Rejao
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 9,220
- 4,056
Hapa kwani kuna siri gani? Hamna mtu asiyefahamu TZ hii ni sehemu gani watumishi wake wanalipwa vizuriKapotea kutoa hy siri?
mimi ni independent person!Kwa kuwa amewagusa mabwana mkubwa wako?
Hapa kwani kuna siri gani? Hamna mtu asiyefahamu TZ hii ni sehemu gani watumishi wake wanalipwa vizuriKapotea kutoa hy siri?
mimi ni independent person!Kwa kuwa amewagusa mabwana mkubwa wako?
jadili hoja hakuna sababu ya kumshambulia kafulila. We rajeo unaonaje juu ya tofauti za mishahara ya watumishi wa umma bila kufuata uwiano wa utendaji na uwajibikaji wao katika utumishi?
Hili la posho za kusafiri nje pamoja na sitting allowance madhara yake ni makubwa sana kwa mustakabali wa Taifa. Ukiangalia kwa undani, moja ya sababu kubwa kwa nchi yetu kuwa na mikataba mibovu katika uendeshaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ni hili suala la sitting allowance pamoja na posho za kusafiri nje.
Mara nyingi pale linapotokea suala la kwenda kujadili ama kuandaa rasimu za mikataba mbalimbali wanaoteuliwa kwenda kufanya shughuli hizo sio wale wataalamu husika bali huteuliwa watu fulani ama hujiteua (kwa manufaa yao binafsi) kwenda kufanya shughuli hizo pasipo kuwa na uelewa wowote ili tu waweze kukomba hizo posho za safari na mwisho wa siku wanaishia kwenda kutalii tu bila kutekeleza kilichowapeleka huko.
Tatizo hili pia linaadhiri mfumo wa ajira katika maeneo fulani ya Serikali kwani waajiri wenyewe wanaangalia wapi kuna safari nyingi ama mishahara yake iko juu ili waweze kujichomeka wenyewe ama kuwaingiza wale wanaowafahamamu pasipo kuangalia uwezo wa kiutendaji na uadilifu kwa wale wanaowaweka kwenye nafasi hizo.
Hivi ni kwa nini watu hupenda kutoa takwimu za kubuni bila kuzifanyia uchunguzi...? Kwa mfano mimi nina ushahidi kuwa gavana wa BOT hulipwa USD 25,000 sio Tzs 20m . kwa hiyo natilia mashaka takwimu nyingine kwa kuwa kwa hii niiijuayo ya BOT governor imepunguzwa sana Tzs 20m sidhani kama Tanzania ingeweza kumpata ndulu kutoka WB!!!
Good boy Kafulila angalau kwa kuthubutu kutujulisha mishahara na posho za hawa wakubwa;
1.Gavana wa benki kuu tsh.20m/-
2.Mkurugenzi mkuu NSSF tsh.18m/-
3.Junior Officer TRA & BOT tsh.7m/-
4.Mbunge tsh.1.8m/-
Pinda alitueleza mishahara ya hawa wafuatao;
5. Daktari tsh.900,000.00
6.Mhandisi tsh.600,000.00
7.Mhasibu tsh.368,000.00
Nami naongezea;
8.Mkurugenzi mkuu NHC tsh.20m/-
Hii nchi inaliwa na watu wachache sana, as if wao tu ndio watanzania!
Huyu kashapotea...sina hata hamu ya kumsikiliza!!
Pamoja na mshahara mkubwa anaolipwa ndulu hakuna deliverables zozote uchumi hovyo kabisa, shilingi yetu inadorora kila siku bora aondoke kuliko kuzidi kuharibu uchumi wa nchiHivi ni kwa nini watu hupenda kutoa takwimu za kubuni bila kuzifanyia uchunguzi...? Kwa mfano mimi nina ushahidi kuwa gavana wa BOT hulipwa USD 25,000 sio Tzs 20m . kwa hiyo natilia mashaka takwimu nyingine kwa kuwa kwa hii niiijuayo ya BOT governor imepunguzwa sana Tzs 20m sidhani kama Tanzania ingeweza kumpata ndulu kutoka WB!!!
Tukumbuke kuwa mishara inayojadiliwa hapa ni mishara ya taasi za serikali/agencies. Ukitaka kuziangalia, hizi taasisi/mashirika yameanzishwa kisheria kwa ajili ya kuregulate masuala fulani either fedha, hifadhi za jamii, miindombinu, mawasiliano, biashara, afya nk. Hawa wanafanya kazi independently na central/local government. Hawa ni kama semi-government, wanajiamulia mambo yao wenyewe, including mishahara.
Sioni kama haya mashirika yanatakiwa yalaumiwe kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mishahara cuz ni kutokana na majukumu na dhamana waliyoibeba. Ndani ya hayo mashirika kuna madaktari, waalimu, wahandisi, wahasibu na watu wa kila professional!
Chamuhumu hapa ni kuangalia serikali itainua vipi mishahara ya watumishi wake wa Central n Local government ireflect current state ya economy na mfumuko wa bei uliopo!