Kadawi Limbu, Katibu Mkuu wa Chama kipya cha ADC Aumbuliwa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kadawi Limbu, Katibu Mkuu wa Chama kipya cha ADC Aumbuliwa...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Jun 14, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Katibu mkuu wa chama kipya cha siasa Alliance for Democratic Change (ADC) Kadawi Lukas Limbu juzi ameumbuka katika mgahawa wa Falcon uliopo mtaa wa Lumumba, alipokuwa akikipondea chama cha CHADEMA.

  Huku akiendelea kujinasibu kwamba chama chake cha ADC ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuiletea nchi mabadiliko yanayohitajika, na kwamba kuichagua Chadema itakuwa ni makosa makubwa sana kwakuwa hakitaweza kuleta mabadiliko yoyote kwakuwa ni chama cha kidikteta.

  Akatolea mifano mbalimbali kushadidia hoja zake mathalani hoja kama ya kufukuzwa madiwani watano wa Arusha, kadhia ya shibuda lakini pia akaongezea kwamba marehemu Bob Makani alikuwa ametengwa, kwamba hakuna mtoto wake hata mmoja mwenye cheo chochote ndani ya Chadema, na kwamba hakuna ndugu yake wa karibu aliyepata nafasi ya kuteuliwa viti maalum pamoja na tuhuma nyengine nyingi.

  Bwana mmoja aliyekuwa amesimama counter akinunua chakula aliamua kumkabili. Baadhi ya hoja alizozielekeza kwa Kadawi ni pamoja kumuuliza, kama anadhani Chadema ni chama kibaya kiasi hicho, mbona wame copy na ku paste mambo mengi ya Chadema ikiwa ni pamoja rangi za bendera ya Chadema? Akamuuliza kama Chadema ni chama kibaya kuliko CCM na CUF, mbona ameikimbia CUF na kuanzisha chama kingine, kwanini hakubaki CUF ama kwenda CCM? Akamuuliza madai kwamba watoto wa Bob Makani hawapati nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama, ni mtoto gani aliwahi kugombea nafasi ya uongozi na akafanyiwa hila, japo hata viti maalum?

  Yule bwana akaenda mbali zaidi kwa kumfahamisha kwamba kama anadhani anaweza kukijenga chama chake cha ADC kwa kupitia mgongo wa Chadema atambue kwamba amepotea njia na anapoteza muda wake kwani wananchi wameshaamua kwamba sasa ccm basi na chadema ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuiongoza nchi hii na kama ametumwa na CCM kuisaidia kufanya propaganda dhidi ya Chadema atambue kwamba ameshindwa kazi kabla hajaianza.

  Baada ya kuona jamaa anazidi kumkabili na hoja moto moto zikiendelea kumwagwa, Kadawi akaamua kuondoka haraka huku watu waliokuwepo wakimdhihaki kwamba amekutana na kiboko yake.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Aliyemtuma Kadawi hakumwandaa kisaikolojia kuwa angekutana na challenges.
  Halafu inawezekana Kadawi ni katibu jina tu.
   
 3. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mamluki mchumia tumbo anakubali kuwa mtumwa ktk nchi yake.
   
 4. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Aliemtuma amdai pesa yake,CDM kimeshateuliwa kuwa mkombozi wa mnyonge wa nchi hii,nashauri siku akitokea pengine azomewe sana....
   
 5. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,027
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hiyo. Pambana na watu wajinga wajinga sio kwa ngumi na mateke (mgeni siku ya kumi) bali kwa hoja motomoto hadi akimbie huku akizomewa kwa aibu.

  Ndimi Bazazi!
   
 6. s

  slufay JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hiyo chama ni cha mbunge wa wawi (ex - CUF expelled member ) hilo ni boya,,,, hajadesa vizuri.
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Siku hizi kila mwanasiasa akitaka ajulikane lazima ainange chadema?
  CUF,NCCR na vinginevyo hawavioni?
  Shame on you Adawi.
   
 8. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna haja ya Msajili wa Vyama vya siasa kuwapima akili watu kama hawa akina Limbu kabla ya kusajili vyama vyao
   
 9. s

  sawabho JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Wapinzani wa Tanzania hawafahamu adui yao ni yupi. Wanapaswa kufahamu kuwa adui yao ni wao wenyewe !!!! Laiti kama nyoka wote wangekuwa na umoja kama wa nyuki, hakuna binadamu ambaye angediriki kumua nyoka.
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  personal namfaham huyu jamaa, jina maarufu ni Limbu, msukuma wa meatu shinyanga, hana lolote ni choka mbaya, no school no nini nadhan kawekwa kama boya tu, baadae ndio wachague katibu, fikiria katbu gani anabishana kwenye mgahawa? njaa mbaya Limbu
   
 11. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Mh! Kaaaziii kweli kweli, yaana kumbe ma zumbukuku wazajuki bado wapo wengi
   
 12. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Hivi kumbe kadawi ni zuzu hivi? Chama chake wala hakijulikani ofisi yake ilipo, na kimeanzishwa juzi juzi tu na hakija pata hata mjumbe wa nyumba kumi, anapata wapi ujasiri wa kuongopea watu kwamba ndo chama cha ukombozi wa taifa hili? Kweli ni katibu boya tu.
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Kumbe ADC, watakuwa wanarithishana vyeo kama wanavyofanya CCM? Basi wasijesema ni watu wa democrasia
   
 14. M

  MTK JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Duh kaka Mwita Maranya asante sana kwani nilikuwa sijui A wala B kuhusu ADC! kama kweli huyo mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri na kuchambua mambo; basi ADC iko matatani, ni kweli imeshindwa kabla ya kuanza. Adieu ADC!!
   
 15. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  kweli huyu limbu ni boya na kilaza wa kutupwa. hizo sera za kuwapa vyeo watoto wa viongozi si za cdm bali ni za ccm. km katibu anaongea pumba hivi huyu mwenyekiti atakuwaje?
   
 16. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Hivi ana undugu na Festus Limbu? kama ndiyo, mbona mwenzake amekwenda darasa za kutosha! au ndo pesa ya ada alikuwa anapeperushia shada tu ?!!
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wahudumu wa falcon walicheka sana siku hiyo wakasema ni mteja wao wa kila siku na amekuwa akiikandia Chadema lakini siku ile alipatikana. Mimi niliamua kukaa kimya tu kwani shughuli aliyokuwa akiipata toka kwa mdau ilikuwa inamtosha.

  Kutokana na chama chenyewe kuanzishwa na wafuasi wa hamad rashid, sina shaka kwamba kadawi ameshikilia ile nafasi kwa muda tu ili wenyewe waje kuichukua muda muafaka ukifika, bora hata angebakia cuf lakini huko alikopelekwa sasa amepotea kabisa.
   
 18. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  si ndugu hata kidogo ni majina tu ya kisukuma
   
 19. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nilipomuona katika mijadala mbalimbali wakati akiwania ubunge wa temeke akiwa cuf nilimuona kama yuko vizuri upstairs lakini kwa aibu aliyokutana nayo juzi ni kamuona kumbe naye bei yake imeshafahamika.
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na nyinyiem inajua sana kucheza na hawa wapinzani njaa kali wanaofahamika bei zao. Ni dhahiri kwamba ADC wanatumiwa na nyinyiem kwani hali yao kisiasa ni mbaya sana kwahiyo wakipata mtu anayeweza kuwasaidia kupigana na Chadema wako tayari kumuwezesha kadri inavyowezekana. Sasa katika mazingira hayo waganga njaa wanayatumia vizuri kujipatia ajira.
   
Loading...