Kagame adaiwa kupandikiza makachero nchini kuipeleleza Serikali… mbunge atajwa kuhusika!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
February 18, 2014


JEURI ya wazi inayoonekana kuwemo ndani ya taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa mara kwa mara na vyombo vya habari vya serikali ya Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake, inaelezwa kujengwa na ushirika wake wa kiintelijensia alioupandikiza ndani ya mfumo wa serikali na taasisi mbalimbali hapa nchini,MTANZANIA limedokezwa.

Taarifa zilizolifikia gazeti la MTANZANIA kutoka kwa watu waliokaribu na viongozi wa Rwanda na wale walioko kwenye taasisi mbalimbali za kiserikali hapa nchini,zinaeleza kuwa taarifa ambazo zimekuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo, msingi wake unaweza kuwa mtandao ambao serikali ya Kagame imeujenga hapa nchini.

Kwamba Rwanda, mbali na kufanikiwa kupenyeza watu wake kwenye mifumo ya kitaasisi hapa nchini, pia imefanikiwa kujenga ushirika na watu wa kada mbalimbali wenye umaarufu,ushawishi na wanaoheshimika nchini, wakiwemo baadhi ya wasomi na wanasiasa.Kuvuja kwa taarifa hizi, kumekuja wakati ambao gazeti la serikali ya Rwanda,Rwanda Times na mtandao wa News of Rwanda, yakiripoti taarifa zinazoigusa serikali ya Rais Kikwete, ikinukuu vyanzo vya kutoka hapa nchini, japo ukweli wa taarifa hizo ukiwa haujulikani,kutokana na Ikulu ya Dar-es-salaam kuzikanusha mara kwa mara.

Dhana hii inapewa nguvu na taarifa mpya kabisa zilizotufikia, ambazo zinadai kuwa katika kuendelea kuimarisha mtandao wake, Serikali ya Rwanda imechangisha fedha kwaajili ya baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ili kulinda maslahi yake.Taarifa hizo zinamtaja Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo, Profesa Silas Lwakabamba, ambae aliwahi kusoma na kuishi nchini kuwa ndiye aliye endesha harambee hiyo ambayo inadaiwa ilimshirikisha Rais Kagame.

Habari zaidi ambazo MTANZANIA imezipata zinadai kuwa katika harambee hiyo, iliyohudhuriwa na baadhi ya Mawaziri wa serikali ya Rwanda pamoja na wafanyabiashara wakubwa nchini humo,Rais Kagame kwa upande wake alichangia Dola 500,000.

Gazeti hili limedokezwa kuwa, lengo la harambee hiyo, ni kuhakikisha ushawishi wake unafanikiwa, hasa kwa watu ambao wamekuwa wakiiunga mkono Rwanda, hususani wakati huu mgumu ambao inakabiliwa na tuhuma za kuchochea mapigano katika eneo la Mashariki ya Congo, ambako Tanzania imepeleka wanajeshi wake.

Katika mkakati huo, walengwa ni vyama vya upinzani, kutokana na kuwa na uhusiano wa shaka na serikali iliyoko madarakani.

Tayari mara kadhaa vyombo vya habari Rwanda, hususani vile vya serikali, vimekuwa vikitumia kauli zinazotolewa na wapinzani hapa nchini, kama hoja ya utetezi wake dhidi ya uhusiano mbaya na Ikulu ya Dar-es-salaam.

Profesa Lwakabamba, ambaye anatajwa kuongoza zoezi la sasa, inaelezwa kuwa serikali ya Rwanda imeamua kumtumia kutokana na uelewa wake kuhusu Tanzania.

Kabla ya taarifa hizi, Lwakabamba aliwahi kuripotiwa na gazeti moja (si MTANZANIA) kwamba ni waziri mwenye asili ya Tanzania aliyechaguliwa katika serikali ya Rwanda.

Inaelezwa kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda, lakini pia alisoma Chuo Kikuu Dar-es-salaam (UDSM) Kitivo cha Uhandisi, na mwaka 1981 alikuwa Mkuu wa kitivo cha Uhandisi, kazi aliyoifanya mpaka anaondoka nchini.

Profesa Lwakabamba, ambaye anaelezwa kuijua vyema Tanzania kutokana na kuishi muda mrefu, alipata elimu ya msingi Muleba, mkoani Kagera na baadaye kujiunga na shule ya sekondari ya Ihungo.

Mwaka 1971 na 1975 alipata Shahada ya Uzamivu katika Kitivo cha Uhandisi, baada ya kujiunga na Chuo cha Leeds, Uingereza kwaajili ya shahada ya fani hiyohiyo.

Msomi huyo anaelezwa kwenda Rwanda mwaka 1997,baada ya kuombwa na Rais Kagame, ambaye alikwenda UDSM kuwaomba baadhi ya wahadhiri kwenda Kigali kufungua chuo kikuu katika taifa lake, baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994.

Gazeti hili lilimtafuta Profesa Lwakabamba kwa njia ya mtandao ili kupata ufafanuzi kuhusiana na harambee hiyo, lakini hakuweza kujibu maswali aliyoulizwa.

Juhudi za kumtafuta Profesa Lwakabamba bado zinaendelea. Wakati hayo yakitokea,taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa katika mkakati huo,mbunge mmoja (jina tunalo), hivi karibuni alisafiri kwenda Rwanda akipitia Afrika Kusini.

Inaelezwa kuwa mbunge huyo alionana na baadhi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Rais Kagame kuhakikisha anaimarisha mtandao wake hapa nchini.

Mbali na mbunge huyo,taarifa hizo zimewataja baadhi ya wanasiasa wengine ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifaidika na fedha za serikali ya Rais Kagame, kwa kujua ama pasipo kujua kama lengo lake ni kuwaweka katika mtandao wake huo.


Chanzo: Mtanzania
 

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,363
2,000
Hivi Kagame, Tanzania ikiamua kumpiga tutapata shida sana au kwa vile ana mtusi mwenzake Museveni.
 

tumiakichwa

Member
Jan 26, 2014
44
0
haya ndo moja ya mapungufu ya usalama wa taifa badala ya kushughulika na mambo ya usalama wa nch wanahangaika na watu ambao wanatetea maslah ya uma.
na tusipoangalia nch inaingia kwenye laana kupitia damu za watu zilizomwagika bila hatia kwa sababu tu ya viongoz wenye ufinyu wa mawazo.
ushaur wangu usalama wa taifa fanyen kaz yenu bila ya shinikizo la kisiasa,na tutambue kuwa katka vita si kagame peke yake ndye atakayepgana na tanzania mfano ni sirya serkal inapambana na kikund kinachoipinga serikal lakn nyuma yake zko serkal znazosaidia sirya na hata hcho kikund kinasaidiwa na mataifa mengne. therefore vita inawaambatanisha mataifa meng na vkund vingi.
mwisho kama ni kwel kuna wabunge wanaoshirki katka huo mpango wa kagame huo ni usaliti kwa taifa na si jambo jema!
ahsanteni!!
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,877
2,000
Nilishasema humu, mijadala hii ya kumsifia KAGAME humu JF na wafuasi wa CHADEMA lazima kungekuwa na watu kutoka nchini wako nyuma ya Sakata hili. na nadhani ndiyo maana Rais katoa tamko kule DODOMA.

Naungana na Mtikila kuwa KAGAME achapwe ili tujue huyo Mbunge aliyekwenda kuchukua harambee huko RWANDA.
 

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,877
2,000
haya ndo moja ya mapungufu ya usalama wa taifa badala ya kushughulika na mambo ya usalama wa nch wanahangaika na watu ambao wanatetea maslah ya uma.
na tusipoangalia nch inaingia kwenye laana kupitia damu za watu zilizomwagika bila hatia kwa sababu tu ya viongoz wenye ufinyu wa mawazo.
ushaur wangu usalama wa taifa fanyen kaz yenu bila ya shinikizo la kisiasa,na tutambue kuwa katka vita si kagame peke yake ndye atakayepgana na tanzania mfano ni sirya serkal inapambana na kikund kinachoipinga serikal lakn nyuma yake zko serkal znazosaidia sirya na hata hcho kikund kinasaidiwa na mataifa mengne. therefore vita inawaambatanisha mataifa meng na vkund vingi.
mwisho kama ni kwel kuna wabunge wanaoshirki katka huo mpango wa kagame huo ni usaliti kwa taifa na si jambo jema!
ahsanteni!!
Ni mapema kuwalaumu usalama wa taifa kwa vile hatujui kama taarifa hizi zimetoka kwao. Inawezekana ni Usalama wa Taifa ndiyo wamegundua janja hii ya Tanzania kuhujumiwa na wanasiasa.
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,094
2,000
Chezea Watutsi..Sasa ka-game project yake ni kumpatia Silas Rwakabamba urais wa Tanzania. Msisahau watutsi, urais uwaziri na ukuu wa majeshi ndio kazi wanazozitafuta haijalishi nchi gani!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom