Kafulila kafulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila kafulia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, Dec 6, 2010.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Jimbo la Kigoma Kusini kupitia chama cha NCCR- Mageuzi, anakusudia kupeleka hoja binafsi katika Bunge la Februari 2011, kutaka Serikali iwajibike kwa kuliingiza Taifa hasara kwenye sekta ya umeme.

  Hoja hiyo ya Kafulila imekuja siku chache baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kushindwa kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kutakiwa kuilipa Kampuni ya Dowans Sh bilioni 185 kwa kuvunja mkataba kinyume na sheria.

  Katika hoja hiyo, Kafulila anataka Serikali aliyosema ndiyo inayopaswa kulipa deni hilo, kutoa maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufikia hapo, kwa sababu haitakuwa sahihi kulipa mabilioni ya fedha kwa kampuni aliyodai kuwa mmiliki wake hafahamiki.

  Kafulila pia anakusudia katika hoja hiyo, kulitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati na Mpango Kabambe wa Usambazaji wa Umeme nchini.

  Kwa mujibu wa madai ya Mbunge huyo, kushindwa kazi kwa Waziri huyo, kumesababisha kutokea kwa mgawo wa umeme nchini mara tatu ndani ya miaka miwili ya uongozaji wake.

  Akizungumza jana katika makao makuu ya chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam, Kafulila alisema kuwa mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya Watanzania.

  Kafulila aliendelea kudai kuwa haitawezekana kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ya uchumi wala ya huduma nchini kwa kuwa takwimu zinaonesha asilimia 40 ya uchumi duniani inategemea nishati ya umeme.

  Alidai chanzo kikubwa cha tatizo la umeme nchini ni Serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hilo na badala yake imebaki kusimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo alidai kwa miaka kadhaa sasa imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa.

  “Asilimia 86 ya mapato ya Tanesco yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote... hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba,” alidai.

  Alidai Tanesco inalipa Kampuni ya Songas takriban Sh milioni 266 kila siku kwa kununua megawati 86 za umeme na mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa, Tanesco inailipa kampuni hiyo Sh milioni 300 kila siku.

  “Tangu mwaka 2006 Serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo la mgao wa umeme huku viongozi wake hasa Waziri wa Nishati na Madini akipotosha Watanzania mara kadhaa kwamba Serikali inalishughulikia na mgao wa umeme utakuwa historia,” alidai.

  Alisema, Serikali inapaswa kuona athari ya matatizo ya umeme katika maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi na kuitaka ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme na wa uhakika kama wa makaa ya mawe Kiwira na gesi asilia ya Mnazi Bay.

  Kafulila alisema miradi yote inaweza kuendeshwa na sekta binafsi iwapo kutakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kuishauri mifuko ya hifadhi ya jamii iache kujenga majengo na ijielekeze katika uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme.

  Alidai kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza Tanesco iingie mkataba na Richmond na baadaye kuuhamisha mkataba huo kwa Kampuni ya Dowans na kwa kuwa Bunge ndio lilitoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na Tanesco ikafanya hivyo, shirika hilo lisibebeshwe lawama.

  Gazeti hili lilimtafuta Ngeleja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ili watoe ufafanuzi kuhusu hoja hiyo lakini hawakupatikana katika simu zao.

  Hata hivyo Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema ni mara yake ya kwanza kusikia Mbunge akitaka waziri mmoja, apigiwe kura na wabunge ya kutokuwa na imani naye.

  Alifafanua kuwa kisheria waziri anaweza kupigiwa kura hiyo endapo yeye binafsi atakuwa na tatizo la kimaadili. Dk. Kashililah alisema katika tatizo la umeme, Waziri Ngeleja anaiwakilisha Serikali hivyo hoja hiyo ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani kwake, haiwezi kuelekezwa kwake binafsi na badala yake inapaswa kuelekezwa kwa Serikali nzima.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,889
  Trophy Points: 280
  Tanzania is more than she is! whats wrong with core motive of Kafulila? mbona tunarukaruka palepale?? He is right, other errors are common and acceptable because of his inexperience in bunge!!! duh!!
   
 3. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  si kweli na hawezi kuwa sawa mrengo alioko ni wa ccm d
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,889
  Trophy Points: 280
  duh!!

  Kuna tatizo gani akiwa ccm D na still anasema vitu vya maan, mara ngapi huwa mnawasifia akina Sita, Mwakyembe,Magufuli walio CCM original? au mara ngapi vyama vya upinzani ikiwemo cdm imewapokea wana CCM original wakiwemo akin Slaa, shibuda na mpendazoe

  let me tell you, huyu jamaa mwacheni kabisa na chuki zenu zinaleta maswali mengi sana, ikiwa tunazungumzia u-ccm na unani, hapa then wengi cdm wametokea ccm hata muasisi wa chama! let debate on what he have said name calling will be pointing four big fingers toward you!!! lets not dig down.
   
 5. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Pumba!!

  Unaacha kujadili hoja iliyo ubaoni unaleta upuuzi wa vyama anakotoka mtoa hoja!!
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  kAFULIALA KASEMA KWELI HATA KAMA ALIHAMA CHADEMA NA KWENDA NCCR CHA MUSINGI NI HOJA YAKE. MBONA MARANDO ALIHAMA NCCR NA KUJITAMBULISHA KUWA ALIKUWA MTU WA USALAMA WA TAIFA LAKINI ALITOA SIRI NZITO KUWA KIKWETE, LOWASSA , ROSTAM NA MKAPA NI VINARA WA EPA NA KAGODA.


  GVT IMESEMA HAWAMUJUI DOWANS NA RICHGMOND WAKATI HATA MTU WA KAWAIDA ANAJUA WAMILIKI NI LOWASSA , KIKWETE NA ROSTA

  BOT YA KIKWETE ILIKUWA INA MULIPA NANI PESA ZA RICHMOND NA DOWANS

  HOJA YA KAFULILA NI NZURI KUWA WAMELIKI WATAJWE KWANZA KABLA YA KUWALIPA 185BILS VINGINEVYO ITAKUWA EPA
   
 7. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  No, because Kafulila isn't a member of CHADEMA.
   
 8. coby

  coby JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ikilipa TANESCO au SERIKALI Does it make the difference? I think All the burden is upon the citizens. Kama ni kujiuzuru kwa Waziri I think he has a point japo namna ya kuijengea hoja seems to be diffiucult kulingana na kanuni zetu
   
 9. papason

  papason JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280

  Duuu hii kali sasa!!
   
 10. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  jamani,hebu naomba niwaulize.....hivi kabla ya kuwa mbungu kisha waziri, NGELEJA alikua anafanya kazi gani??? Labda majibu yatatoa mwanga kuhusiana na hili suala....
   
 11. N

  Ng'wananshoma Member

  #11
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja iwasilishe, mengine baadae
   
 12. N

  Ng'wananshoma Member

  #12
  Dec 6, 2010
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa Tanzania huwa hawakubali ukweli na kujiuzulu kwao ni kwa mbinde kama kina Msabaha na mwenzake
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Tayari umewataja au ni joking?
   
 14. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  frezer
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  frezer
   
 16. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  kali sana nini?huna cha kusema unataka na wewe uonekane upo toa nyepesi hapa
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Frezer ina maana gani mkuu?
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  sijakuelewa,,frezer ndio nini au unaandika kihindi hapa?
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Dec 6, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,889
  Trophy Points: 280
  Alikuwa vodacom, alikuwa mwanasheria wa kampuni,
   
 20. E

  Epifania Senior Member

  #20
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Can't relate the heading and the contents, hayo aliyosema ni ya msingi sana. Ni aibu na fedheha. Tanzania inakuwa kama nchi isiyokuwa na viongozi kabisa. Naendelea kusisitiza, Mwanasheria mkuu wa serikali aliyekuwa madarakani wakati wa mikataba yote mpaka kufikia kupelekana mahakamani anapaswa kuwajibishwa ipasavyo. Inafika mahali mtu unakosa confidence ya kujivunia uTanzania kwa sababu ya upumbavu wa watu wachache wanaojijali wenyewe na si Taifa.
   
Loading...