Kadi yangu ya Bima kutumika zaidi ya mara moja

kaburu mdogo

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
567
400
Jana nilienda hospitali moja binafsi kupata matibabu kwa kutumia kadi yangu ya Bima. Wakati huo nilipata sms kuwa kadi yangu imetumika na kama sijui nitoe taarifa.

Leo muda huu napata tena taarifa kadi yangu inatumika kwenye hospitali ile ile niliyoenda kupata matibabu wakati mimi nipo nyumbani. Baada ya kuona sms hiyo niliwapiga watu wa Bima kuwapa taarifa juu ya hali iliyojitokeza na kuniambia watalifanyia kazi.

Swali langu ni je, kuna unuhimu wowote wa kwenda kwenye hiyo hospitali na kutoa taarifa/ malalamiko au niawaachie Bima wapambane nao?
 
Muhimu shukuru pesa unayolimwa,kuna mtu imemsaidia huko.

Landa kama wanadanganya walipwe zaidi kamisheni.
 
Nakushauri uende kwenye hospitali husika ukatoe taarifa hiyo..Anzia receiption.. Maana inawezekana wao wamedanganya ili wajipatie fedha bila kutoa huduma husika... Na usisahau fungu la OUTPATIENT linateketea bila wewe kuhusika..!!! Kuna siku watakwambia ballance imekata na huku baadha ya transactions huzijui..
 
Shukrani, kesho jioni nitapita hapo
 
Back
Top Bottom