Kafulila afunguka baada ya Magufuli kumsifia sakata la IPTL, asema CCM walimnyang'anya jimbo

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Mbunge huyo amesema ni heshima kubwa kwa sababu jambo hilo liliathiri sana maisha yake, na anashukuru Mungu mpaka leo yupo hai.

Na anatumaini rais kwa dhamira alioinyesha atachukua hatua za kutosha kama kuimarisha ofisi ya TAKUKURU na DPP na wahusika wote wachukuliwe hatua.

Akijibu swali kama sakata la Escrow ndio lilisoababisha yeye kushindwa amejibu vita hiyo imemgharimu mambo mengi na jimbo ni sehemu moja, ameongezea jimbo hilo hakushindwa bali alinyang'anywa baada ya kuibiwa sana ikashindikana akanyang'anywa na rekodi zipo na anaweza kuzionyesha na nguvu zilizotumika kumnyang'anya jimbo hazikua nguvu za kawaida

 
Akizungumza chochote kuhusu ukawa lazima Pombe imkane mchana kweupe. Pamoja na manguvu zaidi ya FARU lakini bado POMBE inamtesa sana. Utawala huu umejaa hofu kubwa sana kiasi cha mkulu kumwogopa dogo aliyebeba bango ambalo kimsingi halikuwa na madhara. Maskini kijana wa watu atakuwa ameshapimwa mkojo mida hii maana haijafahamika alikopelekwa.
 
Kafulila,Filikunjombe,Sendeka,Kilango,Zitto na Mnyika walihama jimbo mtajua walikua upande gani na matokeo yake
 
Huyu naye si angeshukuru tu... hayo alikuwa wapi tangu uchaguzi kuyaongelea tena.

Anakinyongo bado hafai kupata cheo huyu, labda abadilike. Kulalamikaaaaaaaaaaaaaa eti ayaonyeshe leo ndio kakumbuka yapo... ayaonyeshe basi... sio kulalamika baada ya kusifiwa hata kama labda hayo anayodai yalitokea... ila why leo... y sio jana au juzi... huyu kama anadanganya tu... mahakama kukata tufaa si kupo au!? kweli kuna binadamu wanashangaza shaaaaaaa. Pia bila siasa hawezi kufanya biashara au!? Kwani sie tusio kwenye siasa hatuishi!!
 
Kosa la
Mbunge huyo amesema ni heshima kubwa kwa sababu jambo hilo liliathiri sana maisha yake, na anashukuru Mungu mpaka leo yupo hai
Na anatumaini rais kwa dhamira alioinyesha atachukua hatua za kutosha kama kuimarisha ofisi ya TAKUKURU na DPP na wahusika wote wachukuliwe hatua
Akijibu swali kama sakata la Escrow ndio lilisoababisha yeye kushindwa amejibu vita hiyo imemgharimu mambo mengi na jimbo ni sehemu moja, ameongezea jimbo hilo hakushindwa bali alinyang'anywa baada ya kuibiwa sana ikashindikana akanyang'anywa na rekodi zipo na anaweza kuzionyesha na nguvu zilizotumika kumnyang'anya jimbo hazikua nguvu za kawaida


KAFULILA alifulia kwa sababu ya Kuunga mkono UKAWA against CCM ya KIKWETE na Mgombea Urais wakati kwa mara ya kwanza toka Tanzania ipate uhuru hakuna serikali ilijali MASLAHI YA WANAKIGOMA kama AWAMU YA NNE na JPM akiwa waziri wa UJENZI .... Kafulila alikosea njia kuunga mkono lile GENGE la MBOWE, LOWASSA na MAALIM... hawa sio wenzetu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom