Ally Kanah
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 1,479
- 388
MGOGORO WA CHADEMA ...nawasihi vijana na Ndugu zangu watanzania tusiujadili kwa udini na ukabila. Tutajenga msingi mbaya kwa taifa letu zuri. Tukubaliane kwamba hakuna dini wala Kabila lililohusika na mgogoro huu isipokuwa mapungufu ya viongozi husika katika mgogoro wenyewe. Tusimjadili Mbowe, Slaa au Zitto na Kitila kwa misingi ya uchagga au ukristo au uislamu. Tujadili hoja. Hakuna ukristo wala uislamu au uchagga unaohusika hapa. Kinachohusika hapa ni mapungufu ya wahusika tu. hoja zilizopo zinatosha kujadili hili jambo bila kuingiza uchagga au ukaskazini wa Mbowe, tunaweza kuendelea kujadili bila kuingiza ukigoma au uha wa zitto. Tunaweza kujadili bila kuingiza ukristo wa Mbowe na slaa au uislamu wa zitto. Tujadili hoja tu. Tusiwape watu hadhi za udini na ukabila wasizokuwa nazo