Kafulila, hiyo sio njia sahihi ya kujenga chama chako cha NCCR- Mageuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila, hiyo sio njia sahihi ya kujenga chama chako cha NCCR- Mageuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zamlock, Feb 10, 2011.

 1. z

  zamlock JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kafulila kwa kweli wakati unachangia na kulazimisha ndoa kati ya watu ambao awajapendana nilikushanga sana bwana mdogo na sikukutegemea kama unaweza kufikia hatua ile na pia mara ya kwanza nilipokuona ukihutubia pale tegeta na kuwaponda ndugu zako caf na ccm nilisema chama cha nccr mageuzi kimepata mtu ambaye anaweza kukibadilisha na kikawa na mvuto kwa watu tena lakini kwa kile ulichikichangia jana bungeni na kuunga mkono ubadilishaji wa kanuni kwa kweli niliondoa imani yangu kwako na nikasema kama ndiyo njia unayotumia pia kuimalisha chana chako na kujipatia wanachama wapya basi ulikuwa umechemka na tayari umeshaondoa uwepo wako kwa wananchi na auna mvuto tena wa kisiasa.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  uChomete, kwa maoni yangu Kafulila is not only a good politician but also he has the powers to make things happen.

  Japo siungi mkono jinsi anavyoisakama Chadema lakini namkubali jamaa ni smart wa level ya kina Zitto, Mnyika, January, Nape and the like. This is their time.

  Hili la kulazimisha wapinzani waungane mbona pia ni la maana. Chadema tumeshawaambia mara kibao, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Wao wakaamua kuchagua udhaifu.

  Matacticians wazuri kwenye vita hutumia tactics za kuwatumia maadui zao kushinda vita.

  Baada ya Chadema kujua CUF ni maadui, walitakiwa kuwakaribisha nyumbani and use them for their advantage.

  Zitto amechaguliwa kuendelea na POAC kwa sababu amelithibitishia bunge he is over and above party politics akiwa bungeni. Kwake ni maslahi ya taifa mbele.

  Members, wafuasi, wapenzi na washabiki wa Chadema, washaurini viongozi wenu mjipange vizuri now than any other time before its too late!.
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyo kafulila amefulia muacheni tu!!
   
 4. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  crap..!
   
 5. m

  maselef JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ondoa Nape kwenye orodha
   
 6. M

  Majasho JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  point...tatizo chadema ni wanafiki...if you aint with them we ni adui yao,,,wanataka waungwe mkono wao tu..hoja yoyote ya kuwapinga hawataki..they cant admit when they are wrong....chadema inaongozwa na low minded ppl mbowe na slaa..wengine wanafuata upepo...

  ITS BETTER TUONGOZWE NA KICHAA (CCM) TUNAYEMJUA KULIKO AMBAYE HATUMJUI...chadema mkipewa nnchi mtatupeleka pabaya..******
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  First Lady unaposema just crap...! bila kufafanua chochote una maaninisha everthing ni crap. Basi kwa kukuheshimu wewe sio crap only that 'part 'of you must be crap...!
   
 8. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli chadema hawana mindset na ndio maana wanaanguka ovyo ovyo kila saa


  mm nnawapa pole
   
 9. Kagwina

  Kagwina Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati fulani mtu ukipenda chongo utaita kengeza na pengo utaita mwanya! Katika hili chadema wamechemka, Kafulila alikuwa sahihi, upinzani si ubinafsi, kama umepata kidogo hutaki kugawana na wenzako, ukipata kikubwa si utatuchapa viboko! Uaminifu unaanza katika mambo madogo, chadema tunawapenda lakini wasitupeleke huko na sisi wapenzi wao tuwe rational si kufuata upepo.
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ndg yangu Pasco vipi, nilidhani wewe wa maana kumbe ni wale wale bongo lala. Hukuona kuwa katiba yetu inachezewa, muda wowote mtu akitaka kubadili kanuani anfanya tu mradi wana majority. Kwa nini kanuni zibadilishwe pindi CDM WANAPO TAKA kuchukua hizo nafasi maana yake waendelee na madudu yao kwenye serikali maana hakuna wa kuwakemea!!!!!!!! Usifikili watu wote ni bongo lala kama unavyo onyesha, siri zitafichuka coz kuna wengi wana uchungu na nchi hii inavyoendeshwa kifisadi na kiwizi. Soma mwana Halisi ya jana 9/2/2011, pengine wewe ni kibaraka wa RA, NAONA wako wengi hata humu kwenye JF.Hapa hatuzungumzii chama bali kila Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake!!!!!!!!!!!!!!
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kafulila ni mtu makini sana, kwa hili la kubadilisha kanuni CHADEMA walichemka, na watanzania walio wengi hawako na nyie kwa kuonyesha uchoyo na uroho wa madaraka
   
 12. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pasco na wewe tumekuchoka, pamoja na kujifanya uko neutral lakini wapi rangi yako iko clear kabisa. Ngoja nikuulize hivi British Tax payer wanajua kuwa unatumia funds zao kuja kuwashambulia Chadema?
   
 13. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yaani wewe ndio bongo lala zaidi aisee, kwani wapinzani wengine hawana uchungu na nchi hii ila ni CHADEMA tu? acheni kujivika kilemba cha ukoka kwa hili mlichemka na halina ubisha
   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ndio wale wale mchovu huyu, utabana tuu mwisho utakubali. CDM PPL's!!!!!!!!
   
 15. k

  kayumba JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hivi hiyo kanuni imetungwa na CHADEMA baada ya kupata wabunge wengi?

  Tunachotaka wote waliochaguliwa walinde maslahi ya nchi, though i doubt it!

   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hoa wengine wapo pale kuwaziba ziba tuu na kusaidia mafisadi si upinzani rasimi. Ebu nikuulize Bwn Mrema TLP ni mpinzani????????? Au CUF ni mpinzani, mbona NCCR wanampeleka Mdee Courtini, hicho kiti kikipotea utasema ni wapinzani????????Si wanawatengenezea SISIEM nafasi. Upinzani halisi ni CDM wengine ni wasindikizaji tuu!!!!!!!!!
   
 17. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Maneno mazito sana haya mkuu.

  Kati ya Wabunge wachache sana walioanza kazi yao vizuri Kafulila ni mmoja wao, kwa aliyeshuhudia hoja yake ya jana Bungeni atakubaliana na mimi kuwa Kijana ana nafasi nzuri ya kufanikiwa sana kisiasa baadae.
   
 18. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
   
 19. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,052
  Likes Received: 8,538
  Trophy Points: 280
  Viva kafulila you da one
   
 20. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Huna akili nzuri wewe, badala ya kuchangia hoja unakuja na mambo ya kuanguka anguka, hivi umeona hili ni jukwaa la wapuuzi au?? Ndo matatizo ya kuwa na Internet ya bure ofisini inayolipiwa na serikali maskini ya CCm so unajifanyia utakavyo hata kuchangia upupu na kuiacha hoja pembeni. Ole wako, siku zenu nyie mabazazi mnaotuharibia hoja humu jamvini zinahesabika...
  Tukija kwenye hoja yenyewe ni kwamba yule Bw mdogo Kafulila ni mbishi sana, ana kimbelembele na mpenda sifa, hana hoja za maana kivile ndo maana juzi aligalagazwa sana na Simbachawene wa CCm katika Jambo TBC1. Kafulila anafaa kuwa katika vyama vidogo ambavyo havina mitazamo ya watu tofauti. Hafai CUF, CCM, CDM au hata NCCR ikiwa kubwa tena watamshindwa kwa ubinafsi na ubishi
   
Loading...