KAFULILA AIBUKA KISIASA SASA KUELEKEA MAHAKAMA YA RUFAA.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,473
33,426
Kafulila.jpg

PAMOJA NA RAIS MAGUFULI KUPIGA MARUFUKU SIASA MPAKA 2020 INAONEKANA NI SEHEMU YA MAISHA YETU YA KILA SIKU KAFULILA AIBUKA KISIASA SASA KUELEKEA MAHAKAMA YA RUFAA.

Siku 80 baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila imeelezwa kuwa Mahakama Rufaa imempatia fomu za matokeo namba 21B za vituo vyote 382 vya jimbo hilo na sasa yuko tayari kwenda kwenye rufaa.

“Nitakata rufaa,” alisema Kafulila jana wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa kumpatia fomu hizo ambazo alikuwa akizidai kwa udi na uvumba kabla ya hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Ferdinand Wambari, Mei 17.

Hata hivyo, Kafulila hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo jana akisema atazungumzia suala hilo kwa undani leo akiwa na wakili wake. Sababu kubwa iliyofanya kutupwa kwa kesi hiyo na kumtangaza Hasna Mwilima wa CCM kuwa mshindi halali, ni upande wa mlalamikaji kushindwa kutoa ushahidi ambao ungeishawishi Mahakama kutengua ushindi huo.

Chanzo : Mwananchi
 
Hi Selikari niya kibabe sana .nandiomana wanakomesha kwanza watu sugu
 
Yuko wapi Filikunjombe? Yuko wapi Kafulila. Yuko wapi Zitto?

Ni Zitto Tu ndio kabahatika kurudi kwenye Ubunge baada ya watatu hawa kuwa front line kwenye issue ya Escrow.

Hata mtumbua majipu kaufyta na wala hajawahi ongelea Escrow kwenye danadana zake za majigambo. Eti "Mimi" Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu.

Unapoteza rasilimali kuhakiki vyeti vya Shule ya msingi, unaacha kuhakiki Escrow, Lugumi, Kiwira, Nyumba za Umma, Richmond, meli Chakavu n.k.?!!!?

Napita tu.
 
Nchi hii ya ajabu sana mimi ningekuwa mkuu watu kama akina kafulila ni watu ambao hawatakiwi kukosekana bungeni,kwani hawa watu humsaidia sana mkuu kujua maovu yanayoendelea katika jamii yake.bila hao tungeijuaje escrow
 
Karibu kafulira ww ni kiongoz machachari ktk taifa letu bt ungekuwepo na ww ungekuwa umefungiwa miaka 2 usiingie bungeni
 
Yuko wapi Filikunjombe? Yuko wapi Kafulila. Yuko wapi Zitto?

Ni Zitto Tu ndio kabahatika kurudi kwenye Ubunge baada ya watatu hawa kuwa front line kwenye issue ya Escrow.

Hata mtumbua majipu kaufyta na wala hajawahi ongelea Escrow kwenye danadana zake za majigambo. Eti "Mimi" Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu.

Unapoteza rasilimali kuhakiki vyeti vya Shule ya msingi, unaacha kuhakiki Escrow, Lugumi, Kiwira, Nyumba za Umma, Richmond, meli Chakavu n.k.?!!!?

Napita tu.
Bora upite tu, wapi wanahakiki vyeti vya shule ya msingi?
 
Mtoa mada inaelekea hauna watoto wala ndugu!! Au mwenzetu huishi Tz?
 
View attachment 377163

PAMOJA NA RAIS MAGUFULI KUPIGA MARUFUKU SIASA MPAKA 2020 INAONEKANA NI SEHEMU YA MAISHA YETU YA KILA SIKU KAFULILA AIBUKA KISIASA SASA KUELEKEA MAHAKAMA YA RUFAA.

Siku 80 baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora kutupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila imeelezwa kuwa Mahakama Rufaa imempatia fomu za matokeo namba 21B za vituo vyote 382 vya jimbo hilo na sasa yuko tayari kwenda kwenye rufaa.

“Nitakata rufaa,” alisema Kafulila jana wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu uamuzi huo wa Mahakama ya Rufaa kumpatia fomu hizo ambazo alikuwa akizidai kwa udi na uvumba kabla ya hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Ferdinand Wambari, Mei 17.

Hata hivyo, Kafulila hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo jana akisema atazungumzia suala hilo kwa undani leo akiwa na wakili wake. Sababu kubwa iliyofanya kutupwa kwa kesi hiyo na kumtangaza Hasna Mwilima wa CCM kuwa mshindi halali, ni upande wa mlalamikaji kushindwa kutoa ushahidi ambao ungeishawishi Mahakama kutengua ushindi huo.

Chanzo : Mwananchi
Kwa hiyo ina maana form husika zilikuwa Mahakama ya Rufaa? Sijaelewa hapo
 
y
Yuko wapi Filikunjombe? Yuko wapi Kafulila. Yuko wapi Zitto?

Ni Zitto Tu ndio kabahatika kurudi kwenye Ubunge baada ya watatu hawa kuwa front line kwenye issue ya Escrow.

Hata mtumbua majipu kaufyta na wala hajawahi ongelea Escrow kwenye danadana zake za majigambo. Eti "Mimi" Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu.

Unapoteza rasilimali kuhakiki vyeti vya Shule ya msingi, unaacha kuhakiki Escrow, Lugumi, Kiwira, Nyumba za Umma, Richmond, meli Chakavu n.k.?!!!?

Napita tu.
tumeshamjua hana ubavu wa kupambana na ufisadi na hatafanya hivyo, alichokuwa anakifanya mwanzoni ilikuwa ni kupanga safu yake tu, rais anayepambana na ufisadi hawezi kuzuia bunge lisionyeshwe, na hawezi kuzuia mikutano ya siasa, huyu ndo rais muoga kuliko wote waliomtangulia.
 
Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu!
Asikate tamaa tu atafanikiwa km kweli haki yake ailiporwa
 
Yuko wapi Filikunjombe? Yuko wapi Kafulila. Yuko wapi Zitto?

Ni Zitto Tu ndio kabahatika kurudi kwenye Ubunge baada ya watatu hawa kuwa front line kwenye issue ya Escrow.

Hata mtumbua majipu kaufyta na wala hajawahi ongelea Escrow kwenye danadana zake za majigambo. Eti "Mimi" Nimejitoa Mhanga kutumbua majipu.

Unapoteza rasilimali kuhakiki vyeti vya Shule ya msingi, unaacha kuhakiki Escrow, Lugumi, Kiwira, Nyumba za Umma, Richmond, meli Chakavu n.k.?!!!?

Napita tu.
Haaaa haaaa
 
hizo hela za rufaa si akomae tu afanye biashara au alee MTOTO wake na jesca kishoya
 
Back
Top Bottom