MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Enzi ya JK Tanzania ilikuwa haipatani vizuri na Rwanda kwasababu JK alikuwa hapatani na Kagame.
Sijui nani kwa hakika alianzisha ugomvi lakini nadhani ni pale JK alipopendekeza kuwa waasi wa Rwanda wawekwe kwenye meza moja ya mazungumzano na serikali ya Rwanda. Pia kukubali kwa Tanzania kupeleka majeshi (JWTZ) nchini Congo kupambana na waaasi wa M23 ambao Rwanda wanadaiwa kuwatumia. Rwanda ilichukia na ndipo zikaanza sarakasi za kejeli baina ya serikali hizi mbili.
Rwanda ikadai eti JK kapeleka JWTZ Congo kwa sababu mama Salma (mke wa JK) anafanya biashara ya madini na Janeth Kabila (dada wa Joseph Kabila). Magari ya Rwanda yalilipa ushuru mkubwa kwenye mizani kuliko magari ya nchi zingine na wao wakalipa hivyohivyo.
Nchi zilitishiana hivyo Kagame alikuwa adui wa JK kwa Magufuli amekuwa rafiki.
Kagame ndio rais wa kwanza duniani kumpongeza Magufuli kwa ushindi wa urais katika kipindi kifupi cha Magufuli kama rais, Kagame amekuja nchini mara tatu ni urafiki mkubwa kati yao. Rwanda imesaini mikataba mikubwa na Tanzania kipindi hiki cha JPM. Kumbe kwa sasa ni marafiki.
Nilichojifunza: Kagame ni kichwa, alijua alikosana na mtu na siyo taifa. Hakuna adui wa kudumu