Najua habari hii imetoka kwa Kafumu mwenyewe. Anavyopenda ukubwa anajipigia debe ili apate Uwaziri, tena wa Wizara ya Nishati na Madini. Historia yake inaeleweka tangu akiwa Chuo Kikuu DSM alipokuwa kinara wa kikundi cha Punch. Kwa lipi ambalo amefanya hadi kupewa Uwaziri? Mbona wapo Wabunge wengi wazoefu ambao wanastahili kupewa nafasi hiyo kama kweli Rais amechoka na Ngeleja? Taarifa hii ni ya kupuuza kabisa, ikiwa ni kweli, basi Wizara ya Nishati na Madini wamekwisha, maana huyu Bwana ni mpumzikaji ajabu. Alipokuwa Kamishna wa Madini, alikuwa siku zote anawaza safari za nje ya nchi tu. Idara ya Madini yenyewe ilimshinda, sembuse Uwaziri? KWA HILI, Ikulu itakuwa imekosea njia kwa kiwango kikubwa.