Kagame akaa hoteli ya sh milioni 30 kwa siku New York, Kikwete je?

Mojo

Senior Member
Apr 27, 2011
152
90
Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye amekuwa akisifiwa kwa uongozi thabiti na kuiendesha nchi vizuri kuliko Tanzania, sasa inaelekea ameanza kulewa sifa baada ya kufanya vituko huko New York.

Kagame ameripotiwa kulala kwenye hoteli ya kifahari ambapo gharama ya rum (chumba) ni takribani shilingi milioni 30 kwa usiku mmoja.

Pia wajumbe mbalimbali wa marais wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa New York wamekuwa wakionekana mitaa ya New York wakifanya kufuru kubwa, ikiwemo kufanya shopping ya nguo na kula hoteli za bei mbaya. Matumizi yote haya ya anasa yanagharamiwa na walipa kodi wa nchi zao.

Kugundulika kwa matumizi haya ya anasa, kumezua gumzo miongozi mwa Watanzania, wakitaka kujua je Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria mkutano huo wa UN Marekani amelala kwenye hoteli ya dola ngapi kwa siku na anafanya matanuzi gani huko kwa pesa za wavuja jasho wa Tanzagiza?

Gonga hapa kuona source ya taarifa: TANZANIA files
 
images
 
Mi nafikiri tunamlaumu bure hebu tuangalie 30m ni sawa na dola ngapi, ukigawnya kwa 1600, unapata unapata $ 18750, hii ni hela ndogo sana kwa standard ya us, labda mtoa mada atupe data zipo za kuanzia $ ngapi na yeye kaichukua ya standard ipi, otherwise tusiwe tunablame every thing tutaonekana wendawazimu. Je Wanyarwanda wanasemaje kubusu rais wao.
 
Kwa kawaida hoteli ya rais wetu pale NY ni NY Intercontinental ambayo ni ya kawaida sana ila akiwa DC hulala Marriot Maquesambayo bei si haba!. Hoteli zote hizo zina presidential suite kule ghorofa ya mwisho ambapo mara nyingi serikali hukodi floor nzima ila hata kama kaja na nanihii naye hulipiwa chumba floor hiyo hiyo for easy accsess!.
Angalizo: Nimezitaja hoteli hizo as the general rule, there are always exceptional to the general rules.
 
Mwacheni jk wa pili ajirambe kwani wananchi tumempa ridhaa.
 
Mi nafikiri tunamlaumu bure hebu tuangalie 30m ni sawa na dola ngapi, ukigawnya kwa 1600, unapata unapata $ 18750, hii ni hela ndogo sana kwa standard ya us, labda mtoa mada atupe data zipo za kuanzia $ ngapi na yeye kaichukua ya standard ipi, otherwise tusiwe tunablame every thing tutaonekana wendawazimu. Je Wanyarwanda wanasemaje kubusu rais wao.

Ndogo kwa stds za US? Unaishi US gani wewe ...
 
Not fair, 30 grands per night? Kagame you are crossing the line.

naona ndugu munadhani tupo stendi ama,unashuka nakutafuta chumba cha 5000.hawa ni viongozi wa nchi lazima aende sehemu yenye usalama sasa piga hesabu zako pale newyork hoteli rahisi shilingi ngapi ndio utajua maisha ya kule sio kama tz.hoteli yenye usalama pesa zinatoka.
 
Huyo jk hata angelala nje kwenye mitaa ya manhattan,ni sawa 2.
 
Capture.JPG


Kulingana na maelezo yaliyotolewa kule michuzi blog, hili ndio dau analotoa rais wetu kwa usiku mmoja. kwa kweli nampongeza kwa hili!
 
Back
Top Bottom