Kafulila amehukumiwa kwa kutoa siri zipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila amehukumiwa kwa kutoa siri zipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by February, Dec 22, 2011.

 1. February

  February Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa muda sasa tangu uanze mjadala wa kutoa siri za chama kwenye vyombo vya habari nimekuwa nikijiuliza ni siri gani ambazo kijana anahukimiwa kuzitoa? Kabla ya hukumu siku chache kwenye magazeti palikuwa na malumbano ya tofauti za mawazo kwamba kafulila anapinga mbatia kuendelea na kesi ya kawe, kafulila anapinga chama chake kwenda ikulu kufuatia azimio la kamati kuu ya ccm na mengine mengi kuhusu wa chama hicho kuwa na sura ya upinzani. Hii ndio kumbukumbu yangu. Sasa labda nikumbushwe ni neno gani iliyokuwa siri ya nccr ambayo huyu kijana katoa? Mana kama ameshatoa sio siri tena hivyo ni muhimu tuambiwe hicho kinachoitwa siri. Isiwe kama mambo ya serikali yetu kuficha ufisadi kwa kivuli cha siri za serikali. Mana kama mambo yenyewe ni hayo ya kawe na tabia za mbatia kuwa kibaraka wa ccm sidhani kama ni siri mana hapa jf karibu wote tunajua tabia ya mbatia. Tuambiwe kwanza hizo siri ni zipi kuliko kulishwa sumu tu. Simtetei huyu kijana lakini hofu yangu ni kumuhukumu kwa kitu tusichokijua hasa tukizingatia tabia ya mbatia. Mana hazijapita siku bada ya kumfukuza kafulila nccr wametangaza kuitikia azimio la cc ya ccm kwenda ikulu. Tutafakari
   
Loading...