Kafulila afichua siri za watumishi - kuna wanaolipwa 20,000,000/= kwa mwezi

HATUTAKI HUU MFUMO HOLELA WA KULIPANA MISHAHARA NA MARUPURUPU SERIKALINI KWA KUWA INALEA MISINGI YA UVUJAJI WA KODI ZETU NA WACHACHE HUKU WATUMISHI WENGI WAKIGEUKIA RUSHWA KAMA HAKI KWAO

Hakika inakatisha kabisa tamaa kuona mambo kama haya serikali miaka yote hii KULIPA MSHAHARA NA MARUPURUPU kwa watumishi wetu BILA UWIIANO wowote kiasi hiki???????????

Kama uhalisia wa mambo serikalini ndio hivi basi haishangazi kwa nini RAIS KIKWETE KILA SIKU HAISHIWI HAMU YA KURUKA MAWINGUNI kwenda Ughaibuni. Msingi wa kile kinachomsukuma huyu baba wala si uzalendo wala utumishi bora kwa umma bali ni hako ka mwanya kanakojitokeza kutokana na MFUMO HOLELA wa kulipana mishahara na marupurupu bila uwiano tena kwa siri kubwa bila chembe cha uwazi.

Ni wakati muafaka taifa tukapiga mahesabu ni kiasi gani tumemlipa huyu baba katika safari zake zote tangu aingie madarakani na pamoja na mijopo kubwa anayosafiri nayo nje ya nchi kila uchao ikilinganishwa na faida tulizoingiza kutokana na kila safari - tusiwe tukajikuta tunafanya kazi za kuuza zizi zima la ng'ombe wetu kufadhili safari zenye faida ya yai la kuku hapa.

Asante sana Mh Kafulila kwa taarifa hii nyeti sana ambayo serikali yetu haikuwahi kupenda mlipakodi yeyote wa nchi hii ajue; sasa naanza kuelewa kwa kina zaidi na hata kumuonea HURUMA SANA Mhe Dr Hosea na jukumu lake la kupiga vita rushwa nchini. Mpaka hapa hapana shaka kwamba kumbe NI SERA RASMI YA SERIKALI YA CCM kulea misingi ya rushwa nchini wenyewe.

Haingii akilini bwana fedha BoT aandike cheki ya kulipa mishahara TSH 20,000,000/- kwa mwezi na marupurupu ya kukata na shoka wakati yeye anajiambulia Milioni 1.2 na posho kiduchu hata akaacha kukaa kwenye KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI MITHILI YA MFARANYAKI Iringa kusuka mpango mzima na Rostam Aziz juu ya namna gani ya kutuibia walipakodi kwa mtindo wa EPA ili naye apate chochote cha juu.

Mpaka hapa sina shaka kwamba ufisadi uliokubuhu serikalini hivi sasa (Financial Mismanagement; first degree corruption and inappropriation of funds) si ugonjwa wa kutibika leo wala kesho mpaka siku tutakapoamua kulipana kwa kufuata mfumo unaoeleweka kwa wote.

Walipa kodi sasa tujitokeze kuingilia kati kuitisha mjadala wa kitaifa juu ya mfumo mzima wa kulipana mishahara na miposho kwa uwiiano unaoeleweka.

Kumbe ndio maana watumishi wetu wengine huko maofisini utawakuta wapo wapo tu kama walishajikatia tamaa vile huku wengine ni kutegea tu kazi na morali ya chini sana eeehh!!!!!!!!!!!

Bila kuchelewa, walipakodi tunahitaji kuundwa kwa chombo cha taifa kitakachofanya kuwepo MFUMO WA KUELEWEKA NA WA WAZI ZAIDI utakaoleta uwiiano juu ya ulipaji mishahara na marupurupu kwa watumishi wote serikalini tangu Balozi wa nyumba kumi hadi rais wa nchi. Hatutaki usiri zaidi katika eneo mojawapo ambapo walipakodi tunatumia fedha nyingi ajabu kulidumia bila tija kama ulipaji mishahara na posho kwa watumishi wetu hawa.

Nasema hili likishindikana kutekelezwa basi walipakodi tutakua na uhalali kabisa kisheria kuinyima kabisa serikali yetu kodi zetu mpaka kutandazwe mfumo unaokubalika jinsi gani kodi zetu zitatumika kutuvunia faida na tija kubwa zaidi kwa miradi na watumishi wetu kuliko hali ilivyo hivi sasa.

Maafisa wetu TAKUKURU pamoja na Dr Hosea, nawapeni pole sana kwa kutambua leo hii chngmoto mnazozipata kika kupiga vita rushwa katika bahari ambamo cheo kimoja watu hulipana kiujanjaujanja kwa kufuata mifumo wanaojua wenyewe kwa MISINGI YA KUTAZAMANA TU SURA.

Hakika kwa mtindo huu Dr Hosea, hiki cheo chako hicho hata angepewa malaika toka moja kwa moja mbinguni wala hawezi kudhiti rushwa Tanzania hata kwa robo. Pole sana mwenzetu, jibu nimelipata leo!!!!!!!!


Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.

“Angalia Gavana wa Benki Kuu
analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000,” alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.

Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi
posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (SHah. 1,280,000) kwa siku.

IPP Media
 
Huyu kashapotea...sina hata hamu ya kumsikiliza!!
Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??
 
Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??
naona hapa kuna haja ya kufanya utafiti zaidi maana inawezekana wenyewe 'miezi' yao ni tofauti na wengine hili tukijua hilo tukae kimya. Maana imesemwa katika baadhi ya Maandiko kuwa siku inaweza kuwa mwaka au mwaka kuwa sawa na siku!
 
Huyo nae ndio nini kuvaa tai la pinki? au ndio "pinky pinky"?

Dada Faiza na wewe! una macho makali kweli! I guess punde tu utatuambia hata rangi ya c.h.u.p.i aliyovaa!

Keep it up dada Faiza, atafutaye hachoki na akichoka jua ameshapata
 
mimi kinanikera kitendo cha kujadilikwa jumla mbunge au mfanyakazi fulani alipwe shilingi ngapi. mimi nataka watu walipwe kulingana na elimu yao kama mbunge ni darasa la saba au darasa la 12 alipwe kulingana na darasa lake.

Na kama mbunge ni profesa alipwe sawa na maprofesa wengine.....unakuta mbunge ni darasa la saba anataka kujilinganisha na wafanyakazi kwenye sekta nyingine wenye degree mbili hii sio haki
 
Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??
Hili swali lako Slaa atakuwa na nafasi nzuri sana kulijibu zaidi yangu mimi!!!!
 
mimi kinanikera kitendo cha kujadilikwa jumla mbunge au mfanyakazi fulani alipwe shilingi ngapi. mimi nataka watu walipwe kulingana na elimu yao kama mbunge ni darasa la saba au darasa la 12 alipwe kulingana na darasa lake na kama mbunge ni profesa alipwe sawa na maprofesa wengine.....unakuta mbunge ni darasa la saba anataka kujilinganisha na wafanyakazi kwenye sekta nyingine wenye degree mbili hii sio haki

Una maana kama Rais ana degree moja kama JK alipwe mshahara kidogo kulinganisha na waziri wake mwemnye PhD kama Prof Maghembe?

Elimu ni mojawapo tu ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara pia kuna uzoefu, Madaraka/Cheo, Specialization etc. Kwenye vyeo vya kisiasa kama Urais, Uwaziri, PS, Ubunge, U-kuu wa Mkoa na Wilaya etc, ELIMU huwa sio KIGEZO Kabisa, ndiyo maana utamkuta DC STD VII anapokea mshahara na marupurupu sawa kabisa na DC PhD holder!
 


Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.

"Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000," alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.

Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.



Duh!! Yaani hizi njemba zinavyolipana mapesa yote hayo utafikiri zinazalisha chochote chenye manufaa kwa taifa hili.

Ebu angalia malipo hayo, halafu fafanisha na malipo apatayo mhadhiri wa chuo kikuu cha umma ambaye ndie kazalisha hizo njemba:

  1. V.C katika vyuo vya umma anapata takribani tsh. 5.5 million kwa mwezi kama mshahara; hapo anaweza kuongezewa na responsibility allowance ya tsh.1.1 million.
  2. Deputy V.C katika vyuo vya umma anapata takribani tsh. 5.3 million kama mshahara, na responsibility allowance ya tsh. 1 million
  3. A full professor katika vyuo vya umma anapata takribani tsh. 4 million kama mshahara kwa mwezi; allowances nyingine itategemea kama ana cheo chochote.
  4. An associate professor katika vyuo vya umma anapata takribani tsh. 3.8 million kama mshahara, pia allowances itategemea kama ana cheo chochote.
  5. A senior Lecturer anapata takribani tsh. 3.4 million kama mshahara; allowances ni kama namba 3 na 4.
  6. A lecturer anapata takribani tsh. 2.6 million kama mshahara.
  7. An assistant lecturer anapata takribani tsh. 1.8 million kama mshahara
  8. A tutotial assistant anapata takriban tsh. 1.5 million kama mshahara.
NB: Hii mishahara ni kwa mujibu wa GN ya Julai, 2010. Najua sasa inaweza kuwa imepanda kidogo; lakini hivyo ndivyo wazalisha nguvu kazi hapa Tanzania wanavyolipwa.

Ndio maana wengi wanakimbilia kuwa wanasiasa au wengine wanajikomba kwa wakubwa ili wapewe vinafasi katika bodi za mashirika au ukurugenzi katika mashirika ya umma!! Na wengine wanakua hawarudi wakienda kusoma nchi za nje, ambako kwa wastani a full professor katika vyuo vya umaa uweza kupata US$ 99,000 kwa mwaka!
 
Mishahara haiwezi kuwa sawa hata siku moja na huwezi kulinganisha mshahara wa gavana wa benki kuu na daktari wa kawaida. Ila unaweza kulinganisha mshahara wa gavana na neurosurgeon au cardiologist. Wanasiasa wasitake kudanganya umma, kwa hili tatizo.

Kinachotakiwa hapa ni kuona je mshahara wa laki 9 ni sawa kwa daktari ambaye fani yake ni rare huku mbunge akipokea mil 1.8? Ni muhimu kufanya "job analysis" katika sekta ya umma.

Halafu huwezi kulinganisha mshahara wa waziri na mkurugenzi wa shirika lililo chini yake hafahamu hata system ya career progression inayotumika ktk utumishi wa umma. Wanasiasa (mawaziri) mishahara yao sio mikubwa kiasi hicho kama anavyotaka watu tuamini, isipokuwa huku Afrika.

Yeye anadhani Rais wa Marekani analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa NASA? Au analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa CDC? Asidhani wananchi hatujui haya mambo tunafahamu sana.
 
Una maana kama Rais ana degree moja kama JK alipwe mshahara kidogo kulinganisha na waziri wake mwemnye PhD kama Prof Maghembe?

Elimu ni mojawapo tu ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara pia kuna uzoefu, Madaraka/Cheo, Specialization etc. Kwenye vyeo vya kisiasa kama Urais, Uwaziri, PS, Ubunge, U-kuu wa Mkoa na Wilaya etc, ELIMU huwa sio KIGEZO Kabisa, ndiyo maana utamkuta DC STD VII anapokea mshahara na marupurupu sawa kabisa na DC PhD holder!

Hii sio sawa kabisa. Kuna haja ya kufanyiwa marekebisho. Haiwezekani hata kidogo.
Mfano, Marekani professor wa molecular biology and biotechnology halipwi sawa na professor wa literature or history; professor wa MBB analipwa zaidi, na hiyo inakua ni kama motisha na compensation kwa kazi zake.

Hivyo lazima hata Tanzania tuwe na mfumo wa malipo unaoendana na aina ya kazi na utaalamu. Yaani haiwezekani professor wa Kiswahili alipwe sana na professor wa renewable energy pale UD. Hapa simaanishi kudharau taaluma za watu, lakini huo ndio ukweli wenyewe inabidi nchi ianze kutumia mfumo wa aina hii, ili kuto motisha kwa taaluma ambazo zinahitajiwa sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo.
 
Suala hili linahitaji kuangaliwa kwa umakini. Mishahara ya wataalamu imeboreshwa ili kuzuia watu kwenda nje. Nadhani kasoro ni kwamba haikuwafikia wataalamu wengine kama madaktari nk.
 
Mishahara haiwezi kuwa sawa hata siku moja na huwezi kulinganisha mshahara wa gavana wa benki kuu na daktari wa kawaida. Ila unaweza kulinganisha mshahara wa gavana na neurosurgeon au cardiologist.

Wanasiasa wasitake kudanganya umma, kwa hili tatizo. Kinachotakiwa hapa ni kuona je mshahara wa laki 9 ni sawa kwa daktari ambaye fani yake ni rare huku mbunge akipokea mil 1.8? Ni muhimu kufanya "job analysis" katika sekta ya umma.

Halafu huwezi kulinganisha mshahara wa waziri na mkurugenzi wa shirika lililo chini yake hafahamu hata system ya career progression inayotumika ktk utumishi wa umma. Wanasiasa (mawaziri) mishahara yao sio mikubwa kiasi hicho kama anavyotaka watu tuamini, isipokuwa huku Afrika.

Yeye anadhani Rais wa Marekani analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa NASA? Au analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa CDC? Asidhani wananchi hatujui haya mambo tunafahamu sana.

Vyema. Ndio maana ninapendekeza kwa serikali yetu kuangalia upya mfumo wa malipo kwa watumishi ambao ndio watendaji na ambao ndio wanategemewa katika kusukuma gurudumu la maendeleo.

Haiingii akilini kuona mtu kama Lusinde au Ngonyani anapata pesa nyingi kuliko wahadhiri katika vyuo vyetu vya umma.

Lazima sasa tuilazimishe serikali ku-appreciate taaluma za watumishi ambao mchango wao katika maendeleo ya taifa ni mkubwa na wa muhimu sana.
 
Kweli inasikitisha, kama alivyolala huyo jamaa hapo (mbunge wa jimbo maskini/wilaya maskini) tu analipwa 230,000/= per day!!! nchi haina mwenyewe
 
Mbona ni mishahara midogo sana hiyo kwa watu wanaolinda mabilioni, nilitegemea dau awe anachukuwa kama milioni 200 kwa mwezi kumbe millioni kumi na nane tu? huu ni uonevu wa hali ya juu. Ma CEO wa kampuni binafsi zenye ukubwa kama wa NSSF wanakula mihela kibao duniani. Wafikiriwe hawa watu.

Bila shaka unahalisha wewe bibi.
 
Back
Top Bottom