Kadi feki za CCM, kura ya maoni na TAKUKURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kadi feki za CCM, kura ya maoni na TAKUKURU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jul 3, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikiripoti habari ya kuwepo kwa kadi feki ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM. Nimekuwa nikizitafakari habari hizi bila kuelewa ni wapi hasa tunakoelekea na Taifa litarajie kupata viongozi wa aina gani ikizingatiwa kuwa bado CCM ina nguvu katika siasa za Tanzania.

  Imeripotiwa sehemu mbalimbali nchini kuwa baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakikamatwa na kadi feki huku baadhi yao wakikiri kupewa maelekezo na viongozi (wamewataja) kugawa hizo kadi kwa malengo ya kumsaidia mgombea fulani kushinda wakati wa kura za maoni.

  Swali langu linakuja, kwanini hali hii imeachwa iendelee kipindi hiki bila ya chama kukemea vitendo hivyo kwa kisingizio cha kuiachia Takukuru, hawaoni kuwa vitendo hivyo vinakipaka chama matope.

  Binafsi naona kuiachia Takukuru kushughulikia mambo ya ndani ya chama bila chama chenyewe kuonyesha kujali ni kupoteza muda wa Takukuru. Endapo Takukuru itakafanikiwa kuzipata hizo kadi na kujiridhisha kuwa ni feki baadaye chama kikazitambua kuwa ni kadi halali Takukuru itakuwa upande gani.

  Tutegemee nini wakati na baada ya kura ya maoni, na endapo mambo yatakuwa mabaya zaidi mfano kwa baadhi ya wagombea kujitoa nani wa kulaumiwa.
  Heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta. Nawasilisha hoja.
   
 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Luteni,
  Hata mimi nimekuwa nikisoma taarifa hizo kwa muda sasa. Labda nisaidie kuelezea kwa jinsi ninavyojua mimi utaratibu ulivyo.

  Kadi yoyote kwa mwanachama mpya kuelekea hiki kipindi cha uchaguzi inatakiwa ifuate mlolongo ufuatao:

  1. Mwanachama anaenda kulipa kwa katibu wa tawi lake.
  2. Katibu wa tawi anaenda kulipa kwa katibu kata
  3. Katibu kata anaenda kulipa kwa katibu wa wilaya
  4. Katibu wa wilaya anaenda kulipa kwa katibu wa mkoa.
  5. Katibu wa mkoa ndiye anafuata kadi zote za mkoa kule makao makuu CCM.

  Hata wakati wa kuhakiki daftari la wanachama, utaratibu huo ndio utafuata. Kadi ambayo namba yake haiko kwenye mlolongo huo hapo juu ni batili na haiwezi kusajiliwa.

  Kadi nyingi feki ambazo baadhi ya watu walitaka kuziingiza, zimekwama kwa sababu hizo hapo juu. Pia kuna kadi ambazo sio fake lakini zilitengwa kwa ajili ya wilaya au mkoa tofauti nazo baadhi zimekamatwa na baadhi ya wahusika kuchukuliwa hatua kwasababu hiyo hiyo.

  Sijui kwa sehemu zingine lakini kwa uzoefu wangu na habari nilizo nazo mimi kuhusu kule kwetu Kyela, suala la kadi feki litakuwa dogo sana na naamini utaratibu huu ambao CCM wameweka ni mzuri kukabiliana na wale waliotaka kuingiza wanachama kinyemela.

  Mpaka sasa kule Kyela kadi ni chache sana na wengi wa waliotaka kuwa wanachama ili wapige kura hawatafanikiwa kupata kadi.
   
 3. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Siku zote vita ya panzi ni furaha ya kunguru, waacheni wavuruganeeeeeeeeeeeeeeeeee halafu watakatika na baada ya awamu hiyo ndipo itakapofuata awamu iliyo tamu zaidi ya jino kwa jino kwani watakuwa wanajuana amari zao kibindoni, Hivi nyie watu hamuoni kuwa jahazi lakaribia Pwani?
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pamoja na utaratibu huo kibaya zaidi wanaoukiuka ni viongozi waliouweka
  Wasiwasi wangu ni kuja kupata viongozi wasio na uwezo matokeo yake itakuwa ndoto kutekeleza ahadi na kauli mbiu ya Maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Ndio sikatai kuna viongozi na wabunge wenye uwezo na watu wanahoji kama mbunge wao ameweza kujitolea pesa yake kuwajengea kisima na shule nk kuna ubaya gani, mfano Mkono anavyojenga shule kwa pesa yake. Nafikiri hatuhitaji kiongozi wa aina hiyo atafanya hivyo kwa miaka mingapi je akimaliza muda wake tunauhakika gani atakayekuja atakuwa na uwezo kipesa kama wake.

  Tunahitaji kiongozi mbunifu aliye na upeo, uelewa wa mambo, anayejiamini mwenye kujenga hoja hata bungeni na ikasikilizwa si kiongozi anayeingia kwa mbinu za kununua na kulipia kadi feki. Kwangu mimi mtu anayetumia pesa kununua uongozi hatufai anategemea pesa atakayotumia kurudi kwa muda mfupi huyo ni mfanyabiashara si kiongozi.

  Tatizo jingine ambalo CCM kama chama hawalioni au labda kinafumbia macho ni kujitengenezea mamluki wengi watakaokiyumbisha chama wakati wa kura za maoni, maana haitakuwa rahisi kuwafanya watu wakubali mgombea wasiyemtarajia, kuna mifano mingi tuliona wakati wa uchaguzi mdogo wa Busanda Geita ilivyokuwa shida kwa CCM kumuuza mtu ambaye hakuwa chaguo la kwanza la wanajimbo.

  Chama kama chama kinatakiwa ku intervene mapema hali hii kuliko kuiachia Takukuru ambayo wakati inamaliza kufanya uchunguzi labda tayari mambo yatakuwa yameshaharibika.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Luteni,

  Kila sehemu kuna malalamiko lakini ukifuatilia unagundua kwa sehemu kubwa ni majungu tu.

  Nina wasiwasi sana kama hiyo habari ya Songea ina ukweli wowote zaidi ya kuchafuana. UWT watagawa vipi hizo kadi? Wakigawana basi wakati wa kuhakiki zitajulikana tu.

  Sisemi huo utaratibu ni kinga kwa asilimia 100 lakini binafsi niko happy nao. Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi sana na suala la kadi na niliwaambia hata CCM wilaya. Lakini baada ya kuja na utaratibu huu wasiwasi wangu umepungua kwa kiasi kikubwa.

  Baada ya kufunga zoezi la kujiandikisha tutaenda kuhakikisha kwamba kadi zote zimetolewa kwa utaratibu uliotolewa.

  Utaratibu wa sasa ni mzuri sana ukilinganisha na wa huko nyuma ambao mwenye pesa alikuwa na uwezo wa kuwanunua wajumbe 300 na kupata ushindi bila matatizo. Kwasasa hata ununulie watu 30,000 kadi, una uhakika gani hao watu wanakuunga mkono? Kweli watakuunga mkono kwasababu umewanunulia kadi ya shilingi 300?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jul 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nina wasiwasi mkubwa na utaratibu wa ugawaji kadi za chama hiki cha CCM... Leo ktk pita pita yangu blog ya Bibie Jay Dee nimeona mbunge wa Singida Mohammed Dewji akigawa kadi za uanachama wapya wa CCM jimboni kwake...
  MD ni Mbunge, sio kiongozi wa chama kugawa kadi za chama hali yeye anategemea kupitishwa jina lake na wanachama hao hao anaowagawia kadi..Hii kweli inaingia akilini?! Hivi kweli huu ndio utaratibu unaotakiwa kufanyika au?..
  Jamani huko CCM kuna mambo kweli..
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,948
  Trophy Points: 280
  Mimi nimeziona picha kwa Michuzi. Halafu kilichonishangaza sana ni kwamba yeye ndiye aliyewaapisha hao wanachama wapya. Nakumbuka miaka ya nyuma kabla ya kuwa mwanachama wa CCM ilibidi uhudhurie darasa ili kujua kanuni mbali mbali za chama kabla ya kukubaliwa kuwa mwanachama. Siku hizi bora liende tu kadi zinagawiwa kama njugu! ama kweli CCM ni nambari one.

   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mkandara,

  Sina sababu ya kutetea utaratibu huu wa kufungua mashina maana mimi mwenyewe naupinga na in fact hata mimi kuna vijana wengi tu walishaomba nifungue mashina yao na kuwakabidhi kadi, mimi nilikataa. Sababu ya kupinga ni kwamba mashina kama hayo mengi ni vijiwe vya watu wasio na kazi ya kufanya. Wanafungua mashina kama njia ya kutafuta ulaji. Kule kwetu Kyela kipindi hiki mashina mengi tu yanafunguliwa na waheshimiwa. Kuna mengine hata chama hakiyatambui lakini ndio hivyo yanafunguliwa.

  Nilichowaambia, nitakuwa tayari kushirikiana na vijana wanapoanzisha miradi yao ya maendeleo lakini sio huu uanzishwaji wa vijiwe ambavyo wanavitumia kucheza bao na kulewa asubuhi mpaka jioni.

  Lakini kwa CCM, viongozi wengi wanaona hiyo ndio njia ya kupata umaarufu kwa kutumia vijana wasio na mwelekeo. Wakipita hapo wanawaachia sh. 10,000 na kisha vijana wanapiga makofi na si ajabu hata kusukuma gari la mheshimiwa.

  Sasa tukija kwenye kadi, sio kweli kwamba huyo mheshimiwa ndio anatoka na kadi huko na kuja kuwakabidhi. Wanakuwa wamenunua kadi kwa utaratibu wa kawaida na mheshimiwa anawakabidhi tu siku ya mwisho. Hata ukiangalia vizuri picha ya MO ni kwamba alikagua kadi za hao wanachama wapya na hawasemi alikuwa anagawa.

  All in all utaratibu wa sasa wa CCM kupata wanachama wake haufai na labda ni matokeo ya siasa za vyama vingi maana ukisema watu wasome kama ilivyokuwa zamani hupati watu tena. Muundo wa zamani ulikuwa unafaa zaidi kwasababu kadi walikuwa wanapewa watu waliokuwa wanakubaliana na imani za chama.

  Vyama karibu vyote vya TZ vina wanachama wachache sana ambao wako pale kwa itikadi na ndio maana ni rahisi kwa wengi wa wanachama kuhama hama kila mara. Huenda itakuwa muhimu ikifika mahali, vyama viwe na wanachama wachache sana, wale wanaoamini katika itikadi za chama. Wengine wote wawe wapenzi tu ambao wakivutiwa na sera za chama basi wanakiunga mkono, wakichukizwa wanaunga mkono chama kingine. Mashindano ya kuwa na wanachama wengi hayavisaidii kabisa hivi vyama maana wanapata mamluki wengi tu ambao wakikosa walichokifuata basi wanahamia kwingine.

  Kwa TZ kwenye ulaji, kila utaratibu utakaokuja nao, kuna wajanja watatumia mbinu zao kujaribu kuuvuruga. Binafsi naamini utaratibu wa sasa wa CCM kuchagua wagombea wao una faida nyingi kuliko hasara.
   
 9. K

  Keil JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mtanzania,

  CCM ina mafia wengi sana na wakiamua kufanya umafia wanafuata utaratibu sahihi uliowekwa. Niliona mahali umefafanua mfumo wa utoaji kadi kwa wanachama wapya. Nina hakika hao wanaogawa kadi, hakuna kadi fake na zote ni genuine kwa kuwa wanafuata utaratibu.

  Je, una uhakika kwamba kadi anazogawa MO hajazilipia yeye mwenyewe na anachokifanya ni kuwagawia tu hao vijana ama wanachama wapya? Kwani kadi mpya ya CCM ni bei gani? Hivi mbunge mtarajiwa hawezi kupita kijiweni na kuwaomba vijana wapeleke majina kwenye shina then tawi na baadaye yaende wilayani na mkoani mpaka yafike kwa Makamba?

  Hamjiulizi kwanini sasa hivi biashara ya kugawa kadi mpya imeshika kasi? Nina uhakika kwa 100% kwamba hizo kadi mpya zinazogawiwa, hakuna fake, zote ni genuine na wamefuata utaratibu kuziomba ingawa aliyelipia hizo kadi ni mbunge mtarajiwa ambaye anategemea kuwatumia hao vijana kwenye kura za maoni.

  Tena huo utaratibu wa kufungua mashina ya wakereketwa ndio balaa zaidi kwa kuwa vijana wanapokuomba ufungue shina lao wanategemea uwaambie wapeleke majina yako kwenye shina/tawi ili uwalipie kadi mpya kwa ajili ya nominations/primaries. On to of hizo kadi pia uwaachie na shilingi 10,000 wakalewe na kuvuta bangi, halafu wanakaa mkao wa kusubiri mavuno ya primaries.

  Kuna mahali nimesoma wananchi wanaambiwa kwamba kama unahitaji kadi just send an sms then unasema jina lako na unaishi eneo gani, then utapewa kadi na shilingi 2,000 juu. Sasa huo kama siyo uhuni ni nini? Vijana wanazichangamkia kwa kuwa wanajua kwamba hizo kadi ni mtaji ikifika kwenye kura za maoni sawa na ilivyo shahada ya kupigia kura ikifika mwezi Novemba.
   
 10. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kadi feki zaivuruga CCM

  [​IMG][​IMG]
  Saturday, 03 July 2010 08:30

  Mchezo mchafu wa kugawa kadi feki ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baaadhi ya watendaji na viongozi kuwapigia debe baadhi ya wagombea ubunge na udiwani, vimezua mtafaruku ndani ya chama hicho na kusababisha kusimamishana uongozi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuingilia kati.
  Baadhi ya watendaji wa CCM mkoani Arusha, wamekuja na mbinu ‘nyeusi kama kaniki' ya kuwagawia bure wananchi kadi za uanachama ili wawapigie kura za ushindi wagombea fulani katika kura za maoni ndani ya chama hicho.
  Takribani watu 60 wilayani Arumeru wameshanufaika na mradi huo mpya wa ‘kadi kwa kura' kwa nia ya kuwawezesha baadhi ya wagombea katika ngazi ya udiwani na ubunge katika kura za maoni, zinazotarajiwa kuanza Agosti Mosi, mwaka huu.
  Kufuatia hali hiyo, Takukuru mkoani hapa, inaendelea na uchunguzi ambapo watu kadhaa waliopewa kadi hizo wamehojiwa na wengine wanaendelea kuhojiwa.
  Tukio la ugawaji wa kadi hizo limetokea katika kijiji cha Engerora, Kata ya Kisongo, pembezoni mwa barabara kuu ya Arusha-Dodoma. Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Joseph John, aliliambia Nipashe kuwa zoezi la ugawaji wa kadi kwa wanakijiji hao lilianza Mei 30, mwaka huu, ambalo limekuwa likifanywa na kiongozi mmoja wa CCM kijijini hapo. Mmoja wa watendaji wa CCM kijijini hapo, (jina tunalo), amekuwa akituhumiwa kugawa kadi hizo bure huku akiwaelekeza wawapigie kura wagombea wa udiwani na ubunge kwa Jimbo la Arumeru Magharibi.
  Mtumishi huyo kwa siku nzima jana hakupatikana kwenye simu yake ya kiganjani kuzungumzia tuhuma hizo.
  Awali, takribani mabalozi 10 wa CCM wa nyumba kumi, walikwenda kwa kiongozi huyo kuomba wapewe kadi kwa ajili ya watu waliokuwa wakitaka kupewa uanachama, lakini kiongozi huyo alikuwa akiwajibu kwamba kadi zimeisha.
  Lakini Joseph alisema kuwa walishangazwa kuona baadaye kadi hizo zikitolewa kinyemela kwa baadhi ya watu na kwa uangalifu mkubwa huku wakipewa maelekezo ya kumpigia kura mgombea fulani wa nafasi ya udiwani na mgombea mwingine wa kiti cha ubunge.
  Wanaowania kuteuliwa kuwa wagombea wa kiti cha udiwani wametajwa kuwa ni Saitabau Namoyo, Simon Ole Saning'o na wengine wawili ambao majina yao hayakupatikana mara moja.
  Kwa upande wa ubunge, wanaowania kuteuliwa ni mbunge wa sasa, Elisa Mollel, Goodluck Ole Medeye na mmoja aliyetajwa kwa jina la Ngoseki.
  Katika kufuatilia sakata hilo, maafisa wa Takukuru waliokuwa kwenye gari aina ya Toyota Hilux Double Cabin, lenye namba za usajili T 874 BAV, waliwasili katika baa moja iliyopo Kisongo, ambako baadhi ya watu waliopewa kadi hizo walijitokeza kutoa maelezo yao kwa maofisa hao.
  Wanachama watatu walikubali kuonyesha kadi walizopewa ambapo wawili kati yao ni mtu na mke wake.
  Wanachama hao kadi zao zikiwa na namba AD-3779471 na AD-3779490 pamoja na mwenye kadi namba AD-3779460.
  Kadi hizo zilionyesha kuwa zimeuzwa kwa Sh. 1,500 kila moja na ziliuzwa kati ya Juni 23 hadi 29, 2010.
  Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arumeru, Lightness Mwiteni, alisema jana kuwa hakuwa na taarifa iwapo Takukuru walikwenda kijijini huko kuchunguza sakata hilo. Kuhusu uhalali wa kadi hizo, Mwiteni alisema anahitaji muda ili kujiridhisha kama ni kadi halali au feki.
  "Kwa sasa ninahudhuria mkutano hapa ofisi ya CCM mkoa, sipo ofisini na baadaye nitakuwa ninahudhuria mkutano mwingine wa kamati ya siasa, kama ningekuwa ofisini ningeweza kufanya uhakiki wa kadi ili kujiridhisha kama ni feki au la.
  Kuhusu Takukuru kuchunguza sakata hilo, Katibu huyo alisema hana taarifa zozote. Naye Kamanda wa Takukuru mkoani hapa, Ayub Akida, alisema hajapata taarifa kwa kuwa suala hilo lipo wilayani Arumeru.
  "Bado sijapata taarifa. Unajua Kisongo ipo Wilaya ya Arumeru na mimi hadi sasa suala hilo halijafika ofisini kwangu," alisema Akida. Katika hatua nyingine, CCM wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma kimewasimamisha kazi makatibu wa matawi watatu, katibu mwenezi mmoja na Mwenyekiti wa Kata ya Liuli, Samuel Mawanja, kwa tuhuma za kuhusika kumfanyia kampeni kada mmoja aliyetangaza kugombea ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi.
  Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Anastasia Amasi, aliwataja wengine waliosimamishwa kuwa ni Whero Whero Katibu wa tawi la Kondowe katika Kata ya Liuli, Hugo Matifali Katibu wa tawi la Liuli, Isaac Hanganuka ambaye ni Katibu wa tawi la Puulu na Samson Mbena, Katibu Mwenezi wa tawi la Nkarachi.
  Amasi alisema kusimamishwa kwa watendaji na viongozi hao kunatokana na kuwepo malalamiko mengi ya wanachama kuwa wamekuwa wakijihusisha kumfanyia kampeni mmoja wa wagombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi kabla ya wakati na kugawa kadi za CCM ambazo zimeingizwa wilayani humo kinyemela.
  Alifafanua kuwa baada yakuhojiwa ilibainika kuwa walikiuka kanuni zilizowekwa na CCM kwa viongozi kutojihusisha kuwafanyia kampeni wagombea kabla ya wakati wachukuliwe hatua kwa kuwa tabia hiyo imeanza kuonekana kuwa ni tatizo.
  Amasi amewataka viongozi wa chama hicho kutojihusisha kuwafanyia kampeni wagombea kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu na kanuni.
  Amasi aliongeza kuwa kiongozi yeyote atakayebainika anafanya kinyume cha taratibu atachukuliwa hatua kama zilizochukuliwa dhidi ya waliosimamishwa.
  Awali, wanachama wa CCM katika kata ya Liuli waliulalamikia uongozi wa wilaya kuwa kuna baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakipita nyumba hadi nyumba kushawishi wanachama kuwa wanapaswa kumchagua mmoja wa wanachama wanaotaka kugombea ubunge kwenye jimbo hilo, hatua ambayo ilizua mzozo na kusababisha kuwepo makundi ndani ya CCM.
  CHANZO NIPASHE

  Takukuru wanasa vyerehani 15 ofisi za CCM

  [​IMG][​IMG]
  Saturday, 03 July 2010 08:38

  VYEREHANI 15 vimekamatwa katika ofisi ya CCM wilayani Shinyanga vilivyotarajiwa kugawiwa wanawake wa chama hicho ikiwa ni wiki mbili baada ya mtangaza nia mmoja wilayani Maswa kukamatwa na Takukuru akigawa pikipiki tano kwa wakazi wa eneo la Malampaka.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga, Leonalda Ngaiza alisema vyerehani hivyo vimekamatwa kutokana na malalamiko ya kuwepo kwake ofisini humo suala lililoilazimu ofisi yake kufuatilia na hatimaye kuvikuta katika ofisi ya CCM wilaya vikiwa katika marekebisho ya kuviunganisha.

  Aidha, alisema kuwa tayari walishamhoji Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni mwenyekii UWT na pia diwani wa kata ya Kitangiri, Moshi Kanji pamoja na katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Mwasiti Rajabu.

  "Katika hatua ya awali tayari tumeshamhoji mwenyekiti wa UWT pamoja na katibu wake….lakini bado tunaendelea na uchunguzi ili kujua vimetoka wapi, kwenda kwa akina nani na pia vilikujaje," alisema Ngaiza.

  Aliongeza kuwa pia ofisi yake imepokea taarifa kutoka wilaya ya Bukombe kuwa kuna baadhi ya watu tayari wameshagawa vyerehani hivyo kuahidi kufuatilia kama waliofanya hivyo huko Bukombe kama ndiye huyo aliyetoa wilaya ya Shinyanga.

  "Pia huko wilayani tumepokea taarifa kuwa kuna watu wameshagawa vyerehani, ndio tunataka kujua kama ndio hawa hawa kwani huyu wa Shinyanga ni mmoja wa wawania ubunge wa viti maalum... lakini bado tutaendelea kuwahoji watu mbalimbali waliopo ndani ya mkoa na nje ya mkoa," alisema.

  Kamanda Ngaiza alisema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kutokana na uzito wa ushahidi kwani ni mapema sana kuzungumzia adhabu ya jambo hili.
  CHANZO MWANANCHI
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Jul 5, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hili ni tatizo kubwa sana. Mimi nimeletewa kadi ya CCM ikiwa na jina na details zangu zinazohitajika, na kuambiwa eti niihifadhi hadi muda muafaka utakapofika! CCM bwana!!!!!!
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Keil,

  Uko sahihi kabisa kwamba utaratibu wa sasa haumzuii kiongozi ambaye ameamua kufanya fouls kwa kufuata taratibu. Anaweza kwenda kwa wanachama na kuwapa pesa ili wakakate kadi kwenye matawi yao. Kadi kama hizo zitakuwa genuine kwa utaratibu wa sasa wa CCM. Pia anaweza akaongea na makatibu matawi ambao wanaweza kununua kadi kwa kisingizio cha kwamba ni wanachama wamelipia na baada ya hapo wakagawa kwa wale anaowataka mgombea.

  Hayo ndio mapungufu kwenye utaratibu wa sasa. Ila tu wilaya nyingi zina wanachama au wananchi wanaoweza kuwa wanachama mpaka kwenye 30,000. Kujaribu kuwahonga kwa kutumia kadi inaweza kuwa kujisumbua tu. Kadi ni shilingi 300 na sidhani hata ukimhonga huyo mwanachama hiyo kadi ya shilingi 300 basi atakuwa ni wako mpaka siku ya kupiga kura.

  Kuna jamaa aliwahi kunipa ushauri mimi pale mwanzoni kabisa kwamba jihadhari kabisa na kuwanunulia kadi wanachama maana hao hao ndio wanaweza kukumaliza kwa kutumia kadi zako hizo hizo. Na kwa yale ninayoyaona Kyela, kwamba vijana hao hao leo wako na mgombea huyu na kesho wanakuwa na mwingine; hata ukigawa kadi kuna uwezekano mkubwa kabisa wa kwamba zinaweza kuishia kwa watu ambao siku ya mwisho hawatakupigia kura.

  Ni kweli kwasasa wanachama wengi sana wanajiunga na CCM kama njia ya kujiandaa na mkao wa kula. Wanajua kwamba wakiwa na kadi basi waheshimiwa watawajali na wanaweza kuambulia hata pombe za kienyeji. Kule kwetu watu walioomba kadi wanafikia hata asilimia 300 ya wanachama halali kwa sasa. Inaelekea CCM ilikuwa na wanachama halali wachache sana. Kwa mfano kuna tawi ambalo lina wapiga kura zaidi ya 10,000; wanachama halali mpaka tarehe 30/05/2010 walikuwa 50 tu. Ila kilichonifurahisha mimi ni kwamba inaelekea ni ngumu sana kupata hizo kadi maana mpaka sasa kuna wanachama wengi sana wanasubiri pamoja na kununua hizo kadi kabla ya mwezi wa sita. Ndio maana hata CCM NEC wameamua kuongeza muda wa kuhakiki kadi mpaka 15/07/2010 kwasababu CCM makao makuu wanadaiwa kadi nyingi sana.

  Katika jamii iliyojaa rushwa, kila utaratibu utakaokuja nao kuna wajanja watauvunja. Labda kwa sasa huu utaratibu ni less evil kuliko taratibu zingine za nyuma. Lakini ni ukweli tupu kuna wajanja wachache watajinufaisha na utaratibu huu kama ambavyo kuna wengine pia watajifanya wajanja lakini wataishia kupigwa bao. Ngumu sana kujua intentions za wapiga kura.
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU iliundwa kutokana na shinikizo la mataifa ya nje. Kwa hiyo iko pale kama jina tu, na wala haina mpango wowote wa kushughulika na rushwa. Rushwa za kupokea Sh 1500 ndio zitakazokamatwa na kutangazwa sana lakini rushwa zile zenye athari kwa jamii hawashughuliki nazo hata siku moja. Ndiyo maana Chenge na wenzake wanapeta mpaka leo; na wamepewa viinua mgongo vyao bungeni.
   
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Keil na Mtanzania

  Nakubaliana na nyie kuwa mpango wa kuwatumia wanachama wote wakati wa primaries ni mzuri lakini una mapungufu yake. Kama alivyosema Keil inawezekana kadi hizi si fake ni geniune, ufeki wa kadi uko hasa kwenye upatikanaji wake haiwezekani mtu umekaa nyumbani au kwa kutuma email unaletewa kadi, hata kama mlipaji amefuata taratibu zote. Hapo katikati lazima kuna mianya fulani ya uchafu kufanyika.

  Keil ameuliza kwa nini biashara ya kugawa kadi imeshamili hasa kipindi hiki. Mimi nafikiri zamani kulikuwa hakuna haja ya kuwanunulia kadi wajumbe ambao walikuwa hawazidi 300 tofauti na sasa ambapo ili uteuliwe unatakiwa kuungwa mkono na idadi kubwa ya wanachama. Kwa hiyo mradi umehama toka kwa viongozi wa mashina na matawi kwenda kwa wanachama ndiyo maana utaona wagombea wengi wakihaha kugawa kadi mitaani kama njugu.

  Mtanzania, unaweza kufikiri kuhonga kadi ya sh. 300 ni kujisumbua lakini elewa kuwa 70% ya watanzania hufuata upepo wengi hawatambui athari ya kitendo hicho, tumeona wengi wakipewa kofia tu na wengine kupewa ubwabwa na kuna uwezekano mkubwa wa mtu huyo akawa ndiyo kanunuliwa hadi siku ya kupiga kura, maana wengi husema si anataka kura tu nitampa kwani itanipunguzia nini.
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, amelalamika hadharani kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusu kadi feki za uanachama zinazosambazwa na wabaya wake kisiasa kwa lengo la kumhujumu ashindwe katika kura za maoni.

  Wanachama wa chama tawala wanatarajia kupiga kura za maoni mwezi ujao kwa lengo la kuwateua wagombea ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

  Sendeka alitoa malalamiko hayo mwishoni mwa wiki kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ambaye pia ni Mjumbe wa NEC kwa tiketi ya Mkoa wa Kilimanjaro.

  Sendeka na Profesa Maghembe walikuwa miongoni mwa wananchi na viongozi waliohudhuria hafla ya kuzindua Shule ya Sekondari ya Emboreet, iliyopo wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara.

  Baada ya kupewa fursa fupi ya kuzungumza, Sendeka aliitumia nafasi hiyo kumuonyesha Profesa Maghembe kadi moja aliyodai kuwa ni feki na akasema hiyo ni moja tu ya kadi nyingi ambazo zimesambazwa na mafisadi wa demokrasia katika jimbo hilo.

  “Ukiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, naomba kukueleza kwamba hapa Simanjiro kwa wakati huu wamezuka mafisadi wa demokrasia, ambao hugawa kadi feki ili kuvuruga uchaguzi…bila shaka hata wewe katika jimbo lako kuna baadhi ambao wanataka kukuhujumu kwa mtindo huu, ni vizuri chama kikawa macho na watu hawa,” alisema.

  Hata hivyo, Sendeka alisema pamoja na hujuma za wabaya hao wa kisiasa bado wapiga kura wake wana imani kubwa naye na hivyo ana uhakika wa kushinda uchaguzi huo. Upigaji wa kura za maoni kwa wagombea wa CCM wanaowania nafasi za udiwani na ubunge zinatarajiwa kuanza mapema Agosti nchi nzima.

  Kusambazwa kwa kadi feki za CCM katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Simanjiro kumelalamikiwa na wanachama kadhaa na kuthibitishwa na viongozi wa CCM wa wilaya hiyo.

  Viongozi wa CCM wa wilaya hiyo, wameithibitishia Nipashe kufanyika kwa kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya CCM Juni 28 kujadili suala la kadi feki na kuwachukulia hatua waliohusika.

  Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Simanjiro, Brown Mthew Ole Suya, alisema kuwa zaidi ya kadi 1,000 zisizo halali zilibainika kuingizwa katika kata sita kati ya kata 15 za wilaya hiyo.

  Suya alisema baada ya kuzigundua walianza kuchukua hatua kuhakikisha zinasimamishwa na kuzikamata zilizokuwa zimeshasambazwa.

  Alisema kuwa hatua nyingine ni kuwasimamisha watendaji waliobainika kuhusika katika njama hizo kwa kuzipokea na kuzisajili katika daftari la orodha ya majina ya wanachama ambao mwaka huu ndio watakaowapigia wagombea udiwani na ubunge kura za maoni.
   
Loading...