Kafulila uliingia Bungeni kwa "Ndondokela"; Sasa uje kuijenga NCCR inayokufa!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Amani iwe kwenu.

Nimeamua kuandika haya ili kumpa ujumbe mahsusi David Kafulila pamoja na vijana wengine wanaojiingiza kwenye siasa Kipindi cha uchaguzi wakikosa fursa ya ubunge au udiwani basi huvitupa vyama vyao.

Ikumbukwe kuwa Kafulila alijiunga NCCR siku chache kabla ya uchaguzi mkuu 2010 baada ya kutoelewana na viongozi wa CHADEMA hadi kupelekea yeye,Machali na Mkosamali kuitwa "Sisimizi".Naum,walipata fursa kugombea kupitia NCCR na kufanikiwa kutwaa Ubunge bila hata kuelewa katiba wala itikadi ya chama hicho.

Sasa baada ya kushindwa ubunge huna budi kukijenga chama jimboni hapo Uvinza na kitaifa kwani Mbatia kakiuwa kwa kulambishwa Ubunge.

Huu ni ushauri muhimu labda kama huna nia ya kuendelea na siasa.Tumia ushawishi wako kukijenga chama ili kukiondoa mikononi mwa CHADEMA ambao wageuza kuwa tawi lao na Mbatia kuwa Msemaji wao.

Nawasilisha.
 
Dah masikin lowasa aliwadanganya akaanza mashambulizi kwa zitto mwishowe akambulia za uso
Pole sana kafulila kwa kufulia
 
Muosha huoshwa @wa kudadavua!!!!!! Alifurahia sana muda ule kucheza mpira wa Machache ili kumdhibiti Prof. Muhongo...aende kwake sasa hivi atatunzwa tu kifedha kama zile alizopewa muda ule zimeisha....
 
Ikumbukwe pia Zitto ndiye alimpigania Kafulila baada ya kuletewa mzengwe Chadema,akamshauri agombee kupitia NCCR na akamsaidia hili lilimfanya Zitto kuitwa msaliti.
 
Muosha huoshwa @wa kudadavua!!!!!! Alifurahia sana muda ule kucheza mpira wa Machache ili kumdhibiti Prof. Muhongo...aende kwake sasa hivi atatunzwa tu kifedha kama zile alizopewa muda ule zimeisha....
Ilikuwa lazima afanye ili ku"retire" imprest.
 
kafulila alifanya kosa kumuunga mkono fisadi lowasa.....angejiunga na mzalendo zitto angekuwa mbunge sasa hivi
 
Nilivyomuona jana sikuweza kumfahamu harakaharaka,amechoka sana aisee,next time aache upuuzi atapata,haiwezekani unagombana na mpinzani mwenzako kwa sababu za kitoto,omba msamaha kwa zzk
 
Kajinga sana hako kadogo, we mtu makamo ya bibi yake kalimdhalilisha bungeni mpaka akakaita "Mwanangu Kafulila naomba ukae kwanza" kenyewe mishipa ya shingo imekisimama kama jogoo kuchi. Yaani hakakuwa na heshima kabisa, kakawaambi wana kigoma eti wasifuate chama cha Zitto kwani eti ni cha waha watupu, kakawaambia bora waanzishe chama cha mawese!
 
kigoma kuna mawese na inahitaji mtu wa kuwapigania ukimwondoa wabunge waliochaguliwa,nadhani ni wakati wa kafulila kusimamia na kuwatetea wakulima wa mawese kwa muda huu....bila kusahau kuwa kuna mvurugano ndani ya nccr yeye kashamature vya kutosha arudi chamani akaendeleze chama.......
 
Asante Mkuu kwa kuliona hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom