Kadiri ninavyokutana na watu wenye tabia kama zangu, ndio nazidi kuwasamehe niliodhani wananichukia

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,088
nilikua ni mtu wa matani mengi, hata jambo la serious mimi nilikua naleta utani, nilikua na tabia ya sura mbili, nikiwa nyumbani ni mwema nikiwa mtaani wanavunjia adabu watu, nilikua na vitabia ambavyo vinakera ingawa mimi sikuona hili, nilidhani naonewa.

1. Tukio la kwanza

Siku moja nikiwa sehem fulani nilijipaka gundi ya maji nikidhani mafuta, jamaa mmoja aliposikia akasema "ndio vizuri mana anasifa sana huyu" jambo lile liliniuma nikiamini kua jamaa hanipendi ananichukia.

2. Tukio la pili
Nilienda ugenini, mmoja wa wenyeji akawa ananionesha sehemu fulani, alipokua ananionesha, nilifanya utani ila yule mwenyeji hajasema, nilikuja kusikia baadae na mtu mwengine kua alikasirika nilivyojibu, pia niliona kama yule mwenyeji hanipendi coz amekasirika kwa jambo dogo.

Leo hii nimekua nakutana na watu mbalimbali ambao wengine wanatabia kama zangu (nyingi nimeziacha na naendelea kuziacha) ndio naelewa, kitu hiki kimenifanya niwasamehe wote niliodhani walikua wananichukia, tabia zangu zilikua zinakera coz hata mimi nikikutana nazo zinanikera sana.
 
Tabia kama ngozi ya mwili huwezi kuiacha,tupo wengi Mkuu mwenyewe ni MTU wa matani sana pia kwenye majibu ndio utachoka.
Huwa najitahidi kujibu kiungwana lakini najikuta nimerudia hali yangu.
 
Kuna tofauti kati ya utani na misifa we inaonekana una misifa ya kijinga😂😂
 
Utakuwa mwanachadema wewe si bure

USSR
 
Tabia kama ngozi ya mwili huwezi kuiacha,tupo wengi Mkuu mwenyewe ni MTU wa matani sana pia kwenye majibu ndio utachoka.
Huwa najitahidi kujibu kiungwana lakini najikuta nimerudia hali yangu.
Thibitisha kwa kutoa jibu hapa nilivyokuquote
 
Back
Top Bottom