Kafulila: Ripoti ya IMF yaiweka serikali katika wakati mgumu

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
1.Ripoti imeendelea kusisitiza eneo la ukuaji wa uchumi kuwa unakua kwa kasi nzuri ya asilimia 7% , jambo ambalo nimesisitiza mara kadhaa kuwa ukuaji huo upo tangu 2005/06 ambapo uchumi ulirekodiwa kukua kwa asilimia 6.9 kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya mwisho utawala wa Mkapa.hivyo sio jambo jipya. Pia imesisitiza kuhusu mafanikio katika ukusanyaji wa kodi ambao hakuna ubishi kwamba wastani wa makusanyo umeongezeka kutoka 800bn kwa mwezi mpaka 1100bn kwa mwezi.Na Mapambano dhidi ya ufisadi ambayo ni wazi Mhe Rais ameonekana kuonesha dhamira na kuchukuwa hatua ingawa bado kuna changamoto ya kujenga mfumo wenye nguvu ili vita iyo iwe endelevu na uhakika zaidi.(hapa lazma Bunge, Kamati ya PAC na Media), vipewe nguvu ya kutosha kama taasisi za msingi ktk kusimamia uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa.

2. Ripoti imesisitiza kuwa uchumi unakabiliwa na ukata. na kwamba kutatua hilo serikali inapaswa kuhakikisha sekta binafsi inapata mikopo ili kuchangamsha biashara. hii ni changamoto kubwa kwa serikali hasa kutokana na uamuzi wake wa kukopa bank za ndani kiasi cha 1200bn ili kugharamia bajeti.Uamuzi huu wa kukopa ndani utapunguza fursa ya bank za biashara kukopesha sekta binafsi na hali hii itazidisha ukata na mdororo wa biashara (austerity) kwani biashara zitazidi kudorola na mzunguko wa pesa kwenye uchumi kupungua

3.Ukata huu nimepata kuzungumza kwenye kipindi startv na hata channel ten kwamba asili yake kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya sekta binafsi kukosa mikopo bank zaidi na sio pesa za dili tu kama ilivokuwa ikijaribu kuaminishwa. ukweli huu ni kwa mujibu wa report ya robo mwaka ya tathimini ya uchumi(quartely economic review July-sept2016), ambapo ilibainisha kwamba ujazo wa fedha kwa mfano katika robo hiyo uliongezeka kwa kiasi cha 913bn tu ukilinganisha na ongezeko la ujazo wa fedha kiasi cha 3000bnkipindi kama hicho mwaka uliotangulia 2015.(2016 imekuwa pungufu kwa zaidi ya 300%) na kwamba hiyo ndio sababu ya ukata.bank hazitoi mikopo kwa sekta binafsi.

4.Serikali imeambiwa ikope nje kukabili uwekezaji wake kwenye miradi ya maendeleo. Hii kwanza inatuma ujumbe kwamba kwa hali ya mdororo wa uchumi iliyopo kukopa ndani sio afya. lakini inaipa changamoto serikali kuitaka ikope nje ambako imeshakosa hata kuamua kubanana na sekta binafsi kwenye bank za ndani. miradi ya maendeleo mingi imekwama na kwa mujibu wa ripoti ya Monthly economic review na Quartely economic review za mwaka huu zinazotolewa na Bank kuu, zinaonesha wazi kuzorota kwa miradi ya maendeleo kutokana na serikali kukosa pesa kumudu miradi. kwa mfano, kwa mujibu ripoti ya robo mwaka kuanzia July mpaka Sept,2016, Miradi ya maendeleo ya kibajeti iliyotemegea mikopo toka nje kiasi cha 1797bn katika kipindi hicho iliambulia 249bn sawa na asilimia 13% ya utekelezaji wa bajeti ya miradi huyo. na hata ripoti ya tathimini ya mwezi oktoba( monthly economic review) ya mwezi huo iliyotoka mwezi Novemba , inaonesha kwamba miradi ya kibajeti iliyopaswa kutekelezwa mwezi huo kwa kutegemea mikopo na misaada toka nje ilikuwa ya thamani ya 276bn lakini pesa ilopatiakana ilikua ni 45bn ,sawa na asilimia 16% ya utekelezaji. Hali ni hiyo kwa miezi yote kwa miradi iliyotegemea pesa za mikopo na misaada toka nje. na kwa ujumla, utekelezaji wa miradi yote iliyotegemea pesa za mikopo ya ndani na ile ya nje pamoja na misaada, utekelezaji wake ni takribani asilimia30%, kwa maana kwamba asilimia 70% ya miradi ya maendeleo ilopishwa na bunge haitatekelezwa.na hapa ikumbukwe kuwa tayari tumevunja rekodi ya muda mrefu ya kiasi cha kukopa ndani. kwani wakati kwa miaka10, deni la ndani liliobgezeka toka 1.7trilion mpaka 7.5trilion, kwa mwaka mmoja, sasa deni la ndani limefika zaidi ya 10trilion, hii sio afya hasa katika uchumi ambao umedorola( austerity economy).

5.Ripoti ya IMF imeonesha kwamba nakisi katika akaunti ya biashara kimataifa imeshuka. ni jambo jema na afya kiuchumi(uagizaji nje kupungua ukiwianisha na uuzaji nje), lakini ripoti hiyo inaenda mbali zaidi kuonesha kwamba nakisi hiyo imeshuka kutokana na kupungua kwa uagizaji wa malighafi za viwanda(capital goods). Ingekuwa kwamba nakisi imeshuka kwa kupunguza uagizaji wa bidhaa zisio za uzalishaji ingekuwa afya, lakin kushuka kwa nakisi hiyo kunakotokana na kushuka kwa uagizaji wa bidhaa ambazo ni muhimu kwa ajili ya uzalishaji viwandani ni kasoro hasa katika mazingira ambapo serikali inatengaza uchumi wa viwanda. hoja hii inathibitishwa pia na ripoti za tathimini za Bank Kuu , ambapo kwa mfano katika robo ya mwaka ya July- septmba,2016, nakisi ya akaunti hiyo ilishuka toka $1.207bn mpaka $601.8m sawa na kushuka kwa 50%,kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka 2015.

wakati nakisi ilishuka kwa takribani $600m, ukiangalia ripoti ya robo mwaka inayoishia septemba, 2016, inaonesha wazi kwamba bidhaa zilizopungua kwa kiasi kikubwa kuagizwa nje (imports) ni mashine na mitambo iliyopungua toka$433.5m mpaka $298.7m sawa na tofauti ya $134.5m na malighafi kwajili ya viwanda(capital goods) zilizopungua toka $911m mpaka $695m. hivyo wakati nakisi ya akaunti uagizaji nje ilipungua kwa takriban $600m ($1207m-$601.8m), uagizaji wa mitambo na malighafi za viwanda ulipungua kwa takribani $350m. na huu ni ushaidi kwamba kwamba kushuka kwa nakisi hiyo hakuna tija kiuchumi kwakuwa bidhaa zilizochangia kwa kiasi kikubwa mahususi kwajili ya viwanda hizo ni alama ya ukuaji wa uchumi wa viwanda.
 
KAFULILA ANAHANHAIKA NA MAPAMBIO YA KISIFU NA KUABUDU.

anabadilisha sauti tu.

Hujafa hujaumbika
 
Ukosoaji wa David Kafulila kabla hajaonja maji ya kijani yaliyobeba laana..

Kwa sasa akiambiwa kuwa yeye ndiye aliyeanadika haya, bila shaka ataruka kimanga mita 100...!
 
Kumbe hii ilikuwa kabla kafulioa hajafulia nilidhanu sasa
 
Back
Top Bottom