Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizibao, Jan 1, 2011.

 1. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 80
  RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amtetea Mwanawe Fatma Karume kuwa ndio mmiliki halali wa kiwanja kilichopo Mbweni eneo la Mfuuni ambacho kimeingia katika mgogoro kati ya Kanisa la Angalikan na mwanawe huyo.
  Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana, Mbweni, Karume alisema mwanawe ana hati kamili za kiwanja hicho kutoka serikalini kwa kuwa ametimiza vigezo vyote vinavyohitajika na hivyo anastahiki kujenga kwa kuwa kiwanja hicho ni chake.
  Juzi Kasisi Msaidizi wa Kanisa la Angalikan Zanzibar, Mathew Wilfred Mhagama aliongoza maombi maalumu na kumtaja Fatma Karume kuwa ameporwa kiwanja cha kanisa hilo pamoja na sehemu muhimu ya makaburi ya wazazi wao ambayo yamekuwepo kwa miongo kadhaa katika eneo hilo.
  Karume alisema kwamba ni yeye aliyechukuwa juhudi za kuyatunza makaburi yaliopo eneo la Mfuuni kutokana na waumini wenyewe kuyatekeleza makaburi yao kwa muda mrefu sana.
  Alisema yeye na familia yake imefanya kazi kubwa ya kulilinda na kuliokoa kanisa hilo ikiwa pamoja na kutafuta mlinzi kwa kuwa muda mrefu lilikuwa halina mlinzi na milango yake ilikuwa ikiwa wazi kwa muda wa miaka kadhaa.
  “Makaburi yale mlioyaona kwa muda wa miaka 20 sasa yanatunzwa na familia yetu… ni mimi binafsi na familia yangu yote ndio tunaoyatizama na baadhi ya wakati hupata nafasi ya kutoa pesa kwa ajili ya kulimiwa majani na kufanyiwa usafi katika eneo lote lile la makaburi yaliopo pale”alisema Karume huku akiwa amekaa na binti yake pembezoni.
  Awali Karume alieleza masikitiko yake kutokana na kauli zilizotolewa na viongozi hao wa dini huku akisema hawajasema ukweli na badala yake wameendekeza jazba ambazo zimewafanya waumini wao kwenda moja kwa moja katika kiwanja na kufanya fujo la kuharibu mali ya mwanawe ambaye ni mmiliki halali wa kiwanja hicho.
  Karume aliwaita viongozi walioongoza misa juzi katika kanisa la Angalika liliopo Mbweni na kukusanya kundi la waumini wa dini hiyo kwamba ni viongozi waliopotoka na wasiofuata maadili na mafundisho ya kitabu kinachowaongoza.
  Alisema viongozi hao wamepotoka kwa kuwa wameshindwa kufuata maadili ya dini yao inavyowaelekeza na kitendo cha kujichukulia sheria mikononi mwao cha kuvunja vunja vifaa vilivyokuwa katika eneo la ujenzi na kuharibu mali ya watu ni kosa kisheria.
  “Nimeshangazwa sana na hawa viongozi wa dini ni viongozi wa ajabu sana tena wamepotoka kabisa ..kwa sababu wameshindwa kufuata maadili ..naona wanakosa utu na heshima kwa wakubwa zao” alisema Rais Mstaafu Karume huku akiwa amekunja uso wake na kutafuna tafuna ulimi wakena kuongeza kwamba.
  “Tangu enzi za baba yangu pamoja na mimi nimekuwa na uhusiano mzuri na kanisa hilo…..nimehamia hapa katika mwaka 1968 hakuna mtu yoyote katika eneo hili isipokuwa kanisa” alisema Karume na kuwageukia waandishi wa habari.
  Hata hivyo Rais huyo mstaafu aliwapoza waumini wa kanisa hilo la Angalikan kwa kusema kwamba ujenzi wa mwanawe huyo hautoathiri wala kubomowa makaburi yaliopo jirani ya kiwanja hicho hasa kwa kuzingatia kwamba makaburi hayo yanatunzwa na familia yake kwa miaka mingi tu.
  Akiongea baada ya kumaliza baba yake binti huyo Fatma Karume alisema hana mpango wowote wa kuharibu wala kubomoa makaburi ya waumini wa wakrito na ujenzi wake utaheshimu eneo hilo muhimu la makaburi.
  “Mimi ndio mmiliki wa eneo hili kihalali na hati zote kamili za kisheria ninazo mimi dini yangu ya kiislamu na madhehebu yangu yananiagiza kuheshimu dini nyengine kwa hivyo sina matatizo wala nia ya kuharibu wala kubomoa makaburi wa dini nyengine kwa sababu ninaheshimu dini zote” alisema Fatma Karume ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
  Fatma naye kama baba yake alishangazwa na waumini wa madhehebu hayo ya kiangalikan kutokana na kuiruhusu kampuni moja ya Kichina inayojenga hoteli karibu na eneo la makaburi ambapo udongo unaochimbwa katika ujenzi wa hoteli hiyo inayojengwa humiminwa makaburi hapo kwa kuwa uongozi wa kanisa hilo umetoa ruhusa wenyewe.
  Aliulaumu uongozi wa kanisa la Anglikana kwa kuruhusu kampuni inayojenga hoteli na kuweka kifusi na udongo katika makaburi ya Wakristo na hivyo kuyaharibu makaburi hayo ambayo waumini hao wanasema kwamba makaburi yao yamechimbwa na kungolewa misalaba yao wakati uongozi ndio uliotoka kibali cha uharibifu huo.
  “Nimeshangazwa sana na uongozi wa kanisa hili kwa kwa kuiruhusu kampuni hiyo ya kichina kumwaga kifusi wanachokichota kule katika hoteli na kukimwaga katika eneo lile la makaburi….nimekuwa najiuliza nani anayepuuza na kudharau makaburi haya ni mimi au wao wenyewe walioruhusu hii kampuni kumwaga udongo”?alihoji Fatma Karume.
  Juzi kanisa la Angalikan liliitisha misa maalumu ya maombi yaliongozwa na Kasisi Msaidizi, Mathew Wilfred Mhagama wa kanisa Mkunazini Zanzibar, kumshitakia Mungu wakidai wameporwa ardhi yao na binti wa rais mastaafu na kuwataka waumini hao kutembea kwa mguu hadi kwenye kiwanja kilichopo mbweni na kushuhudia ujenzi wa jengo linalomilikiwa na Fatma Karume.

  Na Salma Said
   
 2. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kaaaazi kweli kweli , watawala wetu bana , ndiyo maana hawataki kutaja mali wakiingia na kutoka madarakani
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama kweli basi hawa waumini wanataka kuleta fujo kisiwani wadhibitiwe
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Mbona bosi wako Muddy alikuwa mtu wa fujo?
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Adhibitiwe pia
   
 6. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  I think Karume was not supposed to react. It's a very small issue so Fatma should be able to solve rather the Former president getting involved as Daddy!!!
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ogopa free lunches. Sasa kama hapo mahali walikuwapo rais mstaafu na waanglikana peke yao, hicho kiwanja cha mwanae kilitoka wapi? Na kwa nini awapoze kuwa hataharibu makaburi yao kama hilo eneo alilopewa mwanawe halimo katika eneo la waangalikana? Hayo ya makaratasi hayana maana, maana mtoto wa rais hawezi kuyakosa!

  Amandla........
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  African bigmen!
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa nini mwanae mwenyewe asitete mali yake ila babake? tena kwa kuwa uyo mwanae nasikia ni mwanasheria mahiri wa IMMA nadhani ndio angetoa utetetzi mzuri zaidi. au ndio yale ya double standards? i will keep watching this saga
   
 10. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,361
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Tungependa kujua je nao Waanglikana wana makaratasi ya umiliki au ushahidi wowote wa umiliki wa eneo? Je kati ya vielelezo vya Fatma na Kanisa ni vipi vilitangulia kutolewa? Mwisho napata shaka kwamba iweje kama eneo ni la Fatuma liwe na makaburi ya Waanglikana tena kwa miaka mingi?

  Je huyo dada mwanasheria ni yule ambaye tuliwahi sikia kwamba alimrushia makonde Hakimu pale Kisutu na hakuchukuliwa hatua zozote?
   
 11. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 80
  Inaonesha hiyo habari hujaosoma vizuri.... soma tena hiyo habari.Na kuhus hicho kiwanja Anglikan sio chao kabisa bali sehemu ya makaburi yao yako jirani na hicho kiwanja na hawana hata hati ya kumuliki hicho kiwanja na hakuna record zinazoonyesha hicho kiwanja kama ni chao, Sasa waache waanzishe vurugu wanaweza kukosa kila kitu...Hasa ukizingatia serikali imewaachia kukusanya zile dola 3 kwa kila mtaalii anayetembelea mahandaki ya watumwa pale mkunazini na kutokana na sheria za zanzibar yale mapato yanatakiwa kukusanywa na serikali sasa lakini SMZ hata haiwaulizi sasa wache watikise kibiri..na kuhusu kukipata hicho kiwanja wasahau kabisa kwani hawajadhulumiwa na hicho kiwanja si haki yao na hawana historia ya kukimiliki kwani kabla ya kutaifishwa kilikuwa kinamilikiwa na watu wengine na siyo wao.....na waiendeea ivo zie subra za watu uwaumbia macho naona ama zitaotea
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sio fujo,hawa wote wanataka kuua ukristo katika zanzibar!
  Na ukweli ni kwamba injili ita hubiriwa kwa hali yoyote ile
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nasikia ndiye yeye
   
 14. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #14
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  ...................hapa pangu.................
   
 15. B

  Bull JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa wanajaza makanisa Zanzibar nani anahitaji ? Wazanzibari wanahitaji maendeleo sio makanisa au campaign yakuendeleza ubaradhuli ?
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hayo makanisa yasingekuwa yanahitajika yasingejengwa maana hakuna ambaye angekuwa anahudhuria ibada.Kanisa Anglikana lilikuwepo Zanzibar hata kabla ya babu wa babu yako! Hapa wanachodai ni eneo lao ambalo walikuwa nalo miaka nenda rudi. Kinachopigiwa kelele hapa ni dhulma inayofanywa na mwenye nacho. Au unataka kutuambia kuwa kwa sababu ni wakristu basi hawana haki?

  Amandla.....
   
 17. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 80
  Hahahahaha nazani unakumbuka ya kuwa watu wengi sana walitaifishwa mali zao baada ya mapinduzi ZNZ na siyo Anglikan tu... Na hawana ushahidi wa maandishi ya kuwa ile sehemu ilikuwa ni yao just wanabwabwaja tu kwenye vyombo vya habari na hiyo ndiyo bigest mistake yao wana wataijutia from now on....Na hata hiyo sehemu ikiwa ni yao basi wao siyo special kiasi hicho cha kuwafanya warudishiwe. kwani kuna watu wana documents halali kabisa ya mali zao zilizotaifisha baada ya mapinduzi na hawatopewa. basi kwa hivyo hilo kanisa wasahau kabisa.kwani wananchi wanasubiri kwa hamu kubwa sana nini kitatokea na SMZ haitofanya kosa hilo
   
 18. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna uwezekano mkubwa kanisa ndio wako sahihi. Kwanini siku zote walikuwa wanaambiwa na serikali wawe na subira wakati wanadai hati miliki ya kiwanja? Je haitoshi kuamini kuwa Fatma alimilikishwa kiwanja isivyo halali na serikali ya babake? Ni lazima serikali itende haki kwenye huu mgogoro wenye sura ya kidini.
   
 19. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Wakirejeshewa ardhi yao Kanisa basi na sisi ambao wazee wetu wamechukuliwa mashamba yao na wanazo hati halali za umiliki tangu enzi ya ukoloni tupewe.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,541
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  Nyumba ya bintiye Karume yabomolewa Friday, 31 December 2010 20:49

  Salma Said,
  Zanzibar
  WAUMINI wa Kanisa la Angalikana Visiwani Zanzibar wamevamia kiwanja cha familia ya Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na kuvunja baadhi miundombinu iliyowekwa kusaidia ujenzi katika eneo la Mbweni, mjini Unguja.

  Katika tukio hilo la juzi jioni, waumini hao wakiongozwa na viongozi wao pia walimwaga maji yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye matangi katika eneo hilo, ikiwa ni ishara ya kupinga ujenzi unaoendelea katika kianja hicho wanachodai kuwa ni mali ya kainisa lao.

  Kiwanja kilichovamiwa na waumini hao kinadaiwa kuwa mali ya Fatma Karume ambaye ni wakili jijini Dar es Salaam na kwamba kinapakana eneo ambalo baba yake, Rais Mstaafu Amani Karume, amejenga makazi yake.

  Tukio la kuvamia kiwanja hicho lilitanguliwa na ibada ya maombi yaliyoongozwa na Rev Canon Mathew Mhagama wa Kanisa la Angalikana la Mkunazini, sala iliyofanyika Mbweni kanisa ambalo lipo karibu na kiwanja kinachodaiwa kuporwa na familia ya Rais Karume.

  Baada ya kumaliza maombi hayo, waumini wote kwa pamoja waliongozana hadi kwenye kiwanja hicho, ambapo walishuhudia baadhi ya misalaba ya makaburi yao ikiwa imeng'olewa na hapo walionekana kukerwa na kitendo hicho huku wakidai kwamba misalaba hiyo imedharauliwa.

  “Tuliambiwa tusipendeshe jazba, lakini haiwezekani kwa sababu tumekerwa kwa kuporwa kiwanja chetu, na kilichotukasirisha sana ni kule kuona misalaba ya makaburi ya bibi na babu zetu ikiwa imeng'olewa..hii ni dharau kubwa sana kwa wazee wetu,” alisema mmoja wa waumini hao.


  Kuhusu ibada ya maombi maalumu waliyoyaita kuwa ni ya kuombea kiwanja kilichoporwa na mwenye nguvu, Mhagama alisema lengo ni kushtakia kwa Mungu ili kulainisha moyo wa anayedaiwa kumiliki eneo hilo ili abadilike na kulirejesha kwa kanisa.

  “Leo tumeamua kufanya ibada hii maalumu kwa makusudi kumuomba Mungu atusaidie na kuwagusa watendaji katika idara ya ardhi, watende haki na kuturudishia kiwanja chetu cha Mfuuni ambacho dada mmoja mwenye nguvu za mwili amekichukua na sasa anajenga. Tunamuomba Mungu pia atusaidie na wengine ambao wana maumivu kama yetu” alisema Mhagama.

  Kiongozi huyo na wenzake walisema licha eneo hilo kuwa lao wanashangazwa na hatua ya ujenzi ambao umeanza kufanyika japokuwa haikiweza kufahamika mara moja iwapo jengo linalokusudiwa ni kwa ajili ya makazi au shughuli za biashara.

  “.....Fatma juzi katambia kwamba eneo hili ni lake na kwamba hati anayo, japokuwa hatujathibitisha jinsi alivyoweza kupata hati hiyo...," alisema Mhagama na kuongeza: ".....surname (ubini) wake wa jina lenye historia nzuri ya visiwa hivi, ukilitajataja katika migogoro tutakua hatumtendei haki mzee wetu Abeid Karume ambaye yeye ndie shujaa wa Wazanzibari wote".

  Aliendelea kuhoji; “Swali ambalo tunamuuliza Mkurugenzi na Katibu Mkuu wake je haya makaburi yetu na miili ya ndugu zetu waliolala pale nayo yametaifishwa mwaka 1964, Je sisi na huyu dada nani alieomba mwanzo kupimiwa kiwanja na kupewa hati? Kwanini mnatuambia fanyeni staha, mara mtapimiwa na kupewa hati halafu mtu mwengine anapewa hati, je haki iko wapi hapa, yako wapi yale mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 yaliyoondoa tabaka za itikadi rangi na vyama vya kikabila?”.

  Naye Canon Emanuel Masoud alisema hawatosita kudai haki yao kwa kuwa Wakristo Zanzibar wamekuwa na maumivu kutokana na kudharauliwa kwani ni muda mrefu wamekuwa wakitumia busara za kuomba hati za kumiliki viwanja ambavyo walirithi kwa wazazi wao, lakini hakuna jibu zuri linalotolewa zaidi ya kupewa tamaa tu.

  Askofu Mhagama akitoa historia ya eneo hilo alisema, Askofu George Tozer wa NMCA, Septemba, 1871 alinunua shamba katika eneo hilo la Mbweni ekari 30, wakati Kanisa lilimiliki ekari zipatazo 150 huku Wamisionari mara mbili waliamua kuuza baadhi ya maeneo.

  Alisema mwaka 1964 ilipitishwa sheria ya ardhi kuwa mali ya Serikali kwa lengo la kunufaisha umma na sio kikundi cha watu fulani au mtu na huku wakimsifia Rais wa kwanza, Hayati Abeid Karume kwa kuamua kugawa ekari tatu kwa kila mwananchi.


  Hata hivyo, Askofu Mhagama alisema hakuna kumbukumbu zinazoonesha kuwa mali ya Kanisa imemilikishwa serikalini kisheria au kugaiwa mtu.

  Alieleza mawasiliano yaliyofanyika baina yao na ofisi za Serikali ambapo kati ya mwaka 1998 na 2006 hatimaye Julai 4, 2006 waliahidiwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi kwamba suala la kanisa kupewa hati ya kumiliki kiwanja hicho linashughulikiwa na hivyo kutakiwa wawe na subira.

  Waumini hao wanadai kuwa hilo ni eneo lao ambalo wamelirithi kutoka kwa wazee wao wamekuwa wakilitumia kwa maziko hivyo kuiomba Serikali kuwarejeshea eneo hilo.

  Migogoro ya ardhi ni inayofukuta hivi sasa ni changamoto kwa Serikali ya Awamu ya Saba inayoongozwa na Dk Ali Mohammed Shein kutokana na wananchi wengi pamoja na taasisi kadhaa zikiwemo za kidini kuibuka kwa madai ya kudhulumiwa ardhi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba
   
Loading...