudii ujinga wa wizi. Yuko Jenerali mkubwa wa jeshi kule China na ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Communist Party ambaye baada ya kubainika wizi wake njia muafaka kwake ilikuwa ni kujipiga risasi kwani alijua asingepona.Je, mnawakumbuka wale walisambaza maziwa ya watoto yenye sumu kule China. Walipigwa risasi. Hapa watu wameleta Richmon ambao hata kufunga bulb hawajui bado tunao na baadhi yao wanafikiria hata kupata madaraka makubwa zaidi siku zijazo.

Udikteta ni jambo zuri. KAGAME kwangu ni safi kabisa.
 
Back
Top Bottom