Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema Tanzania na Rwanda zitafanya miradi mikubwa sana ya maendeleo kwa pamoja kufuatia kufunguka kwa ukurasa mpya wa kimahusiano hivi karibuni baina ya nchi hizi mbili.
"Nchi zetu zimejipanga kufanya miradi mingine mikubwa sana ya pamoja ya miundombinu kama ule wa daraja Rusumo kwenye mto Kagera".
Amesema kwa sasa Rwanda na Tanzania zimejikita katika kuiboresha bandari ya Dar es Salaam ili bandari hio itumike ipasavyo kuihudumia nchi yake ambayo haina bandari.
Kagame ameongeza kuwa nguvu kubwa itawekwa katika miundombinu lengo likiwa kuboresha biashara baina ya Tanzania na Rwanda.
"Kwa hakika tumejipanga sana kuhakikisha kuwa Rwanda na Tanzania zinajikita kwenye mambo makubwa mno, kubwa likiwa kujenga na kuboresha miundombinu ili kukuza biashara baina ya mataifa haya mawili, ambapo focus kubwa itawekwa katika masuala ya kibiashara."
Aidha Kagame amesema pia kuwa amefurahishwa sana na ujio wa Magufuli ambao umefungua ukurasa mpya wa ushirikiano na nchi yake kufuatia sintofahamu iliyokuwepo baina ya Rwanda na Tanzania katika utawala ulipita na akaongeza kuwa yaliyopita, yamepita daima yeye hafungamanishwi na historia za nyuma.
"Ninashukuru sana kwa ujio wa Rais Magufuli, kwa kweli anajitahidi sana kuweka mambo sawa kwa nchi yake" alisema Kagame.
Chanzo: The Guardian.