KAFULILA:"MAONI yangu juu ya marekebisho ya sheria ya KATIBA- Hakuna Jipya" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KAFULILA:"MAONI yangu juu ya marekebisho ya sheria ya KATIBA- Hakuna Jipya"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by April, Feb 9, 2012.

 1. April

  April Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  [FONT=&quot]
  Kufuatia kupitishwa kwa SHERIA ya marekebisho ya KATIBA leo Bungeni, Mh. Kafulila atoa maoni yake akitofautiana na maamuzi yaliyopitishwa leo. Mh. Kafulila ameandika waraka huu akiufafanulia UMMA juu ya mchakato huo uliopitishwa jinsi gani hauna TIJA wala hautaleta mabadiliko yoyote ambayo wanaharakati na wananchi kwa ujumla wameazimia.

  MAONI YA MH. DAVID KAFULILA

  Habari Watanzania,
  [/FONT]

  [FONT=&quot]Nina maoni tofauti kuhusu hiki kinachoendelea kuhusu marekebisho ya sheria ya kusimamia mchakato wa katiba mpya.
  Nimejaribu kuomba kuchangia ili niweke maoni yangu wazi lakini imeshindikana, Spika amesema NCCR amepewa mtu mmoja tu Mh. Machali hivyo nikaona ni vema niwajulishe kupitia mtandao maoni yangu.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]

  [FONT=&quot]UTANGULIZI[/FONT]

  [FONT=&quot]Hapa ningependa kukumbusha kuwa kutoka NCCR ni mimi David Kafulila na Felix Mkosamali ambao tulikuwa wajumbe wa kamati ya sheria na Utawala. Mh.Mkosamali ni mjumbe wa kudumu kwenye kamati hii, mimi ni miongoni mwa wajumbe walio ongezwa wakati wa kupitia muswada huu. Pia ikumbukwe kuwa ni mimi na Mkosamali ambao tuliungana na CHADEMA kutoka nje katika mkutano wa tano wa Bunge kupinga namna mchakato ulivyoendeshwa. Niliomba kuchangia bungeni lakini imeshindikana kabisa kupata nafasi lakini kwa kuzingatia umuhimu wa jambo hili na nafasi niliyokuwa nayo katika jambo hili naona kuna umuhimu wa kuzungumza kitu kwani hata wale mabalozi wa nchi tano za Ulaya walipokuja bungeni kwenye mkutano wa tano ni mimi niliyekuwa mmoja wa wabunge waliokutana nao kutoa maoni.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MAONI[/FONT]

  [FONT=&quot]Nimeshangaa kuona mvutano wa kisiasa kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na serikali kwani ninavyofahamu kuna mambo mengi ya msingi katika sheria hii ambayo yalipaswa kubadilishwa, na nilidhani ndiyo yangeletwa kwenye marekebisho ya sheria hii baada ya vikao vya Rais na wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa. Mabadiliko yaliyoletwa sio issues za msingi ambazo zingesaidia kuiboresha tume na mchakato mzima wa katiba mpya.

  Kwa mfano;
  [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]

  [FONT=&quot]1. Hoja ya kumwondoa DC na Kuweka Mkurugenzi (DED)[/FONT]

  [FONT=&quot]Wabunge wengi wa CCM wanataka DC ndio asimamie, wakati hotuba ya kambi rasmi ya upinzani inapendekeza DED.
  Ukweli ni kwamba wote DED na DC hawafai kwasababu wote ni sehemu ya serikali na badala yake ilipaswa jukumu hilo litekelezwe na Tume yenyewe ambayo inapaswa kuwa huru.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2.Hapa ndipo inakuja hoja ya mchakato huu mzima wa kura ya maoni kusimamiwa na Tume huru.
  Uamuzi wa kuifanya Tume ya sasa ya Uchaguzi kusimamia mchakato huu ni kinyume cha msimamo wetu wa awali kama wapinzani kwasababu moja ya hoja ya mahitaji ya katiba mpya ni tume huru ya uchaguzi, sasa inawezekanaje tume mbovu ya uchaguzi isimamie mchakato wa kupata katiba huru?. Hili lilikuwa muhimu sana. Tungekubaliana kuhusu kupata kwanza tume huru ya uchaguzi kisha tume hiyo isimamie mchakato wa katiba mpya tungekuwa na uhakika wa kupata katiba ambayo watanzania wanaitaka.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3.Hoja ya Tume huru ya kusimamia mchakato wa katiba[/FONT]

  [FONT=&quot]Hii pia ni hoja iliyoachwa kwasababu Tume hii ya sasa inateuliwa na Rais na kwa namna ilivyo bado Rais ndio mwenye mamlaka ya kumtoa mjumbe yeyote. Marekebisho yaliyoletwa leo yanapendekeza namna ya kumtoa mjumbe wa tume hii ambaye anayetuhumiwa kukiuka kanuni za maadili, kwamba Rais atateua Kamati ya kufanya maamuzi. Hapa haikupaswa Rais kuteua kamati badala yake ilitakiwa sheria itamke rasmi kamati hiyo itakuwa akina nani ili kamati hiyo iwe huru kuliko iteuliwe na Rais, pengine kosa la mjumbe ni mvutano unaohusu nguvu za serikali kwa tume.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4. Hoja ya Sekretariet huru.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa mujibu wa sheria hii Sekratariet itaundwa na waziri mwenye dhamana. Hii inaondoa uhuru wa utendaji wa sekretariet, ilipaswa Sekretariet iteuliwe na Tume na iwajibike kwa tume ili kupunguza mkono wa serikali kwenye mchakato na utendaji wa kupata katiba mpya.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]5. Hoja ya ushiriki wa Jumuiya za kiraia, taasisi za dini vya vyama vya siasa[/FONT]

  [FONT=&quot]Marekebisho yaliyoletwa sehemu A, kifungu cha 7 yanatoa uhuru wa jumuiya hizi kushiriki kwa kualikwa na Rais, lakini sehemu hiyo hiyo ya marekebisho kifungu cha 8 inatamka kuwa Rais hafungwi na mapendekezo hayo kuteua watu wengine kuwa wajumbe. Hapa kwa tafsiri rahisi ni kwamba, haki imetolewa kwenye kifungu cha 7 na imepokonywa kwenye kifungu cha 8 kwa kuwaweka wananchi tayari wasishangae itakapotokea mapendekezo yaliyopelekwa na jumuiya yoyote kukataliwa yote. Ingepaswa kuweka wazi kuwa Rais atalazimika kuteua miongoni mwa walipendekezwa na sio nje ya waliopendekezwa.[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa ujumla pamoja na sheria hii kupitishwa leo lakini ina matundu makubwa sana kuweza kuifanya isimamie mchakato huu muhimu kwa uhakika. Bado ni sheria ambayo inategemea sana dhamira ya Rais mwenyewe kuliko mfumo tulioweka.

  Napenda ifahamike kuwa, sheria hii iliyopitishwa leo haijafanya mabadiliko ya msingi ambayo sisi sote ( wananchi, wanaharakati na wanasiasa) wenye moyo wa dhati wa kuleta mabadiliko kitaifa tulitazamia.

  Pamoja katika kujenga Taifa
  David Kafulila


  [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 2. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  naona unakasirika kwasababu wabunge wameondolewa
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Sasa kama NCCR wamepewa nafasi mmoja kwa nini huyo bwana asiwasilishe mawazo ya chama au kwa nini hukupeleka mawazo yako huko ili wayafanyie kazi na kuyawakilisha?? Au kwa vile NCCR wamekutimua then hakuna chama kinachoweza kukusikiliza tena??
   
 4. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Haya ni maoni ya Zito na huyu dogo wake, hawa jamaa wana matatizo ya akili.....
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  wacha umbumbumbu, kwanini usiwasilishe maoni yako kwa maandishi kwa spika au unataka show off, uonekane kwenye runinga halafu wananchi waone ulionewa na wakuonee huruma
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Si ndo hapo! Halafu pia hao N.C.C.R. si walienda kumwona rais pale ikulu? Kwanini hakupeleka maoni haya pamoja wakati wa ujumbe ule?
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Labda hafahamu kama kuna utaratibu huo?!?!
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Haya ndio maoni yangu na ufafanuzi japo kwa kifupi najua atasoma na kufanya rejea ya mabadiliko husika kama yalivyowasilishwa.
   
 9. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bongo usa nii tupu! Bunge la Katiba halija guswa kabisa! Uko sawa Kafulila!
   
 10. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mh kafulira ila wanachojaribu kukufanyia Ccm ni kukuweka kama pambo la mbunge endelea kupambana hii tutaihoj
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Ha ha ha aaaa PRO CDM ambao wanajigamba humu kuwa mawazo yao yamesikilizwa kumbe wameliwa na kuingizwa mjini. CDM mmeyaona hayooooooo ya kafulila?

   
 12. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Bwana Kafulila mjadala wa huo mswada uko Bungeni, na wewe ni Mbunge kwa nini usipeleke "schedule of amendment" na ukaitetee huko Bungeni?

  Ni sawa kueleza maoni yako binafsi, lakini nadhani kwa kuwa wewe ni mwakilishi na una haki ya kupeleka schedule of amendment, unapaswa ufanye hivyo, badala ya kulalamika. Ni heri ufanye sehemu yako hata kama amendment haita pita.
   
 13. P

  Paparazi Muwazi JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimeshangaa ametuletea sisi waandishi, wakati kwa kanuni za bunge. Mbunge hata akikosa nafasi ya kuzungumza anaweza kuchangia kwa maandishi, Kafulila angetumia hii njia kuibana serikali bungeni. Naona pia anaelekea kusahau kwa kuwa CHADEMA ilishasema kwenye vyombo vya habari baada ya mazungumzo na Rais kwamba muswada huu ungefanyiwa marekebisho kwa awamu. Awamu ya kwanza kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba, awamu ya pili kuhusu bunge la kutunga katiba na awamu ya tatu kuhusu kura ya maoni kusimamiwa na tume ya uchaguzi.

  Kafulila alipaswa kusema kwenye awamu hii ya kwanza kuna jambo gani lilipaswa kuwepo kwenye marekebisho ambalo halipo? Ndio angeweza kutusaidia vizuri zaidi waandishi. Hizo awamu zingine CHADEMA na wadau wengine wameshasema kwamba wanazisubiria kwenye hatua zinazofuata kwa kuwa huu ni mchakato wa mpaka mwaka 2014 kwa kadiri ya hotuba za Pinda na Kikwete.

  PM
   
 14. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mh Kafulila muambie huyo aliyekutuma ajipange upya alafu akutume tena,maana hoja hii haina mashiko!
   
 15. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu,

  Kama bunge limepitisha marekebisho ya sheria ya katiba na hakuna aliyepinga kwa maana aidha ya kutoa shilingi au kutoka nje sisi wananchi tunasema BUNGE limepitisha kwa kauli moja na hiyo ndiyo itakayokuwa sheria. Kama kanuni za bunge hazikukiukwa Kafulila akubaliane na matokeo maana uwezi kumridhisha kila mmoja.
   
 16. H

  Hume JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 338
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Kipengele kipi cha hoja yake ambacho hakina mashiko?
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kafulila na Hamad Rashid ndio waliokuwa mstari wa mbele wakimtaka Speaker kubadilisha kanuni za bunge ili tafsiri ya 'kambi ya upinzani' ibadilike. Na wawili hawa wamefukuzwa kwenye vyama vyao speaker wa CCM ameamua kwenye hii issue atajificha kwenye hoja ya separation of power ili wabunge hawa waendelee!

  Hadi leo sijaelewa ni kwanini Speaker au hata msajili wa vyama vya siasa wameamua kuwatetea hawa watu ili wabakie bungeni? Kafulila anafanya kazi za NCCR Mageuzi wa za CCM? Na hizi hoja alizoandika hapa ni za chama kipi? alikaa na mwenyekiti wa chama kipi?
   
 18. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  ahsante kwa taarifa yako kwa umma
   
 19. Malunkwi

  Malunkwi JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa hapa zitto anahuckaje?? au ndo walewale wabunge wa sisiem "They think small"...???????
   
 20. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 479
  Trophy Points: 80
  Sina hakika kuwa kikao kijacho utakuwepo, kwahiyo toa dukuduku lako la mwisho mapema ndugu!!!
   
Loading...