Kafulila akamatwa 'uchawi' NCCR-Mageuzi; MBUNGE wa Kasulu M.Machali yuko tayari kujiuzulu

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

na Betty Kangonga

MBUNGE wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), amesema kuwa yuko tayari kujiuzulu nafasi ya ubunge na uanachama iwapo mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, atafanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Mbali na kutoa kauli hiyo, Machali alisema Kafulila alidhihirisha kuwa ni mtu mwenye wivu pale alipohoji sababu ya mbunge wa Hai na kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA), kupewa nafasi za kuuliza na kuchangia bungeni mara nyingi akiwa kama nani.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano jana kwa njia ya simu, Machali alisema kuwa iwapo Kafulila akifanikiwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho atalazimika kujivua wadhifa wake wa ubunge kwa kuwa kiongozi huyo hana uwezo bali ni bingwa wa kuanzisha migogoro.

"Kamwe siwezi kuwa mbunge chini ya uongozi wa Kafulila ambaye anataka nafasi hiyo kwa muda sasa kutokana na kumshikia kigogo mmoja na hakika nina ushahidi wa hilo na wakati ukifika nitamtaja ila kwa sasa siwezi kufanya hivyo kwa vile nimemrekodi...pia amedhamiria kupambana na mwenyekiti wetu hadi mwisho," alisema.

Alisisitiza kuwa Kafulila hawezi kupata kura za uenyekiti kutokana na kukosa uadilifu na kuwa chanzo cha migogoro kila kukicha na ni mtu anayependa chokochoko.

Alisema kuwa Kafulila iwapo anataka uenyekiti hapaswi kuanzisha migogoro bali anachotakiwa kufuata ni kanuni na sheria zilizowekwa na chama hicho ili aweze kufanikiwa.

Mbunge huyo, alisema kuwa Kafulila ana ajenda ya kutaka kuua upinzani usifanikiwe nchini jambo ambalo linaonyesha kuwa halitaathiri chama hicho pekee bali linaweza kuathiri hadi vyama vingine kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Machali alisema kuwa kutokana na tabia yake hiyo umma unapaswa kufahamu umuhimu wa kauli iliyowahi kutolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa kwa kuamua kumuita Kafulila sisimiza kwa ile tafsiri ya kutokuwa na uwezo wa kufikiri sawasawa.

"Kafulila alishanifuata kwa nyakati tofauti akiniomba nishirikiane naye katika harakati zake za kutaka kupata uenyekiti ndani ya chama chetu lakini nilimpuuza kwa kuwa namfahamu ni mtu wa migogoro," alisema.

Kama Kafulila akifanikiwa NCCR Mageuzi kitakuwa Chama cha Vijana

Na Vijana wengi hawana kazi na Maisha yao sio Mazuri
 
Hiv nimakosa kafulila kugomba??
Kwa nini mbatia asiruhusu uchaguzi??
Kama wajumbe hawamtaki kafulila si waamue kwenye uchaguzi??
 
tunamjua kitambo ni kibaraka wa ccm huyo hana tofauti na mrema tena naonaga wanakaa karibu bungeni nahisi mzee anamfundisha strategy za kuua chama
 
Hiv nimakosa kafulila kugomba??
Kwa nini mbatia asiruhusu uchaguzi??
Kama wajumbe hawamtaki kafulila si waamue kwenye uchaguzi??

Demokrasia tanzania hii na njaa zetu ni kazi kweli kweli,na yeye huyo Machali anatumwa na nani?
 
Kafulila anaonekana tu hata kwa nje...lakini hawa watu wa Kg vipi?mbona wako kipopo popo sana wana tatizo gani kisaikolojia ama kibaiolojia?

Nina mfano hai kwa washikaji wangu kusema kweli wanapenda sana heshima na vyeo (recorginition) hata kama uwezo hana,nabaki najiuliza na naendelea kuamini hawa wenzetu wana tamaa sana
 
Machali ni mamluki toka CHADEMA, anajifanya mwana NCCR Mageuzi lakini anafanya kazi kwa maslahi ya CHADEMA. Ametumwa kukisambaratisha chama cha NCCR Mageuzi kisha ahamie CHADEMA. Angekuwa mwanachama safi wa NCCR mageuzi asingetoa siri za chama kwa CHADEMA kupitia gazeti lake Tanzania daima. Badala yake angetumia muda wake wote kutafuta suluhu ya migogoro badala ya kuchonganisha watu.
 
acha asema ukweli unafiki utatuua na umasikini eti kisa siri za chama hayo ndyo yameifikisha ccm hapa
 
Kafulila anaonekana tu hata kwa nje...lakini hawa watu wa Kg vipi?mbona wako kipopo popo sana wana tatizo gani kisaikolojia ama kibaiolojia?

Nina mfano hai kwa washikaji wangu kusema kweli wanapenda sana heshima na vyeo (recorginition) hata kama uwezo hana,nabaki najiuliza na naendelea kuamini hawa wenzetu wana tamaa sana
Hapa umenena mfano mzuri ni Walid Kaborou, Nzwansungwanko Daniel....
 
Machali ni mamluki toka CHADEMA, anajifanya mwana NCCR Mageuzi lakini anafanya kazi kwa maslahi ya CHADEMA. Ametumwa kukisambaratisha chama cha NCCR Mageuzi kisha ahamie CHADEMA. Angekuwa mwanachama safi wa NCCR mageuzi asingetoa siri za chama kwa CHADEMA kupitia gazeti lake Tanzania daima. Badala yake angetumia muda wake wote kutafuta suluhu ya migogoro badala ya kuchonganisha watu.

inaumaa eeh, mbona huwa mnafurahia mnaposikia News za CCM, hebu kua mtu mzima na mwenye tabia za kiume
 
Machali ni mamluki toka CHADEMA, anajifanya mwana NCCR Mageuzi lakini anafanya kazi kwa maslahi ya CHADEMA. Ametumwa kukisambaratisha chama cha NCCR Mageuzi kisha ahamie CHADEMA. Angekuwa mwanachama safi wa NCCR mageuzi asingetoa siri za chama kwa CHADEMA kupitia gazeti lake Tanzania daima. Badala yake angetumia muda wake wote kutafuta suluhu ya migogoro badala ya kuchonganisha watu.[/QU point of correction TANZANIA DAIMA sio gazeti la CHADEMA
 
Kuna bundi mkubwa ndani ya NCCR.

'Chatumkali, njoo utusaidie kummeza huyu bundi' - Hii natania.
Ila ndugu yangu, wala huyu si bundi, ni hali ya kawaida kabisa katika siasa, ambapo wanasiasa hushindana kupata mamlaka ya utawala. katika kushindana kwao hutumia mbinu safi au chafu, husema ukweli na uongo, huzua mambo ama hutumia udhaifu wa washindani wao. Katika Tanzania, tunaye mwanasiasa asiye na tabia hii?
 
Yawezekana Machali yupo sawa lakini mbona kama anavutia upande wa CHADEMA sana. Migogoro ndani ya NCCR inahusishwaje na CHADEMA? Hapo napata uwalakini na naelekea kukubaliana na mjumbe aliesema huyu Machali ni kibaraka wa CDM aliye ndani ya NCCR.
 
Mbati is not straight ni Homo,NCCR haipaswi kuongozwa na gay.

Ndugu Kabembe,
Nakushauri ujitahidi kujua chanzo, ukweli na/au uongo wa hii kashfa kwa huyu kiongozi. Hofu yangu usije kuichafua nafsi na roho yako kwa kushiriki dhambi isiyo ya kwako.
Tunahimizama humu ndani kuwa great thinkers, miongoni mwa sifa za great thinkers ni uadilifu katika mawazo, kauli, na matendo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom