KadaMpinzani asema: Mnyika,Mbowe na Slaa tulieni kama maji ya kwenye mtungi !!

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
86
Yap, i said it !

Mnyika siasa zake kama Mrema, (yupo kwenye siasa kama geresha)
Slaa za kwake ni za kikabila kabila, !
Mbowe (huyu mchafu na uchafu wake hata sijui niuanzie wapi)

Haya wee mwanawane, kaeni mkao wa kula..More info to come !
 
...Yap, you said it KadaMpinzani... and you said it with similar persuasion as in this overdue thread:

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6571&highlight=mafisadi

ee bwana eeh, tena hiyo thread inanikumbusha mbali kweli, maana natoa tu thread ya mafisadi JAMBOFORUMS ikapamba moto nashangaa ikahamishwa almost mara 8 nzima mara huku mara kule, mwishowe wakaifuta then sijui wakaifanyia nini na hiyo yote ilitokana na wao kufuta thread iliyoanzishwa na member mwingine ambaye alikuwa akinipa hongera kwa kufikisha posts 2,000 i think ! AMBAO HAWAKUWA NA NAFASI YA KUSOMA HIYO THREAD BONYEZENI HIYO LINK HAPO ALIYOTOA STEVE-D NA MSOME !

Well, back to the topic, Nitawaongelea zaidi baadae hao niliowataja !

Thanks steve-d kwa hiyo thread !
 
Yap, i said it !

Mnyika siasa zake kama Mrema, (yupo kwenye siasa kama geresha)
Slaa za kwake ni za kikabila kabila, !
Mbowe (huyu mchafu na uchafu wake hata sijui niuanzie wapi)

Haya wee mwanawane, kaeni mkao wa kula..More info to come !

Naona sasa unaingia ushabiki hapa usiokuwa na kichwa wala miguu. Slaa kama siyo kuuvalia njuga ufisadi mkubwa uliofanywa BoT kweli tungejua uozo uliojaa pale uliosababisha Balalli kuikimbia nchi na Viongozi wengine kutotaka arudi Tanzania kwa wasiwasi ushahidi atakaoutoa utawahusisha katika kashfa ya BoT? Je, ufisadi uliofanywa BoT, Richmond na kwingineko ambao Slaa amekuwa mstari wa mbele kuupigia kelele unawagusa wachaga tu na siyo Watanzania wengine!? :confused:

Je, kama siyo Slaa mawaziri waliokuwa wanaohusika kwa namna moja au nyingine na kashfa ya BoT akina Mramma , Meghji na wengine si wangekuwa bado wanapeta tu na nyadhifa zao?

Slaa alipoongea aliongea kwa niaba ya Watanzania wote, naomba nifafanuli uozo uliojaa pale BoT unawagusa wachaga tu na sio Watanzania wote wa kila kona ya nchi yetu?

Wana JF naona kuna njama kubwa sana za kuvuruga majadiliano mazito yanayoendelea hapa kuhusiana na ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi mbali mbali wa siri kali, kama tusipokuwa makini basi hii JF itavurugwa ili tuache majadiliano yenye umuhimu mkubwa kuhusiana na ufisadi ambayo yanaingamiza nchi yetu.
 
Slaa alipotoa tuhuma za BoT aliambiwa ni mzushi na Ballali akatamka hadharani kwa "sijiuzulu ng'o" leo kaikimbia nchi.

Alipotia tuhuma dhidi ya mafuisadi ndani ya Sirikali wengi walitishia kufungua mashtaka dhidi ya Dk Slaa, lakini hakuna hata mmoja aliyefanya hivyo. Watanzania tunajua nani alikuwa anasema kweli katika sakata la ufisadi wa BoT. Hebu kuwa na mapenzi ya kweli ya Tanzania badala ya kutumiwa na watu ambao wanaiangamiza Tanzania kwa ufisadi wao. CCM ni chama tu kinaweza kikasambaratika au hata kufa wakati wowote na halitakuwa pigo kwa Mtanzania yeyote yule, lakini Tanzania ni nchi siku zote inastahili kupewa kipaumbele kuliko CCM

SERIKALI imetoa taarifa kujibu shutuma za rushwa kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu kwa kupitia CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.

Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa Sept. 28, 2007 na Waziri ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Muhammad Seif Khatib (pichani) imesema shutuma hizo hazina msingi wowote na zinastahili kupuuzwa.

"Tafsiri pekee na mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005," imeeleza.

Imesema kwmba Serikali inapinga vitendo vya rushwa nchini "kwa nguvu zake zote" na kama Dk. Slaa na wenzake wana lengo la kupiga vita rushwa basi tuhuma hizo wangezifikisha katika vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.

Dk. Slaa, akiwaongoza wanasiasa wenzake kadhaa wa kambi ya upinzani, walitoa tamko hadharani Septemba 15 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma kuwa wanashiriki vitendo vya rushwa.

Kufuatia tuhuma hizo, gazeti la kila wiki la MwanaHalisi linalotolewa jijini Dar es Salaam, limekuwa likisambaza tuhuma hizo bila ya kutafuta ukweli wake, taarifa imesema.

Taarika kamili ya Serikali inatarajiwa kuchapishwa ikiwa ni tangazo katika magazeti kadhaa ya kila siku Jumamosi Sept. 29, 2007.

Taarifa imesema Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa, awamu ya kwanza ya mwaka 1997/2004 na awamu ya pili mwaka 2005/2010.

Imenukuu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, Ibara ya 110, inayoelezea mapambano dhidi ya rushwa na tamko la Rais Jakaya Kikwete dhidi ya rushwa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge Desemba 29, 2005.

Serikali imeanzisha Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye Wilaya zote nchini, imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na inashirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, imesema.

"Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa [WINDOWS-1252?]nchini…Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongioni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili," imeongeza.

Taarifa imesema Serikali inaelewa kwamba Dk. Slaa na wenzake ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda lakini walishindwa na wananchi kuichagua CCM.

Imesema wananchi wanayaona mafanikio mengi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba wanachokitafuta wale walioshindwa ni kile walichokikosa na hivyo wanajaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani.

"Hivyo ni vyema wananchi wakatambua kwamba wapinzani hawa hivi sasa wanatapatapa na wanataka kutuondoa katika lengo letu la kuwaletea maisha bora Watanzania," imeongeza.
 
Yap, i said it !

Mnyika siasa zake kama Mrema, (yupo kwenye siasa kama geresha)
Slaa za kwake ni za kikabila kabila, !
Mbowe (huyu mchafu na uchafu wake hata sijui niuanzie wapi)

Haya wee mwanawane, kaeni mkao wa kula..More info to come !

Kada anaikumbusha zamani zile tulivyokuwa tunamwibia mapera mzee moja jirani yetu kule Malinyi.
Kwa kawaida tuligawana makundi mawili moja la vijana watatu na jingine kubwa kadri iwezekanavyo.

Ili kuiba mapera kiulanini sisi watatu tulikuwa tunakwenda na kumchokonoa mzee yule barazani kwake kwa maneno ya dharau na kebehi, kwa hasira aliamka na kuanza kutufukuza.
Huko nyuma wenzetu walivamia mti wa mapera na kuyachuma kwa fujo.

Cha ajabu mzee yule alikuwa akiingia Gauge kila siku kwa mchezo ule ule mpka wazee wetu walipo tulamba bakora za matakoni kwa mtindo wa mwana koma ndipo tukaacha mchezo wetu.

Kada ujanja wako wa kutaka kupunguza kasi ya kujadiri mambo muhimu kwa kutengeneza vjidetour tumeushitukia.

Kajipige msasa halafu uje ujaribu tena kwi! kwi1 kwi! kwi!.
 
Yap, i said it !

Mnyika siasa zake kama Mrema, (yupo kwenye siasa kama geresha)
Slaa za kwake ni za kikabila kabila, !
Mbowe (huyu mchafu na uchafu wake hata sijui niuanzie wapi)

Haya wee mwanawane, kaeni mkao wa kula..More info to come !

mwanzoni ulikuwa unaleta hoja mbadala ambazo zilikuwa zinasababisha tufikiri, na ulikuwa unawasha moto wa fikara hapa. Baada ya kupotea kwa muda uliporudi umerudi ukiwa umechagua upande; bahati mbaya umechagua upande si kwa sababu ya uzuri wa hoja zao na matendo yao bali umechagua upande kama vile bendera inavyofuata upepo ili na wewe uonekane unapepea.

Well, kila mtu hana budi kufanya uchaguzi, na wewe umefanya wa kwako. Mwanzoni nilikuwa nafurahia kufungua kila unachosema, but the past week, siyo tu umenikatisha tamaa, lakini umenifanya niamini kuwa hoja zinaposhindwa, wao huleta vioja!.

Good luck!
 
Sidhani kama unaweza kuamini maneno ya mtu mwingine zaidi ya kwako ! Na hicho sio kibaya, imekuwaje hadi umefikia conclusion ya kusema nimekukatisha tamaa, ? umejua nilichotaka kusema kuhusu hao niliowataja ? tutachunguza kuku wote (majike na madume) majogoo, njiwa kwa kanga, mbuzi kwa kondoo, .......! na hao ni akina nani wanaoleta vioja ? kama mimi peke yangu nilileta kioja, then crucify me by myself na sio mwingine !

samahani kama umepoteza taste ya kusoma posts za kada !
 
Naona sasa unaingia ushabiki hapa usiokuwa na kichwa wala miguu. Slaa kama siyo kuuvalia njuga ufisadi mkubwa uliofanywa BoT kweli tungejua uozo uliojaa pale uliosababisha Balalli kuikimbia nchi na Viongozi wengine kutotaka arudi Tanzania kwa wasiwasi ushahidi atakaoutoa utawahusisha katika kashfa ya BoT? Je, ufisadi uliofanywa BoT, Richmond na kwingineko ambao Slaa amekuwa mstari wa mbele kuupigia kelele unawagusa wachaga tu na siyo Watanzania wengine!? :confused:

Je, kama siyo Slaa mawaziri waliokuwa wanaohusika kwa namna moja au nyingine na kashfa ya BoT akina Mramma , Meghji na wengine si wangekuwa bado wanapeta tu na nyadhifa zao?

Slaa alipoongea aliongea kwa niaba ya Watanzania wote, naomba nifafanuli uozo uliojaa pale BoT unawagusa wachaga tu na sio Watanzania wote wa kila kona ya nchi yetu?

Wana JF naona kuna njama kubwa sana za kuvuruga majadiliano mazito yanayoendelea hapa kuhusiana na ufisadi mkubwa unaofanywa na viongozi mbali mbali wa siri kali, kama tusipokuwa makini basi hii JF itavurugwa ili tuache majadiliano yenye umuhimu mkubwa kuhusiana na ufisadi ambayo yanaingamiza nchi yetu.
[/color]

Asante kwa mchango wako !(HII NI REGARDS TO MAANDISHI YA BLUE)
Lakini nafikiri theory kama zako za kusema kwamba viongozi waje ili kutibua michango na mwenendo wa threads IS REALLY RIDICULOUS ! Na nafikiri ulichosema ni signal kwa baadhi ya wananchi kutokuwa na imani na viongozi wao ! Kwa nini nasema hivyo, ina maana member wa kawaida kama KadaMpinzani binafsi hawezi kuja kuibua hoja kama hiyo niliyoibua ili kuleta mitazamo tofauti ? Au ndio unajaribu kusema mimi ni kiongozi, au nimetumwa na kiongozi ? Kwa kweli huo mtazamo wako ni wa kiutumwa na sidhani kama unapaswa kuigwa ! Lakini sitokushangaa maana nafikiri mawazo haya yako huanza chini hadi hufikia kwenye system, because last time i checked hata mtoto wa darasa la saba alipomuuliza EL swali katika hotuba yake na wananchi jamaa wa usalama walimfuatilia usiku kucha na kudai kwamba the boy was planted, THAT TOO TO ME SEEMED WAAYYYYYYYY BEYOND RIDICULOUS ! Anyway the point am trying to make here, in kwamba haiitaji mtu kuwa kiongozi kuja kuvuruga mada (kwa mtazamo wako umesema watu wanakuja kuvuruga mada even though sijui ni vigezo gani haswa ulivyotumia kusema ulichosema) but any ordinary person can do it, YES EVEN ORDINARY PEOPLE CAN DO IT ! So, lets have faith back to ourselves and attack me for me, na sio kuvuruga viongozi wetu wengi wao ambao usiku na mchana huangaikia taifa huku wengine wachache wakifilisi taifa !
 
Hata ordinary people ni lazima wafikirie wanapotoa kauli, wasiongee tu kama kasuku. Slaa kusimama kidete hadi kuanika hadharani uozo uliojaa BoT ni ushujaa, nasema ni ushujaa kwa sababu hata Bungeni alitishiwa na Sitta kwamba angemfungulia mashtaka kwa kuzusha uongo dhidi ya tuhuma za BoT na Slaa alipata vitisho vya kutishia uhai wake, lakini hakuogopa akaendelea kupiga kelele hadi Watanzania tukagundua uozo uliojaa pale BoT tena katika muda wa mwaka mmoja tu wamekupua shilingi 133 bilioni, fikiria kama Govt ingeamua kufichua uozo uliojaa pale kwa kuruhusu ukaguzi ufanywe kuanzia mwaka 2000 mpaka 2006 badala ya 2005/2006. Watanzania si tungelia machozi kwa jinsi ufisadi ambao ungegundulika umefanyika katika kipindi hicho.

Unaposema kwamba yeye uongozi wake ni wa kikabila hakuna ushahidi wowote wa kuthibisha hilo. Nimekuuliza je, kama Slaa uongozi wake ni wa kikabila uozo aliouficha pale BoT unawagusa wachaga pekee yao? lakini hukujibu, je aliposimama kidete dhidi ya mafisadi wa Richmond alikuwa anatetea maslahi ya wachaga pekee yao? unaposema Slaa uongozi wake ni kikabila unamaanisha nini hasa? Tufafanulie ili tukuelewe.

if you don't have anything important to say it is better to keep quiet rather than saying anything that you don't have any evidence to support your arguments. Slaa machoni mwa Watanzania wengi anaonekana ni shujaa wa kutetea maslahi ya Watanzania wote bila kujali kabila zao, kama una ushahidi tofauti na wengi tunavyomuona Dk Slaa basi ulete ushahidi huo hapa ukumbini badala ya kuandika porojo.
 
Mkuu wangu Kada, heshima mbele ndugu yangu sijui kinachoendelea behind hii ishu, lakini viongozi safi wa taifa letu ni lazima tuwape heshima zao kama inavyotakiwa, na hasa Dr. Slaaa, ninasema hivyo kwa sababu zifuatazo,

1. Mimi nilikuwa JKT Oljoro, ambako sio mbali sana na Karatu, ambako tulikuwa tunaedna kucheza mpira wa miguu kila wakati, na hata kambi yetu ilikuwa na mashamba kule kwa hiyo mara kwa mara tulikuwa tukienda kule na kukaa kwa zamu za miezi, ninajua kuwa wananchi wa kule wanampenda sana huyu mkuu, wala sio ishu kabisa, kutokana na uongozi wake shupavu kule jimboni, toka akiwa kanisani.

2. Yeye alikuwa CCM, yalikuwa ni makosa ya Mkapa, akiwa rais yaliyomfanya Dr. Slaa ahamie upinzani, kamati ya kutathmini na kupendekeza wagombea ubunge wa CCM ilikuwa imemchagua Dr. Slaa kuwa apewe nafasi hiyo na cc, mkapa kwa ujeuri wa makusudi akaamua kuliengua jina la Dr. Slaa, na kumuweka rafiki yake nafikiri ni Quaress, ushauri wote aliopewa kuwa huyu mtu wake hawezi kushinda, akaukataa, matokeo Dr. Slaa, akaingia upinzani na kushinda kiti kile cha ubunge mpaka leo.

3. Dr. Slaa, sasa hivi ni mmoja wa viongozi wachache sana wanaoheshimika sana na hata uongozi wa juu na chini wa CCM, na hasa wabunge kutokana na accuracy ya hoja zake, huwezi kumkuta kiongozi yoyote wa juu wa CCM akimponda Dr. Slaa in private, ukilinganisha na kina Mrema, au Mtikila, ni kwa sababu ni kiongozi makini sana.

Sasa kwa kweli sielewi haya malumbano yalikotokea na yanakokwenda, lakini nimeshitushwa kuona Dr. Slaa akijadiliwa kwa lugha ambayo kwa kweli hastahili kabisaa, yeye ni mmmoja wa viongozi wachache sana wa taifa letu, ambao kuwepo kwao bungeni kunatoa changamoto nzito kwa viongozi wengine wote kuanzia wa upinzani mpaka CCM, kufikiria mara mbili ni kwa nini wapo kule bungeni. sina mpango wa kujiunga na haya malumabano, lakini please tuwape heshima viongozi wanaostahili heshima kama Dr. Slaa.

Ahsante.
 
Hata ordinary people ni lazima wafikirie wanapotoa kauli, wasiongee tu kama kasuku. Slaa kusimama kidete hadi kuanika hadharani uozo uliojaa BoT ni ushujaa, nasema ni ushujaa kwa sababu hata Bungeni alitishiwa na Sitta kwamba angemfungulia mashtaka kwa kuzusha uongo dhidi ya tuhuma za BoT na Slaa alipata vitisho vya kutishia uhai wake, lakini hakuogopa akaendelea kupiga kelele hadi Watanzania tukagundua uozo uliojaa pale BoT tena katika muda wa mwaka mmoja tu wamekupua shilingi 133 bilioni, fikiria kama Govt ingeamua kufichua uozo uliojaa pale kwa kuruhusu ukaguzi ufanywe kuanzia mwaka 2000 mpaka 2006 badala ya 2005/2006. Watanzania si tungelia machozi kwa jinsi ufisadi ambao ungegundulika umefanyika katika kipindi hicho.

Unaposema kwamba yeye uongozi wake ni wa kikabila hakuna ushahidi wowote wa kuthibisha hilo. Nimekuuliza je, kama Slaa uongozi wake ni wa kikabila uozo aliouficha pale BoT unawagusa wachaga pekee yao? lakini hukujibu, je aliposimama kidete dhidi ya mafisadi wa Richmond alikuwa anatetea maslahi ya wachaga pekee yao? unaposema Slaa uongozi wake ni kikabila unamaanisha nini hasa? Tufafanulie ili tukuelewe.

if you don't have anything important to say it is better to keep quiet rather than saying anything that you don't have any evidence to support your arguments. Slaa machoni mwa Watanzania wengi anaonekana ni shujaa wa kutetea maslahi ya Watanzania wote bila kujali kabila zao, kama una ushahidi tofauti na wengi tunavyomuona Dk Slaa basi ulete ushahidi huo hapa ukumbini badala ya kuandika porojo.

angalia maneno mekundu ! Hadi hivi sasa sijaelewa wewe na mwanakijiji mmetumia vigezo gani kujudge outcome ya ninachotaka kuandika wakati hata sijawasilisha ninachotaka kuandika LAKINI NASHANGAA PUU CONCLUSION ZIMEFIKA MEZANI WAKATI HATA KUKU HAJACHUNGUZWA.! mwake humu kweli ? kama maneno yako matatu ya katika hayo maneno mekundu yanavyosema, ungesubiri nifafanue ili muelewe na haikuwa "safi" kwako wewe kufikia uamuzi uliosema wakati hata hujaelewa nini nilichotaka kusema !
 
are we speculating kwamba Dr. Slaa ni malaika ?? Sasa subiri niende kwenye mafaili !
 
KadaMpinzani elezea ulichotaka kuelezea tujue na kuweza kuchangia , bila hivyo utatutia shaka - mimi nina shauku ya kutaka kujua ufisadi wa DR. Slaa kwani hadi sasa namchukulia mmoja wa Viongozi safi na mwenye uchungu ni nchi hii.
__________________
 
are we speculating kwamba Dr. Slaa ni malaika ?? Sasa subiri niende kwenye mafaili !

Hatuna malaika hapa, ila tuna binadamu wenye nia njema na nchi yetu na watu wake. Kati ya binadamu hao kuna wachache km Mr. Slaa ambao kwa sasa wanaheshimiwa na Watanzania wengi. Mr. Slaa amejitolea na kuweka kifua chake mbele ktk kupambana na ufisadi, nategemea utaunga mkono kwa hilo km unaamaini ufisadi ni adui wa maendeleo yetu.
Punguza mzunguko mrefu wa maneno, tupatie huo upande mwingine wa Mr. Slaa km ulivyoahidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom