Kagame cup mshindi wa 3: Yanga waingia mitini

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Duh naona Michuzi anatoa nyepesi kwamba Yanga tumeingia mitini.... Nimetokea sipo mjini na kila ninayempigia naye ni amezima simu!! Asalale, hii ni kuwapa wanyama cha kuongea manake si utani hii ndio inaitwa aibu ya karne, heri kulipa faini kuliko aibishwa na mnyama!!

Kwa kweli naona uzalendo umeanza kunishinda!!!
 
Ha ha haaa.... Haya pamoja na Michuzi kusema mambo ni mbele kwa mbele Mnyama ametembea namba 3, nimewasiliana na vijana ni kweli bwana lilikuwa pre-planned deal hivyo Yanga ndio tumemkimbia Mnyama.... Haya mseme tu jamani nadhani tulikubaliana, ha ha haaaaaaaaa!!!

Kaaz kweli kweli kwenye mambo ya viingilio, haya!!
 
yanga ni kama baadhi ya vyama vya siasa......! ATI KUSUSIA UCHAGUZI.....!
MUGABE OYEEEE.....SIMBA OYEEEEE....!
ASUSAYE MUOGA, NA KUSUSA SI MBINU YA KUSIKILIZWA BALI KUONYESHA KUSHINDWA....!
 
Yanga hajatokea uwanjani ktk mechi ya mshindi wa tatu kwa sababu hawaelewana ktk mapato na TFF
 
Hatimaye Simb2 Yanga 0... lakini mezani... baada ya viongozi wa Yanga kufanya mambo ya miaka 47.
 
Fedheha kubwa.Kumkimbia mnyama ni aibu kwa yanga kwa kisingizio chochote.Ni aibu kwa Taifa pia.Yanga inaonekana kama timu ya kijiweni.Napendekeza wapewe adhabu na wajifunze.
 
Hatimaye Simb2 Yanga 0... lakini mezani... baada ya viongozi wa Yanga kufanya mambo ya miaka 47.
...Hii inadhihirisha jinsi gani soka ya bongo inavyozidi kurudi reverse badala ya kwenda mbele....angalau sasa ile ndoto waliyokuwa nayo wa-tz kuwa soka ya Tz inaelekea kwenye mwanga kidogo ndio inafifia. Ni aibu na ujinga uliopindukia kwa timu kubwa kama Yanga yenye viongozi waliokwenda shule kama Madega kukubali mambo ya hovyo kama hayo ya kugomea mchezo kwa kisingizio cha kulipwa pesa waliyoahidiwa kabla ya mchezo wakati kanuni za mashindano wanazielewa wazi kuwa hakuna timu inayopewa pesa zaidi ya zawadi kwa washindi....

Na hii iwe fundisho kwa TFF yetu nadhani Tenga, Magori, Mwakalebela na vijana wao wajifunze kuwa kale kautamaduni ka kutegemea mavuno ya mapato kutokana na kuwepo kwa Simba au Yanga ukome sasa matokeo yake ndio haya kupata fedheha jua linawaka....Mtoto ukimdekeza atakumbua mbele za watu.

TFF kukubali kuburuzwa na Simba na Yanga ni kitu kibaya sana na ndicho kinachoharibu mpira wa Tz.. eti walifanya nao mazungumzo ya kuwapa pesa kidogo ili waingize timu uwanjani....Hivi huu nao hatuwezi kuita ni ufisadi???
 
duh hapa nakiri tunaiogopa simba, Hongereni Simba. Inasikitisha sana, huyu Madega ni mhuni tu, naona ni heri tukamrudisha mzee wa busara Bw. Fransis.
 
Yaani Manji alishindwa kuwapa hizo pesa atimize malengo yake?

Ngoja nitafute makala moja hivi. Aibu kubwa ya KARNE
 
Manji anadhamira njema na Yanga?


Na Mwandishi WETU - MwanaHalisi

KWA mwanayanga yeyote, ni lazima atakuwa anatembea kifua mbele kutambia usajili wa kufuru uliofanywa na bilionea kijana mwenye umri wa miaka 30 tu! Yusuf Manji.

Kwa hakika, Manji ameitikisa nchi kwa usajili wake wa msimu wa 2008/9, baada a kusajili kikosi chenye thamani ya zaidi ya Sh. 500 milioni.

Inaelezwa kwamba, licha ya kumfanya kipa Juma Kaseja avunje rekodi ya usajili Afrika Mashariki na Kati kutokana na kunyakuliwa kwa dau la zaidi ya Sh. 75 milioni, mchezaji aliyelamba fedha kidogo kabisa katika usajili, hakukosa Sh 8 milioni.

Manji amekwenda mbali zaidi na kumsajili kipa kutoka Ulaya, huko Serbia kwa zaidi a shilingi milioni 130!

Nyota hao wote kutoka nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya, wakiwamo wengi wa timu ya soka ya Tanzania `Taifa Stars', kwa ujumla wameandika historia.

Na Manji ameandika historia ambayo bado ni gumzo katika soka ya Tanzania, kila mmoja akihoji ilikotoka jeuri hiyo ya usajili.

Mbali ya kukusanya nyota wanaoaminia kuwa na vipaji halisi vya soka, Manji ameipa pia Yanga timu ya makocha watatu, wote kutoka Ulaya.

Pamoja na usajili na mambo mengine kadha wa kadha makubwa anayoifanyia Yanga, Manji kwa sasa ndiye baba, akiitunza timu kwa takribani shilingi milioni 2.5 kwa siku katika hoteli ya Lamada, Ilala jijijini Dar es Salaam.

Kiasi hicho cha fedha wastani wa Sh. 75 milioni kwa mwezi, achilia mbali mishahara na gharama nyingine.

Kwa kifupi, viongozi wa Yanga hawapasui kichwa hata chembe juu ya uendeshaji wa timu, mishahara, safari, malazi na mambo mengine.

Wameridhika na kudiriki kutembea kifua mbele kwamba hakuna linaloishinda Yanga, kama jambo husika litahusiana na masuala ya fedha.

Pamoja na kumshukuru Manji na kutambia fedha zake, bado kuna maswali lukuki ya kujiuliza.

Kwa mfano, wakati anatia mguuu Jangwani na kupokelewa kwa kila aina ya nderemo, Manji aliahidi kuikomboa klabu kiuchumi.

Akaanza mbwembwe za kupeleka seti ya televisheni klabuni ili wanachama wawe wanakutana hapo na kubadilishana mawazo.

Akahamishia nguvu kwenye kuukarabati Uwanja wa Kaunda unaomilikiwa na klabu hiyo. Tukashuhudia makatapila akichimbua uwanja, lakini ghafla tukashuhudia udongo uliochimbuliwa ukigeuka tope kutokana na mvua kubwa mfululizo.

Mpaka leo hakuna kilichoendelea, zaidi ya kusikia malumbano ya hapa na pale na aliyekuwa mweka hazina, Abeid Abeid `Falcon'.

Na hata klabuni, hakuna kilichoendelea. Jengo la Yanga ghorofa tatu limebaki kuwa gofu, ingawa makadirio ya ukarabati wake, ikiwa pamoja na vyumba takribani 20 vya wachezaji, vingeweza kula si zaidi ya sh milioni 150.

Hii ina maana kwamba, klabu ingerudisha hadhi na hata kuifanya iwe na kambi ya kudumu klabuni hapo, huku sehemu nyingine za klabu zikitumika kama vitegauchumi, achilia mbali jengo la Mtaa wa Mafia linalozidi kufanana na banda, licha ya kuwa katika eneo zuri kibiashara.

Kukamilika kwa ukarabati wa jengo kungeweza kuisaidi mno Yanga katika kuepuka gharama za kuwapangishia nyumba wachezaji `wasela', gharama za kambi na mambo mengi kadha wa kadha.

Hali kadhalika, ukarabati wa uwanja ungeweza kugeuka rasilimali tosha kwa klabu, kwani baadhi ya mechi za ligi na hata za kimataifa zingeweza kutumika kwenye uwanja huo unaokadiriwa kuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 10,000 kama ukiwekwa majukwaa. Ndiyo, kwani ZANACO ya Zambia wanaangaika na nani zaidi ya kutumia uwanja wao wa Sunset pale Lusaka hata katika mechi za kimataifa? Kwa nini Yanga ishindwe?

Hapa ndipo ninapojiuliza kwamba ni kweli Manji aliingia Yanga kutokana na kuwa na Yanga-damu, kwa maana ya ukereketwa au alikuwa na yake?

Na katika yake, suala la ubinafsi haliwezi kuwekwa kando, kwamba pengine ana malengo ya baadaye ya kutaka kunufaika na klabu, iwe kisiasa, kimichezo, kiuchumi na njia nyingine kadha wa kadha.

Ikumbukwe kwamba, wao waliopita Yanga na klabu nyingine kubwa nchini kwa staili ya Manji, wakanufaika walivyoweza, wengine wakipenya katika makujwaa ya kisiasa na kuukwaa uheshimiwa, lakini hawakuonekana tena katika klabu zao.

Je, huko ndiko anakoelekea Manji au ana dhamira ya kweli ya kuisaidia Yanga? Kama ndivyo, kwanini asiijengee misingi imara wakati huu, na badala yake anatumia mamilioni kwa mamilioni ya shilingi kuilaza timu hotelini ilhali Yanga ina nafasi kubwa, isipokuwa yenye kuhitaji matengenezo madogo tu?

Nitakuwa mwenye furaha isiyo kifani kama Manji wenyewe anaweza kunitoa hofu juu ya haya ninayoyawaza kwa sababu hainiingii akilini kuona bwana mkubwa huyo (kwa sababu ya fedha, si umri) akifanya mambo makubwa mithili ya sherehe msibani. Manji afahamu kwamba, Yanga inahitaji fedha zake kwa mambo mengi zaidi ya usajili huu kufuru.
 
Duuh!! Wakimbiaji wamekuwa wengi kweli kweli, km walivyoingia mitini Lwakatare na Kakobe -- ktk kujibu hoja pale Diamond, jana. Wakati huo huo, Mtikila ashiriki, lkn aufyata!
 
kwani waungwana yanga si walikubaliana na TFF kuwa kabla ya mechi timu zote mbili zinapaswa kupewa mil 50 shilingi kwa kila moja?
sasa TFF hawajatoa hata mia...
so kwa nini yanga waingize timu uwanjani?
wakati makubaliano hayajakamilika?

wenye njaa ndo walioingiza timu uwanjani.
 
kama hilo kombe yanga walishalichukua enzi zile lina umaarufu...
achana na sasa hivi lipolipo tu kama kinesi.
na waliweza kulichukua nje ya ardhi ya tanzania na kuleta heshima kwa taifa, mpaka ikafika kipindi watoto wa uganda wakawa wakiulizwa "unataka kucheza mpira kama nani?"
wanajibu kama lunyamila.

so sioni cha ajabu dar es salaam young african kujitoa kutokana na uharo wa TFF.
 
kama hilo kombe yanga walishalichukua enzi zile lina umaarufu...
achana na sasa hivi lipolipo tu kama kinesi.
na waliweza kulichukua nje ya ardhi ya tanzania na kuleta heshima kwa taifa, mpaka ikafika kipindi watoto wa uganda wakawa wakiulizwa "unataka kucheza mpira kama nani?"
wanajibu kama lunyamila.

so sioni cha ajabu dar es salaam young african kujitoa kutokana na uharo wa TFF.

Naona unaleta hadithi ya sungura "sizitaki mbichi hizi".
Kubali tu kuwa mmeingia mitini na hilo ni jambo la aibu. Kama ni kombe la kinesi kwanini mlishiriki? Kama ingekuwa fainali mngejitoa? Ama kweli MNYAMA tishio, yaani mpaka Yaboyebo anaingia mitini. Hamna neno tunawasubiri kwenye ligi na huko nako muingie mitini.
 
...........yanga wamechukua kombe mara 2...simba mara 5..kama unataka kuongelea historia..........................

taratibu za michezo hii ni wazi ..kugawana pesa hakuna ..mmesaini kuingia kugombea kombe na milioni 30..sasa yanga mlitaka milioni 50 na mshindi apewe nini?..afteral si nyie mnajiita mna pesa ..tena za kifisadi ..usajili milioni 800..sasa milioni 50 kitu gani kwenu...mnatia huruma tu!!!!

...leo mnefukuza timu yote ndio maana ivo amekataa kudaka kwa sababu mwaka jana mlimfungia..na hata pesa za kombe mkamyima..haya huyo kaseja ndio wazi anajulikana kuwa ni mwana simba...angefugwa leo si mngemuuwa..hata ingekuwa mimi kaseja nisingedaka...mzungu ndio huyo alikuwa muuza peremende ..mmemleta kuuza sura ...

mwaka huu ni mimba tu kama kawaida......hata mkifunga kizazi itapenya...warembo tu!!!
 
yanga wanashiriki mashindano makubwa msimu huu, yaani wanatazamia kupambana na timu kama al ahly, enyimba musica ambayo last season ilwapiga simba jumla 7-1.
so hatuwezi kukimbizana na simba ambao wanawasubiri villa squad, JKT ruvu, AFC, polisi moro na nyingine za hadhi yenu katika ligi yenu hiyo ya TFF ambayo rufaa zinakubaliwa.
 
Uongozi wa YANGA useme ukweli sababu PESA au MTAALAM WA KAMATI YA UFUNDI [uchawi]katoa matokeo mapema ya kuwa SIMBA watashinda kwa goli nyingi
BORA NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI
SIMBA TUMEWEKA RIKODI MPYA YANGA WAMETUKIMPIA UWANJANI
 
"YANGA ITABAKI MTEJA HADI 2010......!" JAMHURI KIHWELUm na kwa kitendo hiki JAMHURI KUONGEZA MKATABA HADI 2015....!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom