Kafulila na kura ya kutokuwa na imani na waziri Ngeleja

YeshuaHaMelech

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
2,597
37
mbunge wa kigoma kusini ana mpango wa kupeleka hoja binafsi ya kutokuwa na imani na waziri Ngeleja kutokana na issue ya umeme na mgao usioeleweka! Hakumtaja Ngeleja kwa jina bali kwa cheo chake. Anasema umeme usioeleweka ni tatizo kuliko mtikisiko wa uchumi
source Taarifa ya saa 2 ITV
 
Hii ni nzuri ingawa hii serikali ya CCM bado inajifanya kicha ngumu....Ngeleja hafai na hata mfumo mzima wa huduma ya umeme hapa nchini ni ovyo kabisa.......
 
Hiyo wizara nyeti ilitakiwa iwe na waziri kichwa siyo hii mitandao ya ufisadi in practice hawa mawaziri wizara wanapwaya hawafai zaidi ya kuwa wapiga porojo
 
Hiyo hoja itakuwa imekaaje na kanuni za bunge zinasemaje kuhusu hilo?
 
Hii hoja inaweza ikawa nzuri lkn kwa mfumo tulio nao wa kusifia tu viongozi, am afraid it's doomed to fail kwenye parliament. But, ni kiamsha usingizi kwa waliolala na kutetea wananchi
 
asije kuwa anapiga kidomo tu maana sijaona kanunii za hoja binafsi akiitaja kujua anaweza kufanikiwa au la; otherwise tutamuunga mkono maana analopigania halina chama wote twaumia kwa mijoto hapa
 
Juzijuzi rais kwenye hotuba yake bungeni alijisifu kuwa ndani ya uongozi wake idadi ya watanzania wanaotumia umeme imeongezeka. Sasa umeme wanaotumia hao wananchi ni huu wa mgawo au!!!
 
Inawezekana ila itakuwa kazi kuwabadilisha wale jamaa wabunge ccm manake kwao si manufaa kwa taifa bali ubinafsi wa mabosi wao!
 
Ningependa hiyo kura ya kutokuwa na imani na waziri ijumuishe na watendaji wa wizara pamoja na mhandisi wa umeme Tanesco hawa watu wanatakiwa wawe na sera ya kumaliza hili tatizo yenye kutekelezeka na sio ya muda mfupi.
 
Akijenga hoja nzuri na kutokana na hali ya Dowans itakavyokuwa imeendelea, basi lolote laweza kutokea!
 
teh teh wanasema umbea ni uharo, kuubana huwezi.
Hili sakata la huu mgao tutakuja kulijuwa tu na nina imani tutajuwa tu kama kuna kibopa ana majenereta yake na sasa anataka kuyauza au la...
 
mbunge wa kigoma kusini ana mpango wa kupeleka hoja binafsi ya kutokuwa na imani na waziri Ngeleja kutokana na issue ya umeme na mgao usioeleweka! Hakumtaja Ngeleja kwa jina bali kwa cheo chake. Anasema umeme usioeleweka ni tatizo kuliko mtikisiko wa uchumi
source Taarifa ya saa 2 ITV


Hii imekaa vizuri naomba wabunge wote hata wa CCM waunge hoja hii ya Kafulila.

Wizara ya nishati na madini ina umuhimu mkubwa sana kwa uchumi wa nchi yoyote ile, hasa upande wa nishati kwa mwendo huu mwekazaji hawezi kuja TZ kuweka investment kubwa itakayo operate ktk mazingira haya, hembu angalia hata ndugu zetu wenye viwanda vidogovidogo na masaluni wanalala mchana baada ya kufanya kazi umeme hakuna kutwa nzima alafu unasema maisha bora kwa kila mtamzania, hii haiwezekani.

Hii ni wizara inayotaka watu vichwa wa waukweli kama tungepata Magufuli na Mwkyembe wengine wakabidhiwe hii wizara labda mabadiliko yangeonekana. hawa jamaa si walikuwepo awamu ya kwanza ya JK hembu tuwafanyie assessment walifanya nini kuiokoa sekta ya nishati na taifa kwa ujumla.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom