Kafulila alipomkosoa Wangwe kuhusu 'Nidhamu na demokrasia' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila alipomkosoa Wangwe kuhusu 'Nidhamu na demokrasia'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Nov 18, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WANGWE: DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO

  Na David Kafulila:
  Nimekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuzungumzia kinachoitwa mgogoro ndani ya CHADEMA. Ni wazi kwamba kwa wanaonifahamu hali hii itakuwa imewashangaza. Wapo wanaoweza kusema bila shaka ni kwasababu kinachoitwa mgogoro wenyewe unakihusu chama ninachoshiriki kukijenga nikifikiri na kuendelea kuamini kuwa kinayo fursa ya kusukuma mabadiliko makubwa ya kisiasa na utawala wa nchi yetu kama tunavyoendelea kuona.

  Lakini ukweli wa kimya changu ulitokana na fikra kuwa, kwakuwa misingi ya hoja iliyobainishwa na Mh Chacha Wangwe haikuwa na ukweli wa mantiki na nyakati. Nakwamba kilichokuwa kikijengwa na Chacha zilikuwa ni hisia za ujinga wa ubaguzi, basi sikudhani kama hisia hizo zingeweza kutaka kusimama akilini mwa watu wanaoishi katika nchi inayokabiliwa na changamoto nyingi za msingi ambazo kwa ujumla wake zinaelezea umasikini wa jamii hii.

  Nikiri kwamba kwasababu binadamu tumeumbwa kwa kusahau. Nilisahau kuwa uongo unoporejewa mara kwa mara hugeuka ukweli wa watu.Nilisahau kuwa siasa zinajengwa kwa mitazamo, na hisia(za uongo au kweli) ni moja ya vichocheo vya mitazamo.

  Kuna nadharia nyingi kuzungumzia kadhia hii; mwelekeo, historia, na kinachoendelea ndani ya CHADEMA sanjari na mikanganyiko ya kisiasa inayoendelea nchini hasa baada ya CCM kupoteza mwelekeo na matumaini kwa watanzania baada ya kushindwa vita dhidi ya ufisadi.

  Wengine wanaweza kushangaa kwanini nimesema "kinachoitwa" mgogoro. Hii inatokana na ukweli kuwa wapo wanaoamini kuwa mgogoro kwa chama cha siasa ni tofauti za kisiasa baina ya kambi mbili zinazohitirafiana, ambazo kimsingi zinakuwa zinakaribiana kwa ushawishi ndani ya chama kama ilivyokuwa kwa NCCR mageuzi, ambapo kambi mbili zenye nguvu na ushawishi mkubwa katika siasa za ndani na nje ya chama, ya Mabere Marando ilitofautiana na kambi ya Lyatonga Mrema.

  Mtazamo huo unajenga hoja kuwa kwa mazingira ya CHADEMA pengine mgogoro wa msingi ungejitokeza kama magwiji wa siasa za CHADEMA kama Freeman Mbowe, Dk Willibrod Slaa na Kabwe Zitto wangekuwa wamehitirafiana katika masuala ya msingi kuhusu uendeshaji wa siasa na chama. Hii inatokana na ukweli kuwa hawa ni viongozi ambao angalau unaweza kujua wanasimamia nini kwa mwelekeo wa Taifa hili kwa sasa na huko tuendako.Na heshima zao zimejengeka katika misingi hiyo.

  Hali ya sasa ambapo kinachoitwa mgogoro kinabainisha kambi mbili. Ya Mh Chacha Wangwe peke yake dhidi ya ile ya Freeman Mbowe, Dk Willibrod Slaa na Kabwe Zitto inajenga mashaka kwa wachambuzi wa mambo wa siasa hasa tukijua wazi kuwa Mh Chacha pengine kwa bahati mbaya hajapata fursa ya kubainisha maono yake kama kiongozi wa kitaifa(stateman). Siwezai kumlaumu katika hili, natambua mchango wake na ninaelewa kuwa kila kitu ni mchakato,na mchakato ni suala la muda.

  Nimelazimika kusema hayo kwanza ili kubainisha taswira ya kinachoitwa mgogoro kabla ya kuchambua hoja za msingi zinazobainishwa katika hisia hizo za mgogoro. Najua zinaweza kuwa hisia na maoni ya watu tu, lakini umuhimu wake unatokana na ukweli kuwa siasa zinajengwa na mitazamo, najua wanasiasa wengi wasio na sifa wametumia hisia na hata hofu za uongo kuangusha na kuingiza tawala nyingi madarakani tawala nyingi duniani.

  Kuna mambo manne ningependa kujadili kabla ya mwisho wa makala yangu kuhusiana na kadhia. Kwanza ni hoja ya matumizi ya ruzuku, Ukabila, Udikteta na maamuzi ya Kamati Kuu kuhusu kusimamishwa kwa Makamu Mwenyekiti Chacha Wangwe.

  Chacha ni rafiki yangu. Ni kiongozi wangu wa mkoa. Najua kuwa Chacha anapenda demokrasia na uhuru kuliko kitu chochote katika siasa. Hili ni jambo jema. Lakini tatizo lake ni kukosa uongozi wa pamoja ambao chimbuko lake ni nidhamu.

  Ni muhimu wanaomshauri Chacha Wangwe wakampa somo kuwa kazi ya kujenga uongozi mmoja katika chama ni kutekeleza kwa dhati kanuni ya demokrasia na nidhamu ndani ya chama.Chama chetu lazima kiendeshwe kwa misingi ya kidemokrasia kila ngazi.Wajumbe wa vikao lazima wawe huru na sawa katika kuyajadili masuala. Uhuru huu uheshimu maoni ya wachache lakini usiathiri kanuni ya wengi wape maana lazima mjadala ufike mwisho na uamuzi kufanywa.

  Nadharia ya nidhamu ndani ya chama inatokana na ukweli kuwa chama ni chombo cha kutenda, na kutenda kama kitu kimoja.Nakwamba nidhamu ni pamoja na kuwajibika kwa maamuzi ya kikao kinachokuhusu. Uamuzi wa Chacha kukaidi na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ambayo yeye(Chacha ) ni mjumbe ni kielelezo cha namna asivyo muumini wa kweli wa demokrasia.

  Ni ukweli kuwa nidhamu bila demokrasia ni udikteta. Lakini ni ukweli pia kuwa demokrasia bila nidhamu ni fujo.Kanuni ya demokrasia na nidhamu ndiyo inayokiwezesha CHADEMA kuwa chama cha kidemokrasia na papo hapo kuwa kuwa taasisi ya kusimamia mageuzi ya kisiasa nchini kutokana na nidhamu inayokipa uongozi na msimamo mmoja katika vitendo.

  Wanaojua vizuri historia ya CHADEMA wanakiri kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanywa kuitaasisi CHADEMA chini ya Freeman Mbowe na ndio sababu Chama kinafanikiwa katika malengo mengi sasa. Huko nyuma malengo mengi ya chama hayakuweza kutekelezwa moja ya sababu ikiwa ni udhaifu wa baadhi ya viongozi kuhusiana na nidhamu, demokrasia wanaitaka lakini palikuwa na kulegalega kuhusu nidhamu.

  Imekwishajadiliwa na kupitishwa kwenye Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuwa Chama kiendelee kutumia helkopta kwenye oparesheni maalumu ya kisiasa kama kampeni. Uamuzi huu ulifikiwa baada ya majadiliano ndani ya vikao hivyo ambavyo vyote Chacha ni mjumbe. Lakini baada ya vikao anakutana na waandishi wa habari na kudai kuwa yeye anapinga matumzi ya helkopta na mbaya zaidi anasema hayo ni matumizi mabaya ya ruzuku.Anasahau kuwa yeye alipokuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti aliwajibika kusimamia maazimio ya vikao vya chama na kwamba anapopingana na maazimio ya vikao ni sawa na kuomba kujiuzulu!

  Agosti13,2006 wakati wa uzinduzi wa Chama na Mkutano Mkuu, Mh Mbowe alisisitiza sana umuhimu wa viongozi wote kuhakikisha wanasimamia majukumu ya chama tunayojiwekea ili kufikia malengo yale.lakini ni wazi kuwa bila kusimamia kanuni ya nidhamu na demokrasia, tamko hilo haliwezi kutekelezwa katika ngazi yoyote. Ndio maana ilikuwa muhimu sana kumsimamisha Chacha ili kujipa nafasi ya kutekeleza malengo ya chama ambayo kimsingi yanatafsiri nafuu ya maisha kwa watanzania wengi.

  Kwa mfano, Mh Chacha anazungumza hadharani kuwa ruzuku ya chama haiendi mikoani. Lakini anasahau kuwa Kamati Kuu ilisha agiza kuwa kila mkoa ufungue akaunti utumiwe sh 100,000/=(laki moja kwa mwezi). Je Chacha anaweza kutoa mfano wa mkoa uliokwisha fungua akaunti na haujatumiwa pesa hiyo?..Sio hayo, kila wilaya yenye diwani na zile za makao makuu ya mkoa ziilikwishaagizwa kufungua akaunti ili zitumiwe sh 200,000/= kwa mwezi tangu mwaka 2007.

  Na ikumbukwe kuwa CHADEMA kinapata ruzuku ya kiasi cha takribani milioni60 kwa mwezi,dhidi ya CCM inayopata ruzuku ya bilioni1.2 kwa mwezi(takribani mara20 ya ile ya CHADEMA). Ruzuku ya CCM kwa mwezi ni takribani sawa na jumla ya ruzuku ya CHADEMA kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu.

  Zaidi ya fedha hizo kutumwa, Chama kinatengeneza vifaa vya uenezi kama vitabu, bendera,nk na kusambaza wilayani bure ili kuhakikisha chama kinafanya kazi. Viongozi wa taifa wanafanya ziara mikoani mara kwa mara.Kwa mfano, kwa miezi miwili tangu mei2008, Viongozi wamefanya ziara mikoa mbalimbali. Zitto Kabwe amefanya ziara ya Chama Tanga kwa siku nne, na Kigoma kwa wiki mbili. Ilhali Dk Slaa emefanya ziara Singida na Manyara., Ni bahati mbaya kwamba wakati wengine wanaendelea kujenga chama wengine wanahaha huku na kule kutafuta jinsi ya kubomoa badala ya kwenda bungeni au mikoni kufanya kazi.

  Wakati Mh Chacha Wangwe anasema CHADEMA imeshindwa kufanya kazi Dar es Salaam , anasahau kuwa mpaka sasa kuna timu ya kuhamasisha chama mkoa wa Dar es Salaam , na wanatumia fedha za chama. Wamefungua matawi Temeke na sasa wanaendelea Kigamboni. Mh Chacha anafahamu hilo kwasababu imeripotiwa kwenye Kamati Kuu ambayo yeye ni mjumbe. tayari zaidi ya matawi ishirini yamefunguliwa Temeke, Kinondoni na yanaendelea kufunguliwa Kigamboni kwa fedha hiyo ya ruzuku na msaada wa makao makuu. Si katai Mh Chacha kutaka uenyekiti, lakini muhimu ni awe mkweli. Aseme mambo ya hakika kwasababu CHADEMA imejijengea heshima ya kuwa na viongozi wanaozungumza hoja kwa vielelezo. Hali sasa ambapo anajikuta anazungumza mambo yasiyo na hakika alimradi kuusaka uenyekiti sio ustaarabu na ni hatari kwa demokrasia nchini. Ni vema akabainisha sifa zinazomfanya afae kuwa Mwenyekiti badala ya kutafuta kuungwa mkono kwa kubomoa chama kwani inamvunjia heshima.

  Ni ukweli usiopingika kuwa kama chama, CHADEMA kinakabiliwa na Changamoto nyingi za kujijenga yenyewe na wakati huo huo kuthibiti mwelekeo wa Taifa kikiwa na wabunge 11 na madiwani 100 nchi nzima. Na sababu hiyo inayopelekea kulega kwa nyakati Fulani katika maeneo Fulani. Lakini ukweli huo hauwezi kuondoa ukweli mwingine kuwa kuna hatua kubwa imepigwa katika kufikia mpango mkakati wa chama 2005-2010 hasa katika eneo la kuiondolea serikali uhalali wa kisiasa kwa kusimamia vema kwenye vyombo vya maamuzi kama bunge.

  Ni ukweli pia kuwa kumekuwepo na Changamoto ya kutuma ruzuku mikoani katika nyakati Fulani kutokana na mwenendo wa siasa za wakati huo.Huo ndio ukweli unaojulikana kwa Kamati kuu, Baraza Kuu ambapo kote Mh Chacha ni mjumbe mwenye haki na uhuru wa kuhoji na kushawishi maazimio, misimamo na mwelekeo. Kwa mfano, isingetarajiwa kuwa chama kipeleke ruzuku mikoani wakati wa uchaguzi wa Kiteto ambao ulikuwa ukihitaji zaidi ya sh milioni40 kati ya 60 za ruzuku.

  Jambo moja ni kweli kwamba sasa CHADEMA inakubalika kila kona ya nchi. Kazi iliyofanywa na CHADEMA tangu sakata la Buzwagi likiongozwa na Kabwe Zitto, likifuatiwa na hili vita dhidi ya Ufisadi chini ya Dk Slaa mpaka leo sambamba na utendaji mahiri wa wabunge wa CHADEMA vimekuwa sababu kubwa ya mahitaji hayo. Changamoto pekee ni namna kufikia watanzania wote, tena mara kwa mara ili waone kuwa CHADEMA kipo pamoja nao. Naam! Changamoto ni nyingi lakini muhimu ni kwamba CHADEMA kipo kwenye mstari sahihi.

  Mwandishi wa makala hii ni Afisa Habari wa CHADEMA. Lakini haya ni maoni yake binafsi kama mwanachama.

  Itaendelea wiki ijayo kwa kujadili hoja za ukabila ndani ya CHADEMA.
   
 2. t

  tk JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Mchimba kisima huingia mwenyewe"
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  Hii inaonyesha amekosa hekima kama yeye mwenyewe ameshindwa kufanya aliyoyasema
   
 4. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  haya ndo matatizo ya kuwa opportunist.

  Kufulila anapaswa kujua kuwa Hayati Chacha alikuwa na cheo cha kisiasa siyo Afisa kama yeye. Nafasi ya Afisa ni ya kitendaji zaidi, hivyo nidhamu na umakini wa Afisa unapaswa kuwa mkubwa kuliko mwanasiasa. Pia nafasi ya Afisa inaweza kutenguliwa kirahisi na kupewa mwingine kuliko cheo cha kisiasa kama ilivyokuwa Wangwe.

  Hivi ktk chadema wale Maafisa vyeo vyao ni vya kudumu? yaani asiye afisa aliye tu hata weza pata nafasi hiyo hata kama anauwezo au atapata pale tu jamaa atakapoasi na kuhama chama?

  Hivi viongozi wa chama na maafisa wa chama hawana kazi nyingine na wakiondolewa kwenye nyadhifa hizo wanashindwa kuishi? Tz bwana.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na mchimba kaburi je?...........
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  wangapi wako kama huyu? hii ni symbol tunao wengi wanaohubiri wasiyoyatenda,

  Mlimkosea wangwe na hii dhambi itawatafuna sana,

  yetu macho
   
 7. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Akiulizwa kuhusu hili, jibu litakuwa " NO COMENT"
   
 8. B

  Boca1 Member

  #8
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kafulila kafuria
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mimi simlaumu kafulila hata kidogo, nimetafakari sana nimegundua kuna mtego mkubwa unawekwa na Vyombo vya Habari visivyo na lengo zuri na CHADEMA na Kafulila ameingizwa katika Mkenge huo kirahisi sana, amelishwa maneno ya chuki dhidi ya Viongozi wenzake naye akayatapika hadharani. Vijana CHADEMA wasipokuwa makini wengi wataingia katika mkenge huu! Sasa mtanzania na majira wameshamalizana naye tungojee Mwingine
   
 10. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wee!!!!!!!!!!!!!

  Maneno gani tena haya jamani?
   
 11. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Two Down, Two to Go.

  Chama aanzishe Mbowe na familia yake, halafu baada ya chama kunenepa, umaarufu mnataka mchukue nyie kisa demokrasia? Mtakiona cha moto sasa Mbowe na Mzee Mtei wameamua kukirudisha chama kwa wenyewe.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu hajafulia, nadhani angekaa chini akatafakari angegundua ni wapi alipokosea naamini ana future nzuri katika Siasa
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaa, Wenye Chama ni wananchi bana LoL!
   
 14. t

  tk JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wenyewe ni akina nani hao?
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wewe na Kafulila mnaamini vitu viwili tofauti kabisa, sasa sijui wewe na yeye nani mkweli, Mmeponza sasa mmekaa Pembeni mkimcheka LoL!
   
 16. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndege take 5
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kina nani hao unaowaongelea? Wanafiki bwana utawajua tu kwa matendo na maandishi yao. Ukiwauliza Wangwe alikosewa nini na/au kina nani, anabaki katoa macho na kuanza kunyoosha vidole kwa wachagga (kabla ya kutoa hadithi ndefu kuwa amesomea na kuoa uchaggani).
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha... says who?

  Umeishia wapi kwenye kufanya interview na Mbowe?
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Mkuu Nimesoma Gazeti la Mwanahalisi wakimhoji Mama Zitto, kama maneno yake yatakuwa yana ukweli basi ndicho kilichompelekea Kafulila Kujivua Uanachama. Sasa kijana inawezekana amegundua Jaribio lake la Kugombanisha Zitto na Uongozi limeshindikana sasa atafanya nini zaidi ya Kujitoa, sometimes mambo ya kitoto yanaponza sana, nilishawahi kusema kwamba watu wanaleta siasa za DARUSO kwenye vyama ni mbaya saba
   
 20. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hana ubavu wa kumaproach kiongozi yeyote wa CHADEMA
   
Loading...