Kafulila awafungua macho vijana juu ya mgogoro wa chadema

MGOGORO WA CHADEMA ...nawasihi vijana na Ndugu zangu watanzania tusiujadili kwa udini na ukabila. Tutajenga msingi mbaya kwa taifa letu zuri. Tukubaliane kwamba hakuna dini wala Kabila lililohusika na mgogoro huu isipokuwa mapungufu ya viongozi husika katika mgogoro wenyewe. Tusimjadili Mbowe, Slaa au Zitto na Kitila kwa misingi ya uchagga au ukristo au uislamu. Tujadili hoja. Hakuna ukristo wala uislamu au uchagga unaohusika hapa. Kinachohusika hapa ni mapungufu ya wahusika tu. hoja zilizopo zinatosha kujadili hili jambo bila kuingiza uchagga au ukaskazini wa Mbowe, tunaweza kuendelea kujadili bila kuingiza ukigoma au uha wa zitto. Tunaweza kujadili bila kuingiza ukristo wa Mbowe na slaa au uislamu wa zitto. Tujadili hoja tu. Tusiwape watu hadhi za udini na ukabila wasizokuwa nazo

Asante sana Kafulila kwa neno lako hili angalau umefunguka na kuona ukweli .Msaidie Zitto kwa kumpa ushauri ajirudi aende akaseme na wenzake .
 
Hakuna askuwa na dini wala kabila hapo, na hapo nakushauri tu, ungelitumia maneno ya akiba kama kusema hivi : - tujaribuni kujadili mambo ya zitto, dr.kitila, mbowe na slaa bila kutumia dini zao, au ukanda wao ama ukabila wao,

Swali ;
katika uchangiaji waliochangia wengi humu, wengi wamegusia hayo uliyoyasema au
umetumia hisia tu kushauri..?

(a)-Kama jibu ni ndiyo wamegusia, kwa mtazamo wadhani/waamini nini sababu au chanzo?
(b)-Kama jibu ni hisia zako, kwanini uhisi hivyo?
 
wataweza wapi hawa vijana wanachukia wachaga tangu wanakuwa..baba zao wameshindwa waambia kwanini wamakuwa losers,wakati wachaga wanakuwa winners..wataweza wapi wakati kila siku ktk maisha yao wapinga kristu nao hawajui njia nyingine ya kusema kwanini wakristu wamefanikiwa Tanzania ukilinganisha na waislam..ambao hela zipo ktk mikono yao,madaraka yapo ktk mikono yao bado wamechoka na wanaangakuka km Akina Kapuya.Wanaishia lalamika kuwa wamefanyiwa dhulmat.

Watasema nini wakati pamoja na kil akitu hawa watoto wanachopata,kuanzia upendeleo ktk kazi ,elimu ,ajira etc bado wanazidi poteza walicho nacho?
 
Back
Top Bottom