Kafulila....:wanafiki na vipofu wa tanzania ktk tasnia ya siasa mfe mara moja kwa upumbavu wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila....:wanafiki na vipofu wa tanzania ktk tasnia ya siasa mfe mara moja kwa upumbavu wenu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wabusara, Dec 15, 2011.

 1. w

  wabusara Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi sasa na kwa muda mrefu hali ya watu ya kutofanya uchunguzi na uchambuzi wa masuala mbalimbali kwa umakini na kina cha kutosha vinazidi kushika kasi hapa nchini, hii ni kutokana na kile kuwa watu fulani wamekuwa BENDERA fuata upepo,kwa mfano inashangaza kuona na kusikia kuwa watu wanalalamika baada ya katibu mkuu wa nccr mageuzi kumvua ukatibu mwenezi wa chama bw. KAFULILA aka Bw. MIGOGORO eti kwa sababu ni mtu maarufu,mara wengine kafulila ni mjenga hoja mzuri bungeni nk,JE, HIYO NI SABABU YA YEYE AKIFANYA MAKOSA ASIADHIBIWE? Anayesema ndiyo,basi ndiye Mnafiki na kipofu wa Tanzania ktk tasnia ya siasa na mpumbavu wa kwanza, nasema hivyo kwa sababu haitoshi kwa mtu mzima mwenye akili timamu akaamtetea mwovu aina ya kafulila ambaye sababu za kumpinga zipo na za kutosha kama ambavyo Mh. machali alivyowahi kueleza, Kafulila siyo mungu na kwamba ahwezi kukosea, ni mkosefu kama ilivyo kwa binadamu wengine,fanyeni utafiti mtakubaliana nami kuhusu uovu wa kafulila,ni mtu mwongo,mzushi na mnafiki kama baadhi ya watanzania wanaomtetea huyu jamaa bila kujua ukweli wa mambo yanayomkabili hivi sasa. Rejeeni alipofukuzwa Chadema na Dr.slaa,ina maana kila siku watu wanamuone yeye tu?kwa lipi au yapi ya kumuonea? Ondoeni upofu msije mkazidi kulaaniwa kama ambavyo baadfhi yetu wameshalaaniwa na kutaka kuwaaminisha watu wote waone kafulila anaonewa, huu ni ujinga wa hali ya juu, na itakuwa ni ujinga uliokithiri kwa watu kumuamini na kujifanya vipofu kwa nmtu anayependa kanzisha mitafaruku kila anapokaribishwa mahala fulani, tusisahau yale ya Chadema walipomfukuza chini ya Dr. SLAA, Hakuwa mwehu kumshughurikia kafulila hadi kuamua kumuita sisimizi kafulila, leo yupo nccr anafanya mambo kama yale yale, tuepuke tabia ya kumtetea mtu anayemzushia mwenzake hata kama ni mkosaji kiasi gani, hapa kinachoonekana ni kuwa baadhi ya watu wanamuona MBATIA kuwa mkosefu ktk jamii kwa sababu zao binafsi na nyingi ni za kizushi kama kafulila, kumuona hivyo mbatia haimaanishi kuwa hawezi kukosewa na akaamua kuchukua hatua? anayepinga hili ni mpumbavu kupita amelezo,
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wabusara najua ww ni NCCR lakini nakuomba usiwe na Matusi na Jaziba kama Mbatia bosi wako jenga hoja.Hapa usigombane na watu usiowaona.Mimi naweza kukuunga mkono kama utanisaidia busara zifuatazo:1.Kwa nini Mbowe kamukataa Mbatia katika orodha ya Wapinzani. 2.Wdwe uliwahi kusema ni Chadema je kwa nini Mbowe kawakataa wabunge wa NCCR kwenye kambi ya upinzani?. 3.Kwa nini Mbatia amehojiwa na CRDB benki tawi la Mbez Beach wakati wa kuhamisha kiasi kikubwa cha fedha na kufungua ankaunti nyingine mda mfupi baada ya Faustin Sungura kumwagiwa tindikali? 4.Kwa nini Mbatia ameficha ukweli juu ya msaada wa 50m kutoka kwa Sabodo ambaye anatoa msaada kwa vyama vyote na si kukopesha? 5.Kwa nini Mbatia amefungua kesi dhidi ya Mdee ili hali Yeye ni mtu wa tatu? Wakati mtu wapi ccm katulia?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,551
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu wabusara, unatumia jina zuri wabusara kana kwamba una busara kweli kumbe si lolote!. Haya uliyoandika humu ndio unajieleza wewe mwenyewe jinsi ulivyo!.
  Naanzia kwenye hoja na kumalizia na mleta hoja.

  Nilibahatika kumsikia Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi alipokuwa ukitoa sababu za kumvua ukatibu mwenezi Mhe. Kafulila. Naomba tuwa wakweli ndani ya nafsi zetu, jee sababu zilizotajwa ni genuine?!. Wewe unajua zilikuwa kisingizio tuu, sababu halisi wewe unazijua kama ambavyo Ruhuza, Mbatia, Kafulila na wengine wanavyozijua. Kitendo cha kumvua ukatibu mwenezi Kafulila kwa kutoa sababu za scapegoat sio tuu ni unafiki, bali huo ni utoto wa ...!

  Zipo hoja za msingi kuhusu situation ya NCCR Mageuzi na genuine issues that needs serious addressing. Badala ya kushughulikia raised issues mnashughulikia watu!.

  Wawe kama mchambuzi makini wa siasa za Tanzania, uliefanya utafiti wa kina kuhusu uovu wa Kafulila, nilitegemea ungetuletea humu hayo matokeo ya utafiti wako huku ukitumia sababu za usisimizi za Chadema kama reference tuu!. Bado tunasubiri matokeo ya huo utafiti wako wa uovu wa Kafulila!

  Baada ya kumalizana na hoja, natanguliza samahani, kwa kumshambulia mleta hoja kwa kutumia lugha kali za kutukana!.

  1. Wewe wabusara ndio mpumbavu kupita maelezo!. Hivi huwezi kujenga hoja bila kutukana watu ni wapumbavu kupita maelezo?!.
  2.Wewe wabusara ndio mnafiki na kipofu wa Tanzania katika tasnia ya siasa na mpumbavu wa kwanza!. Hivi umeshindwa kujenga hoja bila kuwatukana watu wanafiki, vipofu na wapumbavu wa kwanza?.
  3. Wewe wabusara, ndio mtu mwenye ujinga uliokithiri. Umeshindwa kujenga hoja bila kutukana watu wajinga waliokithiri?.

  Mimi naamini bado unaweza kujenga hoja bila kuwa provoke watu kwa matukano na hoja yako bado ikawa na mashiko.

  Pasco.
   
Loading...