Kafulila abwagwa, Mahakama Kuu yampa ushindi Hasna Mwilima ubunge Kigoma Kusini

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
593
1,712
Habari wakuu,

Aliyekuwa mbunge wa Kigoma kusini, David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima.

Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.

Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Hasna) uliongozwa na wakili Kennedy Fungamtama pamoja na Mawakili wa Serikali upande wa mwanasheria mkuu wa Serikali.
 
Amman iwe kwenu.

Mahakama imempa ushindi Husna Mwilima leo tarehe 16.5.2016.Hivyo Kafulila atalazimika kusubiri hadi mwaka 2020.

Nawasilisha.
 
Hii nchi inaendeshwa kibabe sana kwa sasa lazima tujiandae kisaikolojia maana kuna mambo mengi yanafanyika nje ya sheria za kiutawala.
 
Amman iwe kwenu.

Mahakama imempa ushindi Husna Mwilima leo tarehe 16.5.2016.Hivyo Kafulila atalazimika kusubiri hadi mwaka 2020.

Nawasilisha.
kwani uliambiwa mahakama kuu ndiko ni mwisho wa kufungua shauli,,,,,,,, kwani ni mara ngapi majaji wa mahakama kuu wamekuwa wakitoa maamuzi yasio sahihi na baadae pakaonekana walikosea kwa sababu mbalimbali inaweza kuwa either makusudi au kwa kuhongwaa
 
Back
Top Bottom