Kagaigai ‘awaka’ Tsh milioni 3.3 kununua bastola

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
8,226
13,159
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameagiza wahusika walioidhinisha malipo ya Sh3.2 milioni kwa ajili ya ununuzi wa bastola ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kuzirejesha.

Alisema taratibu za ununuzi wa silaha hiyo zilikiukwa.

Kagaigai alisema hayo jana, alipozungumza katika kikao cha baraza la madiwani wilayani hapa.

“Tangu mwaka jana sioni jitihada ambazo zimefanyika, menejimenti ifuatilie hizi fedha zirudi, vinginevyo mimi nimeandika ni ubadhirifu kwa kuidhinisha matumizi ambayo sio sahihi,” alisema Kagaigai.

“Haiwezekani mwaka mzima hamjafuatilia fedha na bastola ziko huko, hamtendei haki fedha za wananchi.”

Akizungumzia suala hilo, aliyekuwa meya wa manispaa hiyo ambaye ni Diwani wa Bomambuzi, Juma Raibu alisema suala la ununuzi wa bastola lilikiukwa na haiwezekani inunuliwe kwa matumizi ya mtu binafsi.

ADVERTISEMENT
“Tuliliagiza baraza la madiwani lililopita kwamba ununuzi wa bastola ya Sh3.20 milioni iliyokuwa inunuliwe kwa sababu ya mkurugenzi, fedha hizo zirudishwe halmashauri, haiwezekani mkurugenzi wa manispaa kununua bastola kwa fedha za halmashauri,” alisema Raibu.

Akitolea ufafanuzi wa sakata hilo, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Stewart Nkinda alisema fedha za ununuzi wa bastola ya mkurugenzi zilipewa baraka zote na baraza la madiwani.

“Baraza la madiwani lilitoa baraka na pistol (bastola) ya mkurugenzi ikalipiwa fedha, hapa ninachokiona kwenye hoja ya mkaguzi ni namna hizi fedha zilipaswa kurudishwa halmashauri kutoka kwa supplier wa hizo bastola.”

Chanzo: Mwananchi
 

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,632
13,978

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
11,162
12,868
Yaani bastola binafsi imenunuliwa kwa pesa za umma?

Hivi Hawa watu huwa wanajiamini kwa lipi hasa?
Hiyo ni kawaida sana kwenye hii nchi yetu, sema huyo mmoja ndo wamemshtukia. Lakini ukiamua kufanya uchunguzi nchi nzima wako wengi sana kuanzia ngazi za juu. Huyu mmoja ambaye naweza kusema ni "dagaa" wanataka kumwonea tu!! Kama hivyo itolewe kauli kuwa WOTE WALIONUNULIWA SILAHA ZA MOTO KWA FEDHA YA SERIKALI WAVIRUDISHE. Utashangaa huo mtiti!!
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
30,149
30,967
1.5 unapata bastola nzuri tu yakufumulia bongo za wezi wa mali za uma maana kuwanyonga ni kuwachelewesha sana kwenda motoni.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
17,859
31,377
Kwani yake au ya taasisi
Nikueleweshe tu Mjumbe,
Sheria ya umiliki wa silaha na kanuni zake inataka Mmiliki awe Mtu au taasisi. Kwa silaha kama hii ya Pistol moja haiwezi kumilikiwa na Taasisi ya Halmashauri Bali itamilikiwa na Mtu mwenye cheo cha DED na Kwa maana hiyo lazima imilikiwe Kwa jina maana anatakiwa apewe mafunzo ya umiliki na utumiaji silaha. Tatizo litakuja pale atakapoahamishwa Halmashauri huku Leseni ya Umiliki ikiwa na jina lake na mafunzo akiwa amepata yeye na Aina ya silaha ni ya matumizi ya kujilinda binafsi.
Waliopitisha manunuzi hayo aidha hawakuwa na uelewa au walifanya makusudi kumfaidisha DED kutokana na mahusiano mazuri Kati yao.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
8,464
22,015
Milioni 3.3 tu kelele nyingi.
Kwani kuna ulazima gani mtumishi (kiongozi) kuwa na bastola tena ya kununuliwa?
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
17,086
26,213
Vituko vya wabadhirifu
Halafu eti utasikia upumbavu kutoka kwa wapumbavu ''mwache mama kwanza ajenge nchi''. Huu ujambazi wa mchana wa fedha za wananchi uko kila sehemu ya nchi yetu na unafanyika usiku na mchana. Ni kwa sababu ya mfumo wetu wa utawala mbovu. Bila kuufumua na kujenga mfupo mpya ambao wananchi ndiyo watakuwa na control ya matumizi ya fedha zao ni bure. Mkurugenzi na bastola wapi na wapi. Anashughulika na uhalifu?
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom