Kafulila afichua siri za watumishi - kuna wanaolipwa 20,000,000/= kwa mwezi

Kwa mtindo huu kulipana mishahara na marupurupu chini ya meza kwa kutazamana tu sura bila vigezo maalum na ya wazi kwa kada zote katika taifa letu.

Tanzania yetu hii tutaendelea kupoteza kodi zetu nyingi sana kuzalishia mataifa mengine wataalam waliobobea katika fani zao na sisi tukibaki kutumikiwa na jopo kubwa la vilaza na mbumbumbu ambao kinga yao maofisini huko ni matumizi ya ndumba kila uchao na kupika majungu.

Tusahau kabisa kitu maendeleo kama hatuwezi kufanya National Rationalisation of Public Service Salaries and Allownces zenye kuendana na wakati, kuleta uwiano, kuongez morali ya kazi na enye kudhibitika for greater accountability needs.
 
Una maana kama Rais ana degree moja kama JK alipwe mshahara kidogo kulinganisha na waziri wake mwemnye PhD kama Prof Maghembe?

Elimu ni mojawapo tu ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara pia kuna uzoefu, Madaraka/Cheo, Specialization etc. Kwenye vyeo vya kisiasa kama Urais, Uwaziri, PS, Ubunge, U-kuu wa Mkoa na Wilaya etc, ELIMU huwa sio KIGEZO Kabisa, ndiyo maana utamkuta DC STD VII anapokea mshahara na marupurupu sawa kabisa na DC PhD holder!

mboana ata sasa kuna watu kama mkurugenzi wa Tanroads anawazidi waziri wa ujenzi na ata rais kwa mshahara sasa utashangaa waziri akimzidi rais mshahara?
 
Kafulila(4).jpg
427254_283836905017217_100001727290468_821661_1663231869_n.jpg

Kafulila mbunge wa Kigoma Kusini

Naye mbunge machachari wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, ambaye yuko kwenye mzozo na chama chake kilichomfukuza uanachama, alisema kinachosumbua kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wenye usawa wa ulipaji mishahara na posho ndani ya serikali.

Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.

“Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000,” alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.

Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.

IPP Media
Kafulila nakupongeza sana kuonyesha kiini cha matatizo. Tumeuvamia Ubepari na sasa tunajikuta taabani..
 
Du! hizo 20m zingeweza kutoa ajira ngapi kwa wahitimu wamwaka jana waliopunguziwa ajira kwa aslmia 50 . Kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti mfikirie yule mwalimu wa ir anayetumia darasa la majani ya ufuta na mshara wa laki na nusu kwa mwezi, hivi ipo cku atajivunia kufanya kazi tan
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli, kila mahali panapoingiza kipatao kikubwa basi na wafanya kazi walipwe kutokana na hicho kipato na si kwa kuwa fulani analipwa laki mbili basi nchi nzima walipwe laki mbili, ndio mtazidisha wizi na ufisadi. Unamlipa mtu mpaka anakuwa hana ya kuiba.

Millioni 18 au 20 kwa mtu anelinada mabilioni si kichekesho hicho.

Hawa madaktari ichwara mimi nilishasema kima cha chini kabola ya marupurupu walipwe million 5, hiyo ni fair kabisa, lakini wawe wamemaliza intern na wamesha fanya kazi miaka miwili.

Kabola = kabla.

Mama uwe makini, hilo jina la mtu.
 
Jamani..................jamani...........Jamani.......Aisee kumbe watu wanafaidi hivi! Poa, ipo ck.
 
Hao wanaolipwa mishahara mikubwa hata viongozi (politicians) wanawaogopa! Wengine walipewa support wakati wa kampeni. Hiki kizazi kilicho madarakani hakitatufikisha popote! Wengi ni wezi. Wale ambao si wezi basi ni waoga kufanya maamuzi.
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli, kila mahali panapoingiza kipatao kikubwa basi na wafanya kazi walipwe kutokana na hicho kipato na si kwa kuwa fulani analipwa laki mbili basi nchi nzima walipwe laki mbili, ndio mtazidisha wizi na ufisadi. Unamlipa mtu mpaka anakuwa hana ya kuiba.

Millioni 18 au 20 kwa mtu anelinada mabilioni si kichekesho hicho.

Hawa madaktari ichwara mimi nilishasema kima cha chini kabola ya marupurupu walipwe million 5, hiyo ni fair kabisa, lakini wawe wamemaliza intern na wamesha fanya kazi miaka miwili.
Swadakta, na ndio maana nimesema Ubepari tumeuvamia maana watu wanachanganya sana siasa za Kijamaa na zile za Kibepari. Mtumishi wa serikali anataka kujilinganisha na mashirika binafsi, kila mtu apewe kipande cha keki sawa ktk kugawana umaskini..

Nilichopenda kuhusu Kafulila kaonyesha wazi jinsi tunavyotofautiana kiitikadi, yeye kama Mjamaa nadhani yuko sawa kabisa na ndivyo wadanganyika wengi wanafikiria kwamba mwajiriwa ana nguvu ya kuilazimisha serikali au shirika limuongezee posho na mshahara ghafla bin vuu..

Katika Ubepari kama huitaki kazi kwa sababu ya mshahara unaacha unaenda tafuta sehemu nyingine, wapo wengine watakao ridhia na kuchukua nafasi hiyo... bahati mbaya tumechukua mfumo huu tukiwa hatuna wataalam wa kutosha lakini tunataka mgao sawa wa kipande cha keki.
 
Swadakta, na ndio maana nimesema Ubepari tumeuvamia maana watu wanachanganya sana siasa za Kijamaa na zile za Kibepari. Mtumishi wa serikali anataka kujilinganisha na mashirika binafsi, kila mtu apewe kipande cha keki sawa ktk kugawana umaskini..

Nilichopenda kuhusu Kafulila kaonyesha wazi jinsi tunavyotofautiana kiitikadi, yeye kama Mjamaa nadhani yuko sawa kabisa na ndivyo wadanganyika wengi wanafikiria kwamba mwajiriwa ana nguvu ya kuilazimisha serikali au shirika limuongezee posho na mshahara ghafla bin vuu..

Katika Ubepari kama huitaki kazi kwa sababu ya mshahara unaacha unaenda tafuta sehemu nyingine, wapo wengine watakao ridhia na kuchukua nafasi hiyo... bahati mbaya tumechukua mfumo huu tukiwa hatuna wataalam wa kutosha lakini tunataka mgao sawa wa kpande cha keki..

Lakini mzee huo ubepari upo kama haupo; kwa sababu bado serikali haijakiri rasmi (legally kupitia katiba) kwamba tumeacha ujamaa na kufuata ubepari.
Ndio maana bado naweza kusema kwamba Tanzania inatumia mfumo wa ujepari (ujamaa+ubepari).

Hivyo mikanganyo kama inayotolewa na akina Kafulila ipo sawa kutokana na mfumo ambao unatambulika rasmi katika katiba.

Jambo la msingi hapa ni kuangalia namna gani (kwa hii katiba ya sasa) tunaweza kuishinikiza seriklai ifanye maboresho makubwa katika mfumo mzima wa mishahara ya watumishi wa umma. Naelewa mishahara hiyo haiwezi kuwa kama ya sekta binafsi, lakini serikali inaweza weka mishahara mizuri na mazingara ya kazi mazuri ambayo yatatoa motisha kwa watumishi na ambayo yatazingatia weledi wa watumishi.
 
Hao ndo vionozi wetu waliopewa dhamana ya kuongoza akili zetu, maisha na pia "kuongoza" katika kupata mishahara minono. Inabidi sera ya inzi kufia kwenye kidonda ibadilike, labda mambo yanaweza kuwa sawa.
 
Kweli Viongozi wa Tanzania wanatia hasira sana! Yaani wamekuwa wachumia tumbo hata haya hawana! Agrrrrrrrrrrrrrrrrrr!
 
Lakini mzee huo ubepari upo kama haupo; kwa sababu bado serikali haijakiri rasmi (legally kupitia katiba) kwamba tumeacha ujamaa na kufuata ubepari.
Ndio maana bado naweza kusema kwamba Tanzania inatumia mfumo wa ujepari (ujamaa+ubepari).

Hivyo mikanganyo kama inayotolewa na akina Kafulila ipo sawa kutokana na mfumo ambao unatambulika rasmi katika katiba.

Jambo la msingi hapa ni kuangalia namna gani (kwa hii katiba ya sasa) tunaweza kuishinikiza seriklai ifanye maboresho makubwa katika mfumo mzima wa mishahara ya watumishi wa umma. Naelewa mishahara hiyo haiwezi kuwa kama ya sekta binafsi, lakini serikali inaweza weka mishahara mizuri na mazingara ya kazi mazuri ambayo yatatoa motisha kwa watumishi na ambayo yatazingatia weledi wa watumishi.
Kama Watanzania wote wangekuwa na mawazo kama yako nadhani ingekuwa rahisi kufikia suluhisho la matatizo yetu. Hatutaki kukubali wala kuamini kwamba Itikadi ndizo zinajenga msimamo wa chama na serikali, leo hii hatupo ktk Ujamaa wala hatupo ktk Ubepari na sii vyama wala wananchi wenyewe.
 
MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA NA MARUPURUPU YA ENZI ZA SERA YA 'UJAMAA NA KUJITEGEMEA' INAPOLAZIMISHWA KUTUMIKA KATIKA KIPINDI KIPYA TAIFA LINAPOFUATA MFUMO WA 'UBEPARI NA NGUVU YA SOKO' JUMLA YAKE NI MIGOMO ISIOISHA NA KUKIMBIWA NA WATAALAM KUFAIDI UTANDAWAZI KWINGINEKO DUNIANI

CCM, ukweli wa mambo ni kwamba kiuhakika hatuwezi kuendele hivi na mfumo wa zamani wa kulipana mishahara na marupurupu kama tulivyokua tukifanya enzi za sera za UJAMAA NA KUJITEGEMEA wakati santuri tayari tumeubadilisha wenyewe kupitia Azimio la Zanzibar.

Mantiki ni kwamba ukitaka kubadilisha matumizi ya gari yako toyota saloon kutoka katika matumizi yake ya kawaida kwenda ofisini na kufikisha watoto shule hadi kutamani sasa iwe sasa ni ya kusombe vikungu vya ndizi katika milima ya Moshi huko kwenda Arusha, mara hii ni kwamba usiishie tu katika kung'oa viti vya nyuma bali ni kwamba sharti uende mbele zaidi kubadilisha mitairi, nyanyua gari yako juu na ikiwezeka iwekee injini ya lendirova ili walau kusudio lako hilo lionekane linaendana na matarajio hata hivo.

Something is seriously wrong with our public service renumeration system na kwanza ni mshangao wangu sana kwamba kwa mtindo huu kweli viongozi wetu kweli mlikua hamjatishiwa hata siku moja kuchomwa moto maofisini na watumishi hawa wanavyopunjika kiasi hiki!!!!!!!!

Katika hili nasema mshukuruni sana Mwalimu Nyerere kwa malezi bora ya taifa kwa upole wote huu lakini kusipofanyika jambo lenye kubadilisha mambo leo tujue tutakumbana na kizazi kingine kabisa ambacho hakikulelewa na Baba wa Taifa hivyo hadi hapo kitu gani kitafuatia; naona utabiri wako una ushwari sawa kabisa na mimi hapa nilivyokua nikiwaza juu ya changamoto ya malipo bila uwiano wala uwazi ndani yake kote nchini.

Someone somewhere within the government and its institutions has apparently been SLEEP ON THE JOB of not have rationalised a new nationwide renumeration system that is stakeholder-friendlier, more transparent and offering a fit with times tha we live today.

It is with my humbly view that this 'someone fond of sleeping on job' either choses to give way today or start the work on a serious note to help keep in hold any further streak of strikes in the country.

Kimsingi, haiwezekani wengine waonekane kufanya kazi ya kanisa hapa wakati wenzao wengine wanakula na kusaza wakati soko lao ni lile lile Kariakoo anakoenda mwalimu wa shule ya Msingi Hananasif kule Kinondoni na vivyo hivyo ndivyo afanyavyo mke wa Gavana wa BoT; tutaonan wabaya hapa!!!!!!!!!!
 
..gavana wa Benki Kuu ya Tanzania analipwa zaidi ya Chairman wa US Federal Reserve. kitu cha kusikitisha unakuta hawatosheki wanaongezea na ufisadi.
 
Back
Top Bottom