Kafulila, hiyo sio njia sahihi ya kujenga chama chako cha NCCR- Mageuzi

"kwa kweli chadema hawana mindset na ndio maana wanaanguka ovyo ovyo kila saa,
mm nnawapa pole"

Sina hakika kama neno 'mindset' hapa ni mahala pake, lakini pia neno kuanguaka 'ovyo ovyo' sijui ulikuwa unamlenga Kikwete!!!
 
It's more a partisan conclusion than anything.

Ni misemo yenu ktk lugha ya Kiswahili inayoleta hisia kuwa "umoja ni nguvu". Kwa mfano mlipoungana na Z'bar na kiua Tanganyika....ni nguvu zipi mmepata ambazo hapo kwanza hamkuwa nazo?

Je Tz ya leo ni faida gani inazo kulinganisha na Tanganyika..... au Z'bar in that matter. Ni nguvu ipi mnazo leo?
 
Mbunge anayeshambulia chama pinzani wakati na yeye ni mpinzani na kushangiliwa na CCM hawezi kujiita mpinzani nikamuelewa.. Maneno ya Kafulila yanaonyesha bado ana chuki kutimuliwa CHADEMA. Badala ya kupingana na ccm/serikali ili kuifanya iwe makini anakazana kupingana na chadema halafu anafurahia kushangiliwa na wabunge wa chama tawala.... shame on him.:twitch:
 
..sasa hii move ya kina Kafulila imewasaidia vipi wapinzani?

..au lile tamko la Mtatiro wa CUF akiwashutumu na kuwatukana CDM linawapa picha gani?

..hivi mnategemea kuchaguliwa kwa Mrema na Cheyo kuongoza zile kamati kutaliletea taifa hili tija yoyote?

..kwa mtizamo wangu kura za wananchi ndizo zilizowafikisha Chadema ktk nafasi waliyonayo bungeni.

..anayehujumu na kuwachimba Chadema anakuwa amekosa heshima kwa wapiga kura walioipa Chadema ushindi wa pili bungeni.

..ifike mahali siasa ziwe za HAKI na UKWELI, siyo ujanja-ujanja[tactics], fitina, na hujuma.
 
Wanaoshabikia kinachoshabikia wabunge wa ccm nadhani hawajajiuliza swali hili,

Hivi simba wanaweza wakashangilia na kushabikia wakati wanyama wengine wakiungana na kununua silaha ili wawawinde wao ?

Muda utatuambia nani alikuwa sahihi.
 
Mimi sijawai kuwa na imani na mwanasiasa ila nataka niwambie huyo kafulila namfahamu kabla ata hajawa na ndoto za siasa ni mtu ambaye anautaifa kweli labda wamwaribu sasa,kama mwanadamu anaweza kupotoka ila dhamira yake ni ya utaifa,tusinvunje moyo mapema,kafulila big up ni zaidi ya hata hao tunao wasikiaga
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom