Kadi nyekundu kutolewa kwa wachezaji watakaokohoa makusudi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Wachezaji au maafisa wa mechi watakaokohoa kwa makusudi wanaweza kupewa kadi nyekundu, Bodi ya Kimataifa ya Mashirikisho ya Soka Duniani (IFAB) imetahadharisha.

Ifab, yenye maskani yake Zurich, Uswizi ndicho chombo kiku cha kutengeneza kanuni za uendeshaji wa kandanda ulimwenguni.

Kwa mujibu wa bodi hiyo, kujikohoza ni kosa linaloweza kuwa ndani ya makosa ya "kutumia maudhi, matusi au lugha au ishara za matusi."

Imeongeza kuwa: "Kama ilivyo katika makosa mengine, mwamuzi atatakiwa kuchukua uamuzi juu ya ukweli na lengo halisi la tendo hilo."

Muongozo huo umetolewa huku dunia ikikabiliwa na janga mlipuko wa virusi vya corona.

"Kama ni wazi mtu amekohoa kwa bahati mbaya muamuzi hatachukua hatua na wala kama mchezaji ‘atakohoa’ akiwa mbali na mwenzake ," Ifab iliongeza.

Chama cha kandanda cha England (FA) pia kimetoa muongozo kwa ajili ya soka inayochezwa na timu za madaraja ya chini ambao utatekelezwa mara moja.

Katika michuano ya Primia, hakuna muongozo wowote rasmi uliotolewa na itabaki kwa waamuzi kutumia busara yao kutoa adhabu kwa mchezaji.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom