Kafulila afichua siri za watumishi - kuna wanaolipwa 20,000,000/= kwa mwezi

Mwajiri wangu hajui wala haendekezi posho, niko nae tangu Mwanza 2004
Business trip zote zinaandaliwa na kampuni na hutasafiri kwa ndege au gari na kuandaliwa hotel first class nikimaanisha zenye hadhi, iwe Move n' pick (by then) Sea Cliff, New Africa, Holiday Inn, Southern Sun and the like.
Utakula na kunywa vinywaji baridi kadri upendavyo, drink beer & related staff reasonable quantity.
Kwa mwajiri wangu safari za kiofisi is the same as huko ofisini kwako na hivyo does not atttact any extra income out of your salary and other contractual allowances (eg house allowance)

Mwajiri anahakikisha unasafiri vizuri, unalala pazuri, unakula/kunywa vizuri pia na hatimaye baada ya kukamilisha shughuli ya safari unarudi ktk kituo cha kazi vizuri pia.
Tofauti ipo kidogo ni kwa safari za nje, unapewa incidental/emergence allowance but will have to account for on your return to the office. bado fedha hizo kidogo kama utanunua vitu binafsi basi lazima zitakatwa kwenye mshahara wako.

Kwangu mimi na mwajiri wangu hatuna kabisa seating allowance na anapenda hata tunapopata mialiko toka taasisi zingine tunazofanya nazo kazi tusipokee hizo allowance. Na kimsingi mialiko ambayo muandaaji akionyesha kwa maandishi katika mwaliko wake kuwa kutakuwa na cash allowance nje ya accommodation mara zote haitolewi ruhusa ya kuhudhuria.
 
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu sana ..................................


Hizi zote ni kelele za chura wala hazimnyimi tembo kunywa maji (CCM). Bado 2015 wanaendelea tena, Na hapo ndo kitakuwa kilio na kusaga meno.
 
Kafulila(4).jpg


Kafulila mbunge wa Kigoma Kusini

Naye mbunge machachari wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, ambaye yuko kwenye mzozo na chama chake kilichomfukuza uanachama, alisema kinachosumbua kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wenye usawa wa ulipaji mishahara na posho ndani ya serikali.

Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.

"Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000," alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.

Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.

IPP Media

Hili la posho za kusafiri nje pamoja na sitting allowance madhara yake ni makubwa sana kwa mustakabali wa Taifa. Ukiangalia kwa undani, moja ya sababu kubwa kwa nchi yetu kuwa na mikataba mibovu katika uendeshaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ni hili suala la sitting allowance pamoja na posho za kusafiri nje.

Mara nyingi pale linapotokea suala la kwenda kujadili ama kuandaa rasimu za mikataba mbalimbali wanaoteuliwa kwenda kufanya shughuli hizo sio wale wataalamu husika bali huteuliwa watu fulani ama hujiteua (kwa manufaa yao binafsi) kwenda kufanya shughuli hizo pasipo kuwa na uelewa wowote ili tu waweze kukomba hizo posho za safari na mwisho wa siku wanaishia kwenda kutalii tu bila kutekeleza kilichowapeleka huko.

Tatizo hili pia linaadhiri mfumo wa ajira katika maeneo fulani ya Serikali kwani waajiri wenyewe wanaangalia wapi kuna safari nyingi ama mishahara yake iko juu ili waweze kujichomeka wenyewe ama kuwaingiza wale wanaowafahamamu pasipo kuangalia uwezo wa kiutendaji na uadilifu kwa wale wanaowaweka kwenye nafasi hizo.
 
Badala ya kulalama baada ya kukwapua posho ya 200,000/= alipaswa kuchukua hatua kama viule kupeleka hoja binafsi ya kurekebisha suala hilo,


hoja yake ni kwamba, wabunge nao waongezewe posho zao zifikie za TRA NA NSSF NA BoT. haridhiki na mishahara yake
 
Good boy Kafulila angalau kwa kuthubutu kutujulisha mishahara na posho za hawa wakubwa;

1.Gavana wa benki kuu tsh.20m/-
2.Mkurugenzi mkuu NSSF tsh.18m/-
3.Junior Officer TRA & BOT tsh.7m/-
4.Mbunge tsh.1.8m/-

Pinda alitueleza mishahara ya hawa wafuatao;
5. Daktari tsh.900,000.00
6.Mhandisi tsh.600,000.00
7.Mhasibu tsh.368,000.00


Nami naongezea;
8.Mkurugenzi mkuu NHC tsh.20m/-

Hii nchi inaliwa na watu wachache sana, as if wao tu ndio watanzania!
 
Good boy Kafulila angalau kwa kuthubutu kutujulisha mishahara na posho za hawa wakubwa;

1.Gavana wa benki kuu tsh.20m/-
2.Mkurugenzi mkuu NSSF tsh.18m/-
3.Junior Officer TRA & BOT tsh.7m/-
4.Mbunge tsh.1.8m/-

Pinda alitueleza mishahara ya hawa wafuatao;
5. Daktari tsh.900,000.00
6.Mhandisi tsh.600,000.00
7.Mhasibu tsh.368,000.00


Nami naongezea;
8.Mkurugenzi mkuu NHC tsh.20m/-

Hii nchi inaliwa na watu wachache sana, as if wao tu ndio watanzania!

Mkurugenzi wa TANROAD: > TSH 20 MIL
 
Duuu mama yangueeeeee yaani na huu umatonya wetu serikali inalipa viongozi mishahara mikubwa kiasi hiki!!
 
hoja yake ni kwamba, wabunge nao waongezewe posho zao zifikie za TRA NA NSSF NA BoT. haridhiki na mishahara yake

Hapo kwenye red Hawa vikao vyao havina posho labda vile vya bodi tuu.
Pia nimejaribu kufuatilia mishaara yao wanaolipwa vizuri ni wachache sana hasa wale wa ngazi ya pincipal kwenda juu ambao idadi yao haifiki hata 20% ya watumishi wote kadhalika taasisi hii siyo ya kuishobokea saaana hawa wanachukua nafasi ya 12 kati ya taasisi zinazolipa vizuri hapa nchini BOT, TBL, PPF,NSSF,TIGO,VODA,NMB, n.k
ukimwona mwenye maisha posh sana huyo ni wa kuangalia with open eye kama hii nchi ingekuwa inaendeshwa na utawala wa sheria. lakini sasa kama bunge lenyewe limeshindwa kuwadhibiti nishati na madini kwa michango batili na forgery za wazi wazi hatuna la kufanya tumshukuru mungu tuu kwa yote.

 
Hili suala la mishahara ya wafanyakazi wa umma pamoja na posho zao halijakaa vizuri hata kidogo pia utaratibu waposho sioni sababu ya mtumishi kulipwa posho anaposafiri kikazi kwani anapokuwa safarini mshahara wake upo palepale. Posho hizi hizi zinawafanya watumishi wa umma ambao ni mabosi kupora hata safari ambazo hawastahili kwenda wao. Napendekeza safari zote za nje na ndani ya nje ziwe bila malipo na badala yake serikali ilipie gharama za malazi na chakula kwa watumishi wake.

Hili linawezekana KABISA ninafanya kazi kwenye kampuni moja ya kimataifa tangu mwaka 1999 na huwa nasafiri sana nje ya nchi lakini sijawahi kulipwa hata senti moja kama posho ya safari. Niliwahi kuwachomekea hiyo hoja wakati fulani na jibu lilikuwa hivi *Man are yuo crazy! everything is covered in your salary* kama kungekuwa hakuna posho za safari za nje hata idadi ya watu wanaokuwa kwenye misafara ya raisi nje ya nchi ingepungua sana. Nawaapia kwamba kuna watu wanahonga mamilioni ili majina yao yawepo kwenye hii misafara kwa ajili ya posho tuu na wanapokuwa saferini kazi zao zinalala.Naomba kuwasilisha.

Ni kweli mkuu lakini kwa serekali gani? Bila kuiondoa CCM ili tuanze upya hii itakuwa ndoto. Angalia Zambia wenzetu wameanza kuangalia mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi na ufisadi serekalini, lakini ni baada ya chama mbadala kuingia shime shime wa tz!
 
Tanzania tunakazi sana. kuna haja ya mishahara ya mashirika ya serikali iwekewe mfumo maalum, haifai watumishi wa serikali moja wapishane mishahara kwa kiasi kikubwa namna hii
 
Jadili hoja hakuna sababu ya kumshambulia Kafulila. We Rajeo unaonaje juu ya tofauti za mishahara ya watumishi wa umma bila kufuata uwiano wa utendaji na uwajibikaji wao katika utumishi?
Tukumbuke kuwa mishara inayojadiliwa hapa ni mishara ya taasi za serikali/agencies. Ukitaka kuziangalia, hizi taasisi/mashirika yameanzishwa kisheria kwa ajili ya kuregulate masuala fulani either fedha, hifadhi za jamii, miindombinu, mawasiliano, biashara, afya nk. Hawa wanafanya kazi independently na central/local government. Hawa ni kama semi-government, wanajiamulia mambo yao wenyewe, including mishahara.
Sioni kama haya mashirika yanatakiwa yalaumiwe kwa kuwa na kiwango kikubwa cha mishahara cuz ni kutokana na majukumu na dhamana waliyoibeba. Ndani ya hayo mashirika kuna madaktari, waalimu, wahandisi, wahasibu na watu wa kila professional!
Chamuhumu hapa ni kuangalia serikali itainua vipi mishahara ya watumishi wake wa Central n Local government ireflect current state ya economy na mfumuko wa bei uliopo!
 
Good boy Kafulila angalau kwa kuthubutu kutujulisha mishahara na posho za hawa wakubwa;

1.Gavana wa benki kuu tsh.20m/-
2.Mkurugenzi mkuu NSSF tsh.18m/-
3.Junior Officer TRA & BOT tsh.7m/-
4.Mbunge tsh.1.8m/-

Pinda alitueleza mishahara ya hawa wafuatao;
5. Daktari tsh.900,000.00
6.Mhandisi tsh.600,000.00
7.Mhasibu tsh.368,000.00


Nami naongezea;
8.Mkurugenzi mkuu NHC tsh.20m/-

Hii nchi inaliwa na watu wachache sana, as if wao tu ndio watanzania!
kwa mtindo huu naunga mkono mgomo wa madaktari mpaka huu mfupo wa posho na mishahara uangaliwe upya-- sasa hapa namwelewa Job Ndugai kusema akitaja mishahara na marupurupu ya baadhi ya watumishi wa serikali na idara zake wengi mtazimia -- kweli mi dk tano zijazo nazimia.
 
Kafulila%284%29.jpg


Kafulila mbunge wa Kigoma Kusini

Naye mbunge machachari wa Kigoma Kusini (NCCR), David Kafulila, ambaye yuko kwenye mzozo na chama chake kilichomfukuza uanachama, alisema kinachosumbua kwa sasa ni kukosekana kwa mfumo wenye usawa wa ulipaji mishahara na posho ndani ya serikali.

Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.

“Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000,” alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.

Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.

IPP Media

Hili ndilo suala linalotaka muafaka wa kitaifa.
 
Complaining parliamentarians, elected by wailing citizens led by a corrupt government which manages an extremely rich country that is inhabited by extremely sick, poor and helpless people. PARADOX.
 
Back
Top Bottom