Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,898
Salaam toka Kigali hapa mjini Rwanda.Niko hapa tangia leo asubuhi .Lakini sijaja nilikuwa kule Burundi .Nimekuwa na maongezi na Askofu wa Jimbo moja Katoliki hapa kujua ukweli wa mauaji ya wakati ule .
Baadaye nimevutiwa na Rwanda kutokana na hadithi za Kagame kuambiwa shemeji yake aliyemuoa Dada yake Kagame alitaka kujifanya na yeye ni Kagame wa eneo hilo .Wakubwa wakaogopa kumkamata kwa kuwa alikuwa anatumia jina la Kagame kufanya ujinga wake na hata tender serikalini na ushenzi zaidi .
Wakaniambia Kagame akapewa taarifa akaamuri akamatwe awekwe ndani then apelekewe funguo .Jamaa alikamatwa na funguo ikapelekwa kwa Kagame na yeye akai flash chooni akasema nione sasa wa kumtoa .Ina maana hata chakula akawa hawezi kupata tena .
Baada ya siku 4 mkewe alilia sana mbele za Kagame na Kagame akasema vunjeni atoke na aletwe hapa .ikafanyika na jamaa akapelekwa na kuambiwa next time utapotea hii ni Nchi si ukoo wala ushemeji .
Likaja soo la kugawana ardhi .Wale waliokuwa na Kagame msituni wengine wame staafu walijichukuliwa maeneo na kuishi bila wasi wasi .Kagame akasema ardhi sasa igawiwe kwa wote bila kujali mtu .Kweli likafanyika ila wale ma general na wakubwa wengine wakawa hawaguswi.Kagame akauliza anaambiwa wale ni wapiganaji wako nk .
Akaenda mwenyewe akasimamia uhawaji na hakuna kilicho endelea hadi leo Kagame anachapa mzigo .
Njoo Kigali uone usafi wa barabarani .Njoo uulizie ama ujifanye wataka kutoa hongo upate huduma ama unaomba .Kagame kama China anaua na siku chache Rwanda inategemewa kuwa mbali sana .
Nauliza sisi na hao wazee wa amani na utulivu na kulindana tutakuwa lini kama Kagame ?