Che Mkira
Senior Member
- Jul 8, 2014
- 117
- 152
SHIRIKA LA CHAKULA DUNIANI (FAO) LILIONYA SERIKALI KUCHUKUA TAHADHARI KUHUSU NJAA.JPM HAKUISOMA.
Mhe Rais ni vema akajua kwamba kwa namna anavowasimamia walio chini yake upo uwezekano mkubwa wa kupotoshwa na wasaidizi wake kuhusu ukweli na ukubwa wa tatizo la njaa kwa hofu ya kutumbuliwa.
Ndio mana hata Mamlaka ya Hifadhi ya Chakula nchini inampotosha ilhali taarifa za kiuchimi zipo wazi kwenye tovuti ya Bank Kuu.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Tathimini ya Uchumi ya Mwezi Oktoba ilotolewa Novemba 2016, (Monthly Economic Review ), inaonesha kwamba akiba ya chakula nchini sana. Inaonesha Mwezi Oktoba 2016, akiba ilikuwa 90476tonnes, wakati Oktoba miaka mingine hali ya chakula ilikuwa;
2015- 253656tonnes
2014- 426999tonnes
2013-235817tonnes.
Hii ni taarifa ya BOT, na ndio latest. kwenye tovuti ya BOT. kama wataalamu wake hawasomi hilo ni tatizo.
Hali ya njaa ilishatabiriwa na Shirika la Chakula duniani(FAO) , tangu July28,2016 kwamba ukanda wa kusini mwa Africa utakabiliwa na njaa kuanzia mwisho wa Disemba mpaka March 2017 na huenda hali ikaendelea mpaka kati kati ya 2018 kama hatua hazitachukuliwa kusaidia wakulima wadogo hasa kwa kuwapatia pembejeo mapema na wapande mapema mvua za Oktoba 2016.Na kwamba hatua zisipochukuliwa kuna uwezakano wa watu zaidi ya milioni 23 kukosa kabisa chakula. hizi ni taarifa zipo kwenye tovuti ya Shirika hilo la Chakula Duaniani.
Nchi zilizotajwa hapo ni pamoja na Tanzania, Malawi, Mozambique,Namibia, Swatzland, Lessotho, Zambia, Zimbabwe.
Wakati taarifa hii ya Shirika la Chakula duniani likitoa tahadhiri hii, na kutaka nchi husika kusaidia wakulima mbolea na dawa na kwamba walime kwa wakati mvua za mwezi wa kumi, Tanzania kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, ruzuku ya mbolea ilishushwa kutoka 78bn za mwaka 2015/16 mpaka ruzuku ya 10bn kwa mwaka 2016/17. Hii inaashiria Serikali haikujua kinachoendelea kwenye kilimo na hali ya chakula dunani.
Aidha Shirika hili laFAO limeshatoa taarifa kuhusu njaa kali pembe ya Afrika ambapo Kenya ni moja ya wahanga, Ni kwasababu hiyo kiasi kikubwa cha chakula Tanzania kimeuzwa huko na kuzidisha makali ya njaa nchini.
Taarifa zote hizi za BOT, FAO kuhusu baa la njaa pembe ya Africa na Uhaba wa chakula kusini mwa Africa ni taarifa tosha na za mapema kwa serikali kujiandaa lakin cha kushangaza ndio hivi ruzuku ya mbolea inashuka kutoka 78bn mpaka 10bn na akiba ya chakula inakuwa pungu ya ile ya mwaka jana kwa zaidi ya asilimia 200%