Kadanganya ni mjamzito, kumbe anaweka matambara tumbo liwe kubwa

Mr mgeni

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
1,222
804
Shemeji yangu anamdanganya kaka kwamba ana mimba kumbe hana, mwezi wa 4 sasa anavisha tumbo matambara liwe kubwa, hiyo ni baada ya siku moja kumfuma bila yeye kutarajia.

Nipeni ushauri nipasue hilo jipu au?
 
Ukitoboa utakuwa huna ushahidi unaotosheleza. Pia wanandoa wana tabia moja kuwa pale unapomshitaki mwenzake kwake kuwa anachepuka watavutana alafu baadae watapatana na kwa pamoja watasema mchawi wa ndoa yetu ni wewe watakuaibisha mpk jamii itakuona unavunja ndoa ya watu.
Kaa mbali na hiyo ndoa km itavunjika ivunjike yenyewe we usiweke mkono wako hata km una ushahidi wa kuchepuka, haitakusaidia kwa lolote.
 
Miezi 4, anavaa tambara? Jamaa hajui? Inamaana wanatombana gizani? Miezi minne hata hawajawahi oga pamoja?

Huyo jamaa wala usimwambie, hakuna namna, huyo jamaa sio rizki, hata yeye anahusika na hiyo mimba feki ili ndugu jamaa na marafiki waamini kuwa nae ni mzima, tena anamlipa huyo dada ili kuigiza hivyo na kuficha aibu ya jamaa, baada ya muda mtasikia mimba imetoka.
 
ndo maana nimeomba ushauri nisije nikapayuku
Achana nao
Utakuja onekana mchawi bdae
Au unadhan hata akijua shem anadanganya unadhan atamuacha?
Hatomuacha watagombana alafu watapatana NDIPO UTARUDI KIJIJINI maana shem atakulipiza
Temana nao walipotongozana hukuepo
 
Shemeji yangu anamdanganya braza kwamba ana mimba kumbe hana,mwezi wa 4 sasa anavisha tumba matambara liwe kubwa,hiyo ni baada ya siku moja kumfuma bila yeye kutarajia.nipeni ushauri nipasue hilo jipu au?
Mwana kuna vitu vya kutunga kama unataka kujaza thread sio hivi....daaaaah....miez 4 kwan mchiz kipofu au???mm nadhan braza waKo KIPOFU...
 
Anavisha matambala kwani huyo kaka yako halali na mkewe mpaka kashindwa kumgundua?????? acha umbea acha siku atajionea mwenyewe
 
Ushauri gani unaotaka sasa hapa mkuu vitu vingine unajiongeza mwenyewe bana
 
Shemeji yangu anamdanganya braza kwamba ana mimba kumbe hana,mwezi wa 4 sasa anavisha tumba matambara liwe kubwa,hiyo ni baada ya siku moja kumfuma bila yeye kutarajia.nipeni ushauri nipasue hilo jipu au?
MJINGA MKUBWA WW TOA HII POST YAKO HAPA, HUYO KAKA YAKO HAWALALI NA MKE WAKE???

YAAN ULALE NA MWANAMKE ANA MATAMBALA USIGUNDUE
 
wewe na shemeji yako mna tatizo la akili!!!!!!

utashangaa lakini huo ndio ukweli.

tatizo hilo kwa shemeji yako ni yeye kutokupata mimba imemuathiri kisaikolojia mpaka uwezo wake wa akili kutafakari na kuona hilo ni jambo ambalo linawezekana katika maisha na tatizo linaweza kutoka upande wowote katika pande zinazotengeneza mimba. sasa ana mshauri asiyemjua anayempa mawazo ya kujifanya ana mimba kumbe hapo ndio anafanya jambo la kawaida la yeye hajapata mimba kuwa tatizo kwa kuweka nguo kufeki mimba. sio yeye bali ana mshauri.

kwako wewe ni vigumu kukuaminisha kuwa una ugonjwa wa akili kwa maana imani hazijaingizwa rasmi katika magonjwa ya akili lakini uwezekano wa wewe vile vile kuwa na mshauri anayekupa mawazo ni mkubwa.

kwa kifupi kinachompa mawazo shemeji yako aweke nguo kinamdanganya na kitacreate scandal out of that na sio solution. sasa ili kutengeneza hiyo scandal ndio hapo wakati anaweka hizo nguo unaletewa mawazo kwenda kuangalia. hapa unaweza kujisikia kwenda sehemu fulani au msukumo fulani na unapofika na kukuta jambo unajisifu eti mungu kakuonyesha kumbe ni vitu vinadanganya watu na vinatumia watu waliowazunguka kutengeneza scandal.

jinasue kwenye ujinga unaolekea kusambaratisha ndoa ya ndugu yako umwendee shemeji yako na umweleze kuwa kutokupata mimba ni jambo la kawaida na kujaribu kudanganya atavunja ndoa na asijaribu kabisa.

lakini inwezekana wewe hujaona shemeji yako ana mimba kweli ila ugonjwa unao wewe tu unaletewa mawazo ya hana mimba anaweka matambaa. kuwa na uhakika maana ukikurupuka mahusiano yako na shemeji yako yataingia dosari.

Shemeji yangu anamdanganya braza kwamba ana mimba kumbe hana,mwezi wa 4 sasa anavisha tumba matambara liwe kubwa,hiyo ni baada ya siku moja kumfuma bila yeye kutarajia.nipeni ushauri nipasue hilo jipu au?
 
Shemeji yangu anamdanganya braza kwamba ana mimba kumbe hana,mwezi wa 4 sasa anavisha tumba matambara liwe kubwa,hiyo ni baada ya siku moja kumfuma bila yeye kutarajia.nipeni ushauri nipasue hilo jipu au?
Acha miezi 9 itimie mwenyewe atajua. kwani akila tunda haoni hilo tumbo?
 
Back
Top Bottom