Kadinali pengo na askofu kakobe: Mmetupa mwanga na njia (thanks) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kadinali pengo na askofu kakobe: Mmetupa mwanga na njia (thanks)

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Gobret, Sep 28, 2010.

 1. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kiongozi wa dini anayetambua nafasi yake hawezi kusema au kushawishi kumchagua kiongozi fulani. Ndicho walichofanya viongozi wetu hawa wawili wa imani. Askofu Kakobe ameonyesha msimamo gani tuwe nao ktk kuchagua. Amesema tuangalie zaidi uwezo wa mtu mhusikana ktk kuleta maendeleo kwa watu husika hata kama ana madhaifu mengine. Kwa kuzingatia kuwa Hakuna mtu mkamilifu. Kadinali Pengo hivyo pia amewaasa watu wenye mapenzi mema kwa TZ kuchagua kiongozi bora ambaye hahongi watu kwa kanga etc, tunajua wanaotoa rushwa ZA NAMNA HII ni CCM. TUWANYIMA CCM KURA. WAKOSE KURA KAMA WALIVYOKOSA TANU. WATANZANIA TUJALI ZAIDI TZ YETU. KULIKO KITU KINGINE. KAMA NIMACHAFUKO NANI ATAOKOKA. HIVYO KILA MWENYE MAPENZI MEMA NA TZ ATAWANYIMA HAWA CCM. CCM WAMEOZA, WANANUKA RUSHWA. HAWANA NIA NJEMA NA NCHI YETU. TUNATESEKA WAO WANASHEREKEA NA FAMILIA ZAO. CHUKUA TAHADHARI MAPEMA. TUWAWEKE PEMBENI WAGEUKE OMBAOMBA. KILA LA KHERI WATZ. KTK MAAMUZI YENU.
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  tupatie hotuba zao
   
 3. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nimeisoma hotuba ya Pengo nimeipenda sana ni mwongozo mzuri sana
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Na Peter Mwenda

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amewataka wakristo kufuata dhamira ya Mungu ya kuchagua viongozi ambao hawawarubuni kwa khanga, bia na fulana.

  Akihutubia waumini katika ibada ya kuombea amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu iliyofanyika katika Kijiji cha Hija, Parokia ya Pugu juzi, Kardinali Pengo alisema wakristo wakatoliki wajue kwamba kura zao zina thamani kubwa kwa jamii na mbele ya Mungu.

  "Kama mngejua thamani ya kura yako kwa jamii na mbele ya Mungu huwezi kupokea zawadi za khanga na bia kwa ajili ya kumpigia mtu asiyefaa kupewa kazi ya kuongoza," alisema Kadinali Pengo.

  Alisema Mwenyezi Mungu anafanya kazi kupitia dhamira ya kila mwanadamu, hategemei ushabiki wa vyama wala kumchagua kiongozi asiye na utashi ambaye anatoa rushwa ili apate uongozi.

  "Si kuambiwa na mwenyekiti wa jumuiya, kasekista (Mwalimu wa dini), kadinali au padre kuwa mchague fulani, hakuna atakayesimama kwa dhamira yako, anayefaa ni yule anayejiepusha na matendo ya rushwa," alisema Kadinali.

  Alisema kumetokea minong'ono hivi karibuni kuwa Kanisa Katoliki limeteua viongozi wa kupigiwa kura katika ngazi ya juu. "Huo si msimamo wa Kanisa Katoloki."

  Alisema akiwa kiongozi wa kanisa hilo anaweka bayana msimamo wa Wakatoliki kuwa hawafungamani na itikadi za kichama, kisiasa au kabila.

  "Kanisa Katoliki lingefanya hivyo likawa na watu wake au kusema fulani ni chaguo la Mungu ni balaa linaloweza kuleta machafuko na uvunjifu wa amani," alisema Kardinali Pengo.

  Alisema uchaguzi wa kibinadamu ni chanzo cha mfarakano lakini wakristo ambao wana utashi wa Mungu wasimchague kiongozi wanayemjua kuwa ni mwizi na mla rushwa ambaye anatumia kushawishi ili achaguliwe.

  "Tuchukue na kuamini hilo kuwa ni ukweli wa Kanisa Katoliki halina mtu kuwa huyu awe rais, mbunge au diwani. Haliwezi likasimama likasema fulani awe hivi," alisema Kadinali Pengo.

  Alisema Wakristo nchini kote wapige kura kwa dhamira ya kumuogopa Mungu kuwa siku ya mwisho watasimama mbele yake na kusema madhambi yao.

  Katika ibada hiyo ambayo Kadinali Pengo alisaidiwa na mapadri 15 kutoka parokia mbalimbali za Jimbo Kuu la Dar es Salaam alisema kutafuta madaraka kwa kutumia nguvu au ushawishi ili kuhalalisha madaraka si njia ya kuleta amani bali kuashiria machafuko ambayo kanisa inapinga vikali.

  Mkurugenzi wa Haki na Amani wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Alister Makubi aliwaasa waumini wa kanisa hilo nchini wasichoke kusali kuombea amani wakati wote wa uchaguzi.
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Umeelewa lakini
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Tusubiri tuone sijui kabla au baada ya uchaguzi
   
 8. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  kila mtu na amchague ampendaye na kwa vigezo vyake mwenyewe..mfano mie mpaka sahivi sioni anayefaa maana hakuna hata mmoja aliyeniahidi maisha-bora kwa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa hasa hizi biere
   
 9. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata waislam hawapendi kabisa UFISADI na pia wanapenda mabadiliko. Uislam unafundisha pia maadili safi, sio kudanganyadanganya watu miaka yote.
   
 10. F

  FM JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zaidi ya hayo Pengo aseme nini. Ahsante Kadinali
   
Loading...