Kafulila asipoacha tamaa na papara atafuliakila aendako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila asipoacha tamaa na papara atafuliakila aendako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpayukaji, Dec 18, 2011.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]

  [​IMG]
  Ingawa kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini NCCR-Mageuzi, David Kafulila si haki, kulitarajiwa kutokana na tabia ya mhusika. Kafulila alipoingia kwenye siasa za upinzani alijiwekea malengo makubwa kupita uwezo wake. Kwa wanaokumbuka kilichomtoa CHADEMA, watakubaliana nasi kuwa Kafulila hajatulia.

  Bahati mbaya sana kwa Kafulila, anataka kufikia malengo yake kwa njia ya mkato ambayo ni kuanzisha vurugu zisizo na sababu kwenye vyama. Wapo wanaomuona kama mganga njaa na mtu mwenye tamaa. Wengine wanamuona kama Uvuruge wa kawaida wakati wengine wakimshuku kuwa pandikizi la CCM. Yote yawezekana. Je Kafulila atarejea CHADEMA? Je CHADEMA, kwa alivyowachafua, watakuwa dhalili kiasi hiki kumpokea? Je Kafulila yuko tayari kuramba matapishi yake ili angalau apate nyenzo ya kurejea kwenye ulaji? Je Kafulila ni mwanasiasa makini au mleta fujo na mtafuta riziki kwa mgongo wa kisiasa? Je Kafulila atarejesha kiti chake? Je atakwenda CCM?

  Kimsingi, pamoja na Kafulila kufukuzwa na mtu mchafu kuliko yeye yaani James Mbatia ambaye anasemekana kuwa pandikizi na kuwadi wa CCM, anapaswa kujiulaumu kwa kutaka kuukata mkono uliokuwa ukimlisha yaani chama. Na hapa ndipo anapoteza umakini na upambanaji aliokuwa akivishwa wakati si mpambanaji kitu. Kama kweli alilia asamehewe na Mbatia tena mbele za watu, basi hana lolote zaidi ya kubangaiza. Kama alikuwa akiamini alichokuwa akisimamia na kupigania, hakupaswa kulialia kama kichanga. Hata hivyo, kutimuliwa kwa Kafulila kuna somo kuwa CHADEMA ni chama makini. Kwani wao hawakumtimua zaidi ya kumvua uongozi kwa faida yake na chama. Bahati mbaya Kafulila hili hakulipata akaamua kufunga virago kumkimbia mjusi na kumkumbatia mamba. Ama kweli wahenga walinena kuwa ngoma ya watoto haikeshi.

  Kafulila anapaswa akae ajifue na atulie kama kweli ana ajenda ya maana na yenye mashiko katika siasa zaidi ya kutafuta uheshimiwa ili kuhomola. Wenye akili tieni akilini siasa si lelemama wala nyenzo rahisi ya kutafutia neema miongoni mwa mafisi na mapapa kama ilivyotokea kwa Kafulila. Yetu macho kuona nini kitafuata.
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana mdogo ameshindwa kuelewa kuwa hauwezi fika 3 kabla ya 1 na 2.

  Tatizo ni la mkoa anaotoka. Ni wapenda sifa. Washamba sana, watu wakujikweza.
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280

  huwa hamueleweki! mara mnataka watu wakeli, mara anapenda sifa, mara ana malengo makubwa! ili mradi umepost!

  ninachojua ni kuwa vyama vya siasa vina makundi fulani...akitokea intruder lazima atawajibishwa..........badala ya kushabikia ujasiri wa dogo unamponda...what NCCR does for betterment of this nation what is the significance of mbatia?? unataka akae mpaka lini?

  ndiyo nyie mnawaza ukombozi wa nchi hii utaletwa na CDM, wakati kila reserach inaonyesha si leo wala kesho CDM kusihika nchi...lazima kuwe na vyama vingi strong! mbatia anatuchelewesha sana, bahati mbaya kuna watu wenye mawazo kama yako ambayo huwa negative kwenye situation kama hii,.....ila positive jkwa chadema tu!

  leo akitokea mtu chadema aulize mapato na matumizi atatimuliwa....muulze hamad cuf!

  nyie wenzetu mnaojua kila kitu mnawafanya wengine waishi vizuri huku wakichekea akili zenu!!!

  viva kafulila viva...ukweli tu...mbatia ni kibaraka wa CCM haihitaji kuwa na uroho au uruhu kulisema hili

  you are man...a hero to be specific
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  umevamia mawazo feki ya mpayukaji...amekufisadi na umeropoka mpaka visivyotakiwa kuropokwa!!!

  tatizo ni mkoa aliotoka.......siyo kafulila sasa! what a shame...nashindwa nianze kudadavua hoja hii kuanzia wapi!

  kwa kifupi hakuna mtanzania mwenye asili ya pale anapoishi! history 101!
   
 5. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa kweli kaacha kukumbatia mjusi kamkumbatia mamba sasa ameona mchezo mchafu wa mamba ajiandae kuliachia hilo jimbo maskini ndo hapati tena posho. Nitarudi baadae kidogo
   
 6. M

  Milindi JF-Expert Member

  #6
  Dec 19, 2011
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,212
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180

  Tatizo sio mkoa anaotoka pamoja kwamba mkoa unachangia kwani ni ajabu Moses Machali kuwa mbele kuhakikisha kafulila anaondoka ni aibu kwa mkoa wa kigoma wabunge wa chama kimoja kutopendana ni aibu kwa nccr mageuzi;

  Tatizo ni kuwa mkweli sana ktk siasa, lazima upate cha mtema kuni;
  Pole devi!!!
   
 7. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tena mamba aliye toka kuhatamia mayai yake.
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,654
  Trophy Points: 280
  Ujasiri wa KULIA?
  Hahahh Mwanaume Haliii!!!!!!!!
  Amekuwa kama PINDA
   
Loading...